Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Na kuondoka kwake kutaathiri timu uwanjani na sokoni

Woodward anabip kila mchezaji anatulia bila kujali muda.

Kupata msaidizi kashindwa au hataki maana haiwezekani dunia hii haina technical director wakufanya kazi Man united, ni woodward pekee anayeliamini hili
muda umeshatuonyesha muelekeo wa hii kadhia
  • hajapatikana technical diector kwa miezi saba tokea uanze mchakato
  • usajili umeendelea kuwa wa mashaka.
  • pogba amepandisha mashetani yake muda tunaomuhitaji aongoze ibada
 
kijamaa kimekuwa god father,
tetesi za bruno fernandez zimeishia wapi?
nafasi ya sita inatuhusu tena wallahi
Yaani Madrid wameshashusha majembe ya kutosha,sisi tupotupo tu na pre-season hii hapa..Huyo bruno tetesi zimekufa,saivi naona tupo kwa sean longstaff,Teilesmans

Hivi Rabiot si yupo free tu,kwa nini asije kutupa backup kwenye midfield??

Pogba naye anataka kusepa..damn..next season tusipokuwa makini tutapigwa na kuchakaa
 
nilijua mapema manchester united hawana target za uhakika hivyo basi wataendeleza tabia ya kubangaiza kila mchezaji kama ilivyo kawaida yao kila inapofika dirisha la usajili.

ok wachezaji inawezekana ni ghali sana lakini mbona madrid wanasajili, hivi madrid na united wana utofauti wowote kifedha?
madrid hawajahi kumkosa mchezaji wanayemuhitaji lakini kwetu sisi ni tofauti.

bajeti yako pengine ni ndogo sasa kwa nini unagombania kumsajili wan bissaka haliyakuwa thomas mounir thamani yake ni pound million 22?
 
Hiyo ndo pointi..

Mbona timu nyingine target zao wanazipata??..hilo ndo swali
 
akishaondoka unaletewa yule muingereza wa newcastle united
Longstaff, sidhani kama OGS amechoka kuifundisha United kiasi hicho, after all yule dogo ni defensive, na Pogba ni creative

Mbadala lazima atakuwa creative midfielder, probably tutaongeza nguvu kusainisha Bruno F, Ndombele na wengine wanaofanana na hao

Pogba ni janga pale United

Kinachofurahisha zaidi kiasi cha £120m+ kitaongezeka kwenye transfer budget kuongeza hela iliyopo

Kwa wale ambao wapo desperate Pogba abaki waniambie Pogba amefanya nini katika miaka yake 3 pale United zaidi ya kuleta sumu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…