Msuluhishi
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 248
- 198
Chile, nimependa maelezo yako. Ningeweza kuchangia mengine hapo ila muda wangu hautoshi kwa sasa. Ila nitaeleza kidogo mawazo yangu kuhusu OAU kugawa kamati zake na TZ kupata ile ya Ukombozi. Ukweli ni kwamba si nchi zote wanachama wa OAU walitaka hii kamati iundwe. Kamati hii iliundwa kutokana na ushauri na msukumo wa Mwalimu. Bila Mwalimu hiyo Kamati, hata kama ingeundwa, isingefika popote. Mwalimu aliamini kwa dhati kabisa ya moyo wake kwamba Afrika ilikuwa na jukumu la kuikomboa sehemu ya Afrika iliyokuwa bado inatawaliwa. Nchi nyingine nyingi ziliamini kwamba hilo ni jukumu pekee la wananchi wa nchi hizo! Hata Kenya na Malawi, kwa mfano tu, viongozi wao waliamini hivyo. Hata kama OAU ingekataa kuanzisha Kamati ya Ukombozi, Mwalimu na viongozi wengine kama Obote, Kaunda, Sekou Toure, Haile Selasie, yule aliyekuwa Rais wa Misri, etc wangeanzisha kamati kama hiyo kwa nia hiyo hiyo. Tanzania kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo kulitokana na juhudi za Mwalimu za kuianzisha kamati hiyo na siyo kwa sababu tu kwamba ilipendekezwa na OAU.NI kweli, Nyerere kafanya mambo makubwa sana tena sana ukilinganisha na Mandela!!
Wakati Nyerere alikuwa ni mpigania uhuru wa Afrika Mandela hakupata fursa ya kuonesha kwamba alikuwa ni mpigania uhuru wa Afrika na kwahiyo kilichopo kwenye kumbukumbu ni upiganaji wake dhidi ya nchi yake!
Hata hivyo, kwa wakati ule hakuwa na namna zaidi ya kuipigania nchi yake ambayo bado ilikuwa kwenye minyororo ya makaburu!!
Lakini pamoja na yote hayo suala la kuunda Truth & Reconciliation Commission si jambo la kupuuza hata kidogo na sina shaka hili ndilo lililompa sifa nyingi Mandella!!!
Hata kama Msumbiji walikuwa na kitu kama hicho bado Mandella hakulazimika kufuata nyayo za Msumbiji!!!
Hata kama angehubiri akuanzae mmalize bado Mandela angepata support kubwa sana kutoka kwa wananchi wa Afrika Kusini! Hawa wananchi bado walikuwa na madonda mabichi ya moyoni yaliyotokana na udhalimu wa Makaburu!!!
Ingekuwa ni rahisi sana kwa sababu suppression kubwa ya Makaburu ilikuwa mijini; tena kwa kiasi kikubwa ni kutoka jiji lile lile kubwa kuliko yote!! Hapa Mandela angepata support kubwa sana kama angeamua "akuanzae mmalize!"
Kwanza kuna tofauti kati ya Truth & Reconciliation Commission ya Msumbiji na ile ya South Africa!
Kwa kumbukumbu zangu, Tume ya Mapatano Msumbiji iliundwa baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya RENAMO & FRELIMO! Kwavile sina uhakika sana am ready to be corrected with evidence lakini naweza kutumia logical argument ku-support madai yangu!!!
FRELIMO hawakuwa na sababu ya kuunda Tume ya Mapatano ya kuwasuluhisha na Wareno kwa sababu Mreno Msumbiji hapakuwa kwake na alitakiwa kuondoka na yule atakayebaki abaki huku akijua Msumbiji halikuwa koloni la Wareno tena!!!
Na kweli, Wareno waliondoka na kurudi Ulaya haidhuru hata kama wapo waliokuwa wamebakia!!!
Sasa kama ni Tume ya Mapatano kati ya RENAMO na FRELIMO pamoja na wafuasi wao; katu huwezi kuilinganisha na ile tume ya Afrika Kusini!
Wakati tume ya Msumbiji ilikuwa ni kuwapatanisha ndugu... Waafrika kwa Waafrika wasahau waliyofanyiana wao kwa wao, ile ya Mandela ndani ya Afrika ya Kusini kimsingi ilikuwa ni kuwafanya Waafrika wasahau unyama wote waliofanyiwa na wageni... Makaburu kutoka Ulaya!
Si jambo dogo hili hata kidogo!!!!
Wakati pasingekuwepo ile tume ya Msumbiji basi Waafrika wangeendelea kuuana wao kwa wao!! Lakini kama isingekuwepo ile ya Afrika Kusini; ambao wangeathirika zaidi ni Makaburu kwa sababu walikuwa outnumbered kwa kiasi kikubwa.
Hata Kibaraka wao Chief Mangosuthu Buthelezi asingeweza kuwasadia kwa sababu wafuasi wa Inkatha Freedom Party
ambao walikuwa tu Durban nao walikuwa outnumbered kwa mbali sana na wafuasi wa ANC!
Lakini pamoja na yote hayo... Mandela akasema let bygone be bygone na kuamua kuunda Tume ya Mapatano ambayo kimsingi ni kwa ajili ya kupatana na wale wale waliomweka korokoroni kwa miaka 27!!!!!
Si jambo dogo hilo hata kidogo!!!!
Pamoja na yote hayo, Mandela anaamua kushirikiana serikalini na wale wale waliomweka ndani kwa miaka 27... si jambo dogo hili!!
Pamoja na yote hayo, Mandela anampa cheo cha Uwaziri wa Mambo ya Ndani (mnaweza kunisahihisha kwa sababu sikutaka ku-verify) Chief Mangosuthu Buthelezi, kiumbe wa Kiafrika ambae wazi wazi alikuwa akiihujumu ANC... si jambo dogo hili!!!
Na ile ilikuwa ni truth commission kweli kweli manake kila kitu kilikuwa wazi!
Bado nakumbuka na Kiingereza changu cha Form I nilivyokuwa namfuatilia Winnie Mandela Live wakati akihojiwa hadi akanifanya nitafute dictionary kufahamu neno "ridiculous" ambalo Winnie alikuwa akilitumia mara kwa mara wakati amekalishwa kitimoto!!!
Si jambo dogo kumwacha mke wako nae awekwe kitimoto tena mbele ya kamera za televisheni!!!
Kwahiyo alichokuwa amefanya Mandella is more than kufanya kile ambacho kilifanywa na Msumbiji bali alifanya jambo ambalo lilihitaji kitu kingine la ziada!!!!
To sum up, ingawaje nakiri Nyerere amefanya mambo makubwa kwa Afrika kuliko Mandela lakini bado Mandela nae ana-deserve heshima anayopata na wala hajapata kwa upendeleo!!
NI bahati mbaya sana dunia haifahamu mchango wa Mwalimu ingawaje kwa dunia siwezi kushangaa kwa sababu Mwalimu alikuwa anawasaidia waafrika wenzake na nje ya Afrika it's none of their business!!! Uchungu wangu ni pale ambapo hata Afrika yenyewe inapoonekana kutofahamu mchango huu wa Mwalimu!!!
Lakini ngoja niweke kumbukumbu sawa kwa manufaa ya vizazi vyetu manake wengi huwa hatulizungumzii vizuri hili jambo!!
Pamoja na kwamba tangu mwanzo Mwalimu alionesha kusaidia harakati za ukombozi, lakini mengine mengi yaliyofuata alikuwa anatekeleza kazi aliyokuwa amepewa na OAU.
Baada ya OAU kuundwa, pia ziliundwa kamati mbalimbali kwa ajili ya kufanikisha na kutatua changamoto mbalimbali barani Afrika! Kwa mfano, kulikuwa na Kamati ya Viwanda (and something) ambayo Makao Makuu yake yalikuwa Gaborone, Botswana!!!
Tanzania tukatwishwa zigo la ukombozi ambapo Kamati ya Ukombozi ilikuwa na makao yake makuu Dar es salaam!!!
Main goal ya Kamati ya Ukombozi ilikuwa ni moja: kuhakikisha nchi zote zilizokuwa chini ya ukoloni nazo zinapata uhuru! By the time, nchi hizo zilikuwa Msumbiji, Angola na Guinea Bissau!!
Na kweli, Mwalimu Nyerere aliifanya kazi hiyo kwa moyo mmoja na mara kadhaa kutumia raslimali za taifa ili mradi tu kuhakikisha lengo hilo linafikiwa na kweli likafikiwa!!
Nadhani Kamati ya Ukombozi ndie kamati pekee ya OAU iliyokuwa imefanikiwa malengo yake miongoni mwa kamati zingine zote!!!
Remember, Afrika Kusini haikuwa considered kama ilikuwa inatawaliwa! Ni kama Zanzibar... Zanzibar haiwi considered kwamba ilitawaliwa na Sultan at least baada ya ujio wa wakoloni wa Ulaya!!!