Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kama tuna selfish wingers wakisajili goal poacher ndiyo itakuwa hatari zaidi.

Kane ndiyo complete striker bora duniani. Kigezo cha umri hakina tija, ana misimu 2-3 kukiwasha EPL.
Kama ana misimu 2 ilitakiwa aende timu ambayo ina msingi tayari.

Hii yenu inayosema inajijenga itamuona mchawi
 
Kwanini mnamtoa Newcastle? Yeye hawezi kutoa draw au kufungwa angalau moja kati ya hizi?

1. Vs Arsenal (Home)
2. Vs Leeds (Away)
3. Vs Brighton (Home)
4. Vs Leicester (Away)
5. Vs Chelsea (Home)

Mimi swala la Top 4 sina wasiwasi nalo kabisa labda mpira unishangaze tu.
 
Sio mechi moja tu anaweza fungwa hata mechi 2 kati ya hizo, ila yeye tunamtoa kwa sababu walau anaonyesha yupo serious kidogo sio kama sisi wazee wa maji kupwaaa maji kujaaa.
Ukiangalia hata last 3game results unamuona Newcastle ameikamia top 4 tofauti na Utd yetu.
 
Ten hag anapaswa awe na roho ngumu kuleta mataji United.
1. Ajenge morali ya dak 90
2. Nidhamu na ushirikiano kwa wachezaji ndani ya pitch iko Wazi ndani ya box kila mchezaji anataka afunge yeye hasa forward zetu ( martial, rash, na anthony)
3. Asajili wachezaji wafia timu, napendekeza wenye sifa aina ya i) KANE, ii) DE JONG, iii) CHIESA, iv) FIRMPONG na CB na middle no# 10 mmoja...kwa msimu huu kaonyesha mwanga kwa tactics zake na baadhi ya sajili nzur hii ni optimistic about the future....binafsi namuunga mkono na nataka awe serious na kazi tunamtengemea.
NB: awatoe martial, Maguire, elanga, fred, woughost. All the best. GGMU
 
Mbona umemsahau Rashford mkuu?
 
Hyo namba mbili ni tatizo kubwa mno , solution yake ondoa wote wenye majina leta madogo kama Mitoma , alaf ndo ulete striker finisher kama Kane ndo utaona matokeo , Ila hao selfish waliopo Huyo Kane ni Nani boya atakuwa anamlisha afunge yeye alaf wao wasionekane kitu ambacho Ronaldo mwenyewe kilimshinda sababu ya majungu ya hao madogo , kama Kane akija akifikisha magoli 15 kwenye ligi basi ni mwanaume , Antony , Rashford , Sancho , Martial etc wote wanataka wafunge
 
Kibarua cha Kuirejesha Manchester United juu kimekuwa kigumu sana..

naweka akiba ya maneno ila..Only Pep Can Do That..

Our Ten Hag tutamuonea tu..

huwezi beba ubingwa wa EPL na wachezaji dizaini ya Sancho, Rashford, Antony, and co..

Manchester United inahitaji 5 Worldie kubeba EPL..as of now ni Only Casimiro..ndie World Class Player..


yule bwana hamis77 huwa tunamuona snitch ila kiuhalisia yupo sahihi..

Imagine Manchester United wame spend karibu £250M.. ila mpira bado hauna uelekeo..

Mchukue Rashford mpeleke Real Madrid, Bayern Munich, Manchester City, PSG, tuone atamweka nani benchi?

Safari bado ni ndefu..tuwe na subira..ingawa bila watu sahihi wa usajili safari ni ndefu zaidi..
 
7 hag kaonesha mwanga gan ambao waliopita hawakuonesha?

Katika sajili zake Ni zipi unaweza kusema zimelipa ukimtoa Martinez?
Casemiro na Eriksen usiwahesabie hao Ni wazee ,Kama Eriksen hata dk 90 hawez kumaliza, casemiro tumeona alivyochoka had Sasa
 
Hapo kwa Kane naomba niendelee kumkataa kwa nguvu zangu zote.

Mosi,Manchester ni Team inayojijenga,yaweza chukua miaka 2 tena tuweze kukaa katika nafasi yetu ya mwanzo (Enzi za Sir Alex).Kane anatakiwa kwenda team kama City au PSG huku kwetu tunamtafutia lawama bure.

Pili,Winger zetu zote ni self sana,sijui wakati wa usajili walifikiri nini ?.

Tatu Man inahitaji wachezaji wasiopungua watano watakaoingia moja kwa moja kikosi cha kwanza (first eleven).Ukimnunua Kane unaweza kutumia 110 hadi 130 Million hii itapunguza budget yetu na hivyo kuathiri maeneo mengine muhimu kama mlinzi wa kati,kulia,kiungo na mshambuliaji wa kulia.

Mwisho lazima mtambue wachezaji wa kiingereza wanauzwa ghali sana.Kane angekuwa Mdachi au mfaransa bei angeuzwa 30 or 40 million only.Mchezaji kama Erickson,Casemiro,Varane ni 30 or 32 hawa wapo katika kumalizia mpira wao wa kiwango cha kabla hawajatimkia Italy or USA.Varane ni mchezaji wa kiwango cha juu lakini muda mwingi anakuwa nje ya uwanja kwasababu majerui sasa hii imesababusha tatizo kubwa upande wa ulinzi.Wakati tunaka yule kubwajinga aondoke lakini pia majeruhi wa mara kwa mara waondoke pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…