Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kuvunjia mkataba sio easy sana hasa kwa mishahara wanayopokea na hicho kitu either Glazers ama akitokea mmiliki mpya sidhani kama wataweza kukifanya maana inahitajika pesa si kidogo.

Mtu kama Martial akikataa kuondoka waangalie alternative yupo mwaka wa mwisho wa mkataba,Maguire wakati anatua alisaini mkataba mrefu sana nadhani unaisha 2027 huyo ndio wamtoe kilazima akikataa kuuzwa maana mishahara ndio inawatamanisha,Ralf alishasema wakati ndio anaanza kazi kuwa failure yetu kubwa imetokana pia na mikataba ya wachezaji.

Kuna muda unatamani uuze wachezaji mizigo ili ufanye replacement ila sasa mikataba inawabeba na wanajaza nafasi tu za wachezaji bila faida.


Navutiwa na anachokifanya Todd pale Chelsea mikataba mirefu ila mishahara sio mirefu,hapo hata wakilflop wanauzwa kirahisi,ila kwetu mtu mzigo anapokea €250k per week hata akikaa benchi hana hasara kwake.

Tutaona kama hiyo ruthless way inaweza kutumika.
 
EtH hafiki krisimasi, mark my word
 
hiyo timu yenu mnajitahidi tu kuwepo top 4 lakini hamuwezi pata kombe lolote kubwa
 
Hali tete

| Manchester United are operating under takeover uncertainly, strict FFP regulations which means they’re operating around £100m net spend in mind.


[via @MelissaReddy_].
 
UTAPELI HAUTAWAHI KUISHA


10hag want Sofiyan Amrabat


Nasikia 10hag ana connection nae huyu jamaa toka kipindi Cha nyuma
Ukiwa ushawahi kuishi Netherlands na unaweza kupiga danadana basi ushapata mkataba United.


Jokes aside, Amrabat mtu wa kazi chafu hana kuremba. Alinipotezea kiungo moja la kitapeli la £100m kwenye fainali ya.........
 
Tukutane July 22
 
UTAPELI HAUTAWAHI KUISHA


10hag want Sofiyan Amrabat


Nasikia 10hag ana connection nae huyu jamaa toka kipindi Cha nyuma
Ten hag hana mbinu, hana ushawishi kwa wachezaji, mchezaji yoyote anaesakwa na huyu kipara ni either

*Amewahi mfundisha (hii haina tofauti na Ex, simu moja tu kafika)

*Huyo mchezaji amewahi chezea ligi ya uholanzi

*Au ni mholanzi

Fuatilia sajili zake zote utaniambia
 
Cry more kijana acha kocha afanye kazi na anaowaamini tutamuwajibisha timu ikifanya vibaya.

Ni timu yetu ndio haina ushawishi kwani kukataliwa na wachezaji na kupigwa si kumezoeleka hata kabla yake kutua.

Kocha ana percentage nzuri kuliko wote waliopita unakaa na taarabu zako kila siku.


Cry more Cry more mzee humtaki nenda Al Nassr utarudi akishafukuzwa
 
Habari mpya zilizozagaa na za chini² toka kwa mtu wa karibu wa Ferdinand tunaweza kusikia update ya takeover muda wowote kuanzia kesho
Hii ndio muhimu kuliko zote. ..ila wakimpa yule muingereza imekula kwao. ..muarabu ndio habari ya mjini kwa sasa
 
Hii ndio muhimu kuliko zote. ..ila wakimpa yule muingereza imekula kwao. ..muarabu ndio habari ya mjini kwa sasa
Yule Muingereza mbona alishafeli bid yake ni illegal shareholders wangewapeleka Glazers na yeye mahakamani
 
hivo mtu anatolea wapi nguvu ya kusema Ten Hag sio kocha?

Mnakumbuma Amonia walivyotufunga goli msimu uliopita kwasababu ya kutojua wachezaji wasimame wapi wakiwa na mpira na wasipokuwa na mpira...

Maneno sio matendo moja ya waongeaji wakubwa wa theories Rafk Rangnick alipewa nafasi wote tuliona alivyoharibu kabisa...

Ten Hag amejitahidi kwenye vingi sana kuanzia tactical awareness ya wachezaji wetu... Sahizi unaona tusipokuwa na mpira wachezaji wanasimama maeneo sahihi .

Ni mtu sahihi na hii Aina ya mapira amecheza sababu wachezaji wa kucope na aina ya system yake hamna...

Tutafika au mmesahau tumemaliza nafasi ya 3... Kutokea kusema timu nzima iuzwe.

Hata akitaka wahilanzi 30 kama tutaendelea kuimarika awalete
 
Kocha wakawaida huyo ndo maana alipopewa bajeti kubwa hakufanya lolote Sasa wamempa bajeti kiduchu apambane sio kulialia
 
Kocha wakawaida huyo ndo maana alipopewa bajeti kubwa hakufanya lolote Sasa wamempa bajeti kiduchu apambane sio kulialia
Tatizo lenu hamtaki kuleta facts.

Msimu wa kwanza Gurdiola anatua City alipewa €216.25 akamaliza nafasi ya 3 akiwa hana hata kikombe cha kahawa. Je, hapo Fraudiola alifanya lolote? Au mnamuona EtH tu!

EtH msimu uliopita amepewa United iliyochoka vibaya mno ikiwa chini ya uongozi usioleweka, mezani akawekewa €243.28 kamaliza nafasi ya 3 na kombe la EFL. Hata Gurdiola hii ilimshinda.

Msimu wa pili wa Gurdiola waarabu wakaweka mezani €317m hakuna timu ingeweza kushindana na City maana waliweka levels mpya EPL: 100 points, kwasasa ubingwa wa EPL ukiutaka uwe na kikosi cha kupata points kuanzia 90.

EtH pesa ya usajili aliyopewa mpaka sasa ni €303.28m. Misimu miwili Fraudiola alitumia €538.25m / nusu bilioni na chenchi.

EtH aliwahi kusema "A coach can't perform magic."
 
Fun fact Antony 86£
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…