Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ole sijamwelewa kumpeleka Rashford pembeni na Martial kati. Kwa mawazo yangu Rashford angekuwa kati na Martial ni mzuri sana ikitokea pembeni.
Tuwe na msimamo

Rashford amecheza hiyo nafasi kipindi martial kaumia na ilikuwa ni upuuzi mtupu

Martial anacheza vizuri kwenye hiyo nafasi kushinda Rashford

Rashford atokee pembeni
 
Leo tunacheza vizur mbona, tunatengeneza nafasi na tukiwa hatuna mpira tunakaba vizur

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo ndio utagundua sasa kila mtu anautazama mpira kwa macho yake. Binafsi naona timu imecheza vizuri sana kipindi cha kwanza,sikutegemea kabisa. Ni kama vile wachezaji wameanza kuelewana. Fred anazidi kunifurahisha siku hadi siku.
 
Mweleze huyo, Mata anakabia macho, timu ikishambuliwa inakua kama tupo pungufu

Sent using Jamii Forums mobile app
Na ndio kinacho mbeba Lingard. Huyu dogo hutimiza majukumu yote anayoelekezwa na makocha.
Kumbuka kipindi cha Ferguson yeye alikuwa anamkubali sana Danny Welbeck kwakuwa dogo alikuwa anafanya kazi yake kikamilifu japo alikuwa ni mtu wa kukosa magoli sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu msimu unaanza Martial amekuwa akicheza katikati na Rashy anatokea pembeni, hii haizuii sometime wao kupishana, yaani Tony kwenda pembeni na Rashy kuingia kati

Hata timu ya Taifa Rashy amekuwa akitokea pembeni kushoto ambapo anacheza vizuri zaidi

Tumeshafanya experiment ya Rashy kucheza center forward kipindi Tony ni majeruhi, hii experiment ilishindwa vibaya mno

Tunapaswa kupata goli la pili ili tusiwe na pressure kadiri mechi inavyoelekea mwishoni
Tuwe na msimamo

Rashford amecheza hiyo nafasi kipindi martial kaumia na ilikuwa ni upuuzi mtupu

Martial anacheza vizuri kwenye hiyo nafasi kushinda Rashford

Rashford atokee pembeni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…