Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Sure thing,sijui solskjaer anamwonea aibu Rashford.
Kimsingi Rashford alipoteza sana mipira.
 
Zote zilikua failed project, ipi ilifanikiwa tangu aondoke Fergie?
hakuna project iliyofanikiwa japo mourinho huwezi sema ni filed project maana alitupa europa na kutuweka nafasi ya pili.....

Nadhani watu wajuu wa kutoa maamuzi sio wazuri ngoja tuone hali itakuwaje kwa ceo mpya na kina Fletcher
 
Dirisha la usajili lililopita;

1. Pellistri (Non starter)

2. Amad (Non starter)

3. Van De Beek (Non starter)

4. Cavan (Eventual starter)

5. Telles (Non starter)

Objective ilikuwa nini kuleta wachezaji wote wanaishia benchi tu?
 
Dirisha la usajili lililopita;

1. Pellistri (Non starter)

2. Amad (Non starter)

3. Van De Beek (Non starter)

4. Cavan (Eventual starter)

5. Telles (Non starter)

Objective ilikuwa nini kuleta wachezaji wote wanaishia benchi tu?
Yani hii timu bwana, inanishangazaga mno aisee 😀 ina wachezaji bus zima la mkoani kutoka Dar kwenda Mwanza linajaa kabisa ukiondoa siti ya dereva 😆 hata Ole Guna hapati siti humo 😅 labda waforce apakatwe na mzee baba Cavani 😂
 
Ole na man u ni failed project mkuu.....ataendelea kujificha kwenye kichaka cha rebuild hadi mwaka 2024 na hakuna kombe atakalobeba......fainal ya jana ilikuw nyepesi sana tena sana.
Ole na Man. Utd siyo project iliyofeli, next season project inaendelea tena cha muhimu Ole apewe watu anaowahitaji kama anavyosikika kwenye interview zake kuwa dirisha hili atahitaji karibia watu watatu watakaoanza kikosi cha kwanza.

Fainali tuliyofungwa isiwe sababu ya kusahau kazi kubwa aliyofanya Ole msimu huu, yaliyotokea yote ni sehemu ya mchezo. Wote tunajua timu yetu ilikuwa haina uwezo wa kubeba EPL mbele ya City, UCL tulitolewa kwa timu yetu kufanya makosa yanayojirudia kwenye safu ya ulinzi.

Tukirudi kwenye fainali ya Europa ulitaka Ole afanye nini zaidi ili abebe hilo kombe? Kama ni kikosi alipanga kizuri kwa lengo la kutafuta ushindi. Kwenye sub pia alifanya vizuri sana kwa kujua aina ya mchezo na umuhimu wake, Ole alifanya vizuri kama kocha, ulibaki mchezo tu kuamua na wala muda haukuwahi wala kuchelewa Villareal akawa bingwa.
 
Kwani sisi tunazungumzia kipindi gani, tunazungumzia kipindi hiki cha Corona, sub 5 kwenye muda wa kawaida na sita kwenye extra time
Kwani kigezo wa kocha bora lazima abadilishe wachezaji? kwangu mimi bado kocha bora kama kapatia first 11 na tactical right dakika 90 yule wakubadili tu basi kakosea kupanga, tuache hili kulikuwa na nani wa kuingizwa toka bench katika wale wachezaji? nimesoma labda kosa kumtoa greenwood badala ya Rash basi hakuna jipya bench.
 
Wewe ukiwa kocha utabugizwa tu kwa sababu una perception mbaya juu ya soka
Hata kocha apatie namna gani , factors zinazomlazimu kocha kufanya sub ziko nyingi na nyingi kati ya hizo ziko nje ya uwezo wake
  1. Kwa asili kuna wachezaji amabao sio consistence
  2. Bahati mbaya siku hiyo mchezaji unayemtegema anaweza akashuka form
  3. Kwa bahati mbaya timu pinzani inaweza kumkamia na kumfanya asicheze kabisa nje na matarajio
  4. Anaweza mchezaji unayemtegemea akakamia kucheza sana na kuchoka mapema
  5. .............................??
  6. ...........................??
Hizo sababu zinatosha kumfanya kocha alazimike kufanya sub
 
Nime-like

Ole kazi alioifanya inaoneka na itazidi kuonekana. Mandezi mnaomponda ole wala msichoke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…