Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ole anatuletea shida sana yani hatuwezi nilikiota mpira kabisa team yetu inabahatisha pasi 2 ya 3 imepotea....owky tunawachezaji poor so hata kuuchezea tu mpira tuoate suluhu ya 0 0 hatuwezi....mbona kipindi cha van gal hadi Phil Jones alicheza kiungo na timu pinzani tukazikamata......set up ya ole ni mbovu shida sio kiungo wala nini
 


De gea kasave Sana leo, kilikuwa kipigo cha mbwa mwizi kama De gea asingeridhishwa Jana na mpenzi wake
 
Mkuu tatizo linaanzia kwenye kiungo, huwezi kuchezea mpira bila kuwa na kiungo kizuri, utauchezea wapi sasa?😂

Unapomzungumzia LVG unazungumzia kocha bora na mzuri sana,sio mbabaishaji Ole. Ndio maana nilitamani baada ya Mou aje Carl Ancelotti au Antonio conte, huyu Ole tutapata aibu sana.

Game ya leo alipaswa kabisa kuanza Fred na sio Matic pale kati, Matic ni mzito hata kuufuata mpira. Kocha haelewi ni kujaribu jaribu tu😂😂😂
 
Sina cha kuongeza hapa.
 
Matone ya mvua yameshaanza kutupata.
bwana PTER baada ya kumalizika mechi ya man utd dhidi ya chelsea jose mourinho alizungumza maneno yafuatayo.

Chelsea were not compact defensively, too much space to play, not enough aggression on the ball, the defensive line, the midfield, the attack, they were not compact.
I think United will find it much more difficult to play against teams with low compact blocks, if the block is low blocks, it will be really difficult for them without pure striker"

wolverhampton 1 vs man utd 1
man utd 1 vs crystal palace 2
southampton 1 vs man utd 1
man utd 1(penalty) vs leicester city 0
man utd 1 vs astana 0
westham 2 vs man utd 0.

ukiondoa mechi ya chelsea hakuna mechi nyengine tuliofanikiwa kufunga goli zaidi ya moja.
baadhi ya wakati huwa namlaumu bila ya sababu ya msingi marcus rashford kumbe tatizo si yeye na wala lukaku hakuwa tatizo.

mtoto akiwa anakojoa kitandani anayepaswa kulaumiwa kwanza ni mzee kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.
 
Kumuuza lukaku tena bila mbadala ilikua kosa
 
4 2 3 1 ya Ole imefeli ahamie kwenye 4 3 3 au hata 3 5 2
 
Aisee genge la wahuni tupoo
Bado tu tunaendelea kujipa matumaini kuwa Ole Sendeka atatufikisha top 4


Chelsea ni mbovu lakini sidhani kama ndugu zetu Mwantesa Utd tutaenda popote chini ya Rashid Makame


Fumueni body ya timu nzima kuanzia Edwood Ward

Fumua kikosi chote na kusajili hata zaidi ya wachezaji wa8

Bila hivyo hata ashuke malaika bado tu mtakuwa mnatwanga maji kwenye kinu
 
Kuna kitu hapo kimeongelewa "Without a pure striker" hcho kipengele unatakiwa ukibold na rangi juu,
 
Hujambo hapo hospitalini kwa kulazwa sababu ya matokeo mabovu ya timu yako Mwantesa Utd?
 
Kawaida ya timu yetu, mmeacha matatizo ya msingi mmemtafuta wa kum bebesha mzigo matic
 
Mkuu mpira ni mchezo wa ajabu sana na unamaumivu sana... Nashukuru hata leo sijaenda kuangalia mechi yetu
Umefanana na mimi shabiki kindakindaki wa Chelsea nilikuwa napiga zangu zoezi tu sababu najua kabisa timu yangu ndiyo inajengwa upya so nilishajiandaa na lolote kuliko hawa ndugu zangu wanaojitesa bure tu hapa
 
Majirani mna hali mbaya sana,poleni next week mnakutana na Arsenal dah.
Sipati picha kwa hali kama hii mliyokuwa nayo alafu mnakutana na Man City,tutatafutana humu JF.
Man City ni ndugu yao hata wakifungwa haiwaumi sana sababu wanapata raha kuona kombe la epl linatua Etihard stadium kuliko kwenda Anfield
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…