Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ole aliposema hana nia ya kupigania ubingwa nilimuona kiazi kweli hii ilikuwa justification kwa Woodward kumsajili average squad.

Kufundisha timu kubwa kama Manchester halafu ukawa na projection za timu ndogo kama Burnley kupungukiwa akili.
Ndio maana anawapa mikataba wachezaji wa hovyo.
 
Mtu pekee anayeweza kuikoa Man United hapo ilipo ni Klopp, Guardiola na Mourinho.

Still ninaamini Man United kumfukuza Mourinho ni katika Makosa makubwa sana kuwahi kuyafanya kwenye karne hii ya 21
Subiri tushuke daraja kwanza ili wamiliki wauze timu, management itolewe, kocha afukuzwe na wachezaji waoneshwe mlango wa kutokea.

Kubadili kocha kwa sasa itatupa short term orgasm ataturudisha nafasi za kushindania Europa.

Msimu utakaofuatia atanyimwa hela kama Mou alivyokataliwa kupewa winger na beki hadi akafukuzwa.

Wacha tushuke daraja kwanza, italeta attention kwa wamiliki.
 
Kocha apewe muda... klopp imemchukua misimu mitano kuwa hapa walipo... kocha wa spurs msimu wake wa saba huu nothing ole aachwe ajenge TEAM.. apewe muda
 
OGS naona kama hajitambui, alivyopewa timu tu akamuongezea mkataba Smalling na Lingard, alafu Smalling kamtoa kwa mkopo, sasa kama aliona uwezo wa smalling ni mdogo kwann alimuongezea mkataba?
Kiufupi timu yetu ina matatizo mengi sana na kadri siku zinavyosonga yanazidi kuongezeka, kuanzia kwa kina Ed Wood kule juu, manager mpaka wachezaji, tuna michezaji mingi tumeisajiri haina hadhi ya kuichezea Man Utd
 
Mtu pekee anayeweza kuikoa Man United hapo ilipo ni Klopp, Guardiola na Mourinho.

Still ninaamini Man United kumfukuza Mourinho ni katika Makosa makubwa sana kuwahi kuyafanya kwenye karne hii ya 21
Klopp hawezi kuokoa jahazi lililopo. Hizo kazi waachie Mou, El Chollo, Ancelloti na Hiddink. Klopp atahitaji apewe muda na wkt timu inazidi kupotea.
 
Kocha apewe muda... klopp imemchukua misimu mitano kuwa hapa walipo... kocha wa spurs msimu wake wa saba huu nothing ole aachwe ajenge TEAM.. apewe muda
Spurs na United ni vitu viwili tofauti kabisa..ndani ya hiyo miaka saba ya spurs hata ukiangalia spending zao ni tofauti kabisa na United na hata expectation za mashabiki wa spurs na United ni tofauti kabisa..Spurs wanafanya vibaya sana na wao recently,je umeona kuna pressure kubwa kama iliyopo United??
 
Kocha apewe muda... klopp imemchukua misimu mitano kuwa hapa walipo... kocha wa spurs msimu wake wa saba huu nothing ole aachwe ajenge TEAM.. apewe muda
uongozi wa manchester united kwa kushirikiana na mashabiki wengi wetu kwa kiasi kikubwa tunamhukumu mwalimu kwa kuangalia zaidi matokeo aliyoyapata.

namaanisha ili kocha apewe muda wa kutosha ni lazima awe na tiketi mkononi ya kuipeleka manchester united kwenye michuano ya ligi mabingwa haijalishi kwa kupitia mlango wa nyuma (nakusudia europe league kama alivyofanya jose mourinho).

liverpool ya miaka mitano iliopita haikuwa ajabu kiupande wao kukosa kushiriki ligi ya mabingwa kimapato na pia ndani ya uwanja ndio maana jurgen klopp alipewa muda na hivyo hivyo kwa upande wa tottenham hotspurs japokuwa na wao wameshaufahamu utamu wa ligi ya mabingwa ndio maana andre villas boas alipofanya vibaya kibarua chake kiliota nyasi.


manchester united pamoja na kampuni ya adidas walisaini mkataba wa vifaa vya michezo wenye thamani ya paundi millioni 750 kwa kipindi cha miaka 10 (wastani wa paundi millioni 75 kwa mwaka), inasemekana kwenye mkataba huo kuna kipengele wameekeana cha kupunguza asilimia 30% (kutoka kulipwa millioni 75 hadi millioni 53 kwa mwaka) ya malipo endapo klabu itashindwa kushiriki ligi ya mabingwa kwa miaka mfululizo kama nitakuwa sipo sahihi wadau wengineo watakuja kunisahihisha.

usisahau pia klabu inawakata asilimia 25% ya mishahara wachezaji pindi klabu inaposhindwa kushiriki michuano ya uefa kila mwaka, hii inaonyesha dhahiri klabu haipo tayari kupoteza mapato yake kwa hoja dhaifu ya kujenga timu.

wewe jenga timu yako uwanjani lakini hakikisha unatupa tiketi ya uefa kila mwaka na hiki ndicho wanachokiwaza mabeberu waliovamia mchezo wa soka.

tujaalie leo hii timu ya liverpool ifundishwe na steven gerrard ambaye tayari wajinga wa kiingereza wanampigia upatu arithi mikoba ya fundi jurgen kloop halafu washindwe kushiriki uefa mfululizo unadhani wale wamarekani wataendelea kumpa muda wa kutosha wa kuendelea kujenga timu?
unajua kama liverpool wanaelekea kwenda kusaini mkataba wa kufuru na kampuni fulani kubwa duniani?
beberu hana rafiki kwenye fedha​
 
Huyo ed ndio kirusi sasa
Kuna tatizo pale United ambalo muda mwingi nimekuwa silielewi kabisa.

Kama unakumbuka kipindi cha Mou, ule msimu wa Zlatan, timu ilikuwa inatengeneza nafasi nyingi sana za kufunga. Walikuwa wanafika hadi kwenye box na kutengeneza nafasi za wazi kabisa ila kwa wafungaji kulikuwa na uzembe wa kumalizia. Kipindi hicho tatizo kidogo lilikuwa upande wa mabeki. Kwa mazingira haya inamaanisha kiungo kilikuwa safi.

Ghafla leo tupo na Ole timu imekufa kabisa,kiungo sifuri,mbele kule ndio usiongee. Tumebaki na mabeki pekee.

Shida ni nini? Ni kile alichosema Neville kwamba timu inafanya maamuzi ya kukurupuka?
 
Matatizo ni makubwa sana.

Tukimshushia yote Ole tutamuumiza.

Tumuachie machache kwanza.

Kuwauza wachezaji wazuri na kubakisha makapi ni mzigo wake.

Kutoa recommendation ya kuwaongeza mikataba Lingard, Rashford, Jones, Young, Mata, Smalling ni matatizo yake.

Kukosa wachezaji sahihi ni shida za Ed.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…