Manchester United (Red Devils) | Special Thread

If we want to be like Man City we must invest heavily on matured Good players walau tuwe na vikosi viwili vya ushindani

Sent using Jamii Forums mobile app
True that..

Jana kikosi cha Man City kilichoanza dhidi ya Rotterdam kwenye FA kilikuwa na watu kama De Bruyne,Mahrez,Gundogan,Otamendi,Zinchenko,Walker,G.Jesus,Delph..na hawa wote hawakuanza gemu iliyopita ya Liverpool..hapa utaona ni kwa jinsi gani baadhi ya wapinzani wetu walivyo na vikosi vipana ambavyo ni strong tofauti na sisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Sancho walimruhusu kuondoka lakini walimzuia kusajiliwa na United,

Manchester United walitaka kumsajili Sancho

Sent using Jamii Forums mobile app
Walimzuia kusajiliwa moja kwa moja akitokea City lakini baada ya kwenda Ujerumani United wanaweza kumsajili bila City kuweka kizuizi lakini kwa Diaz ni tofauti, japo City wameshamuuza wamemzuia kiaina kwenda United akiwa timu nyingine.

Let's say Madrid wakitaka kupata angalau miioni 100 kwa kumuuza huyo dogo, United wakimtaka watalazimika kumuuza kwa milioni 140

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesikia tetesi za coutinho kutakiwa na united,kwa anayeweza kuthibitisha hii taarifa tafadhali
 
Uzi unakaribia kufika millennium

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha ngoja niufikishe millennium ya pili.


Kama sijasahau mwaka jana miezi ya 8 na 9 kulikuwa kuna fununu za Man U, kuteua DoF , na habari zilidai ifikapo January zoezi hilo litafanyika, anyway Jan haijaisha nisijisumbue bure.

Sasa basi inasemekana Man u hatutasajili mpaka DoF apatikane, hii isemekana lakini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa hesabu ya haraka haraka hapo asilimia 40 ya 140m ni 56m na asilimia 60 ya 140m ni 84m
 
.OLE Gunnar Solskjaer anajaribu kuteka akili ya kila mchezaji kwenye kikosi cha Manchester United ili wapambane kwa ajili yake. Kocha huyo wa muda, amekichukua kikosi chake na kwenda nacho huko Dubai kutafuta hali ya joto, huku wakijiandaa na mechi yao ngumu kabisa dhidi ya Tottenham Hotspur Jumapili ijayo.

Kwenye mtoko huo wa Dubai, Solskjaer amewaambia wachezaji wake kwamba habanwi mtu, kila mtu afanye anavyojisikia na kuwasisitiza kwamba jukumu la kuitafutia mambo mazuri Man United ni la kila mtu. Jambo hilo limedaiwa kuwafanya wachezaji wa Man United kuona kwamba sasa wanaheshimika na kusimamiwa kama watu wazima.

Kwenye ziara hiyo amekosekana mchezaji, Paul Pogba, lakini ataungana na wenzake baada ya siku mbili baada ya yeye kubaki England kufanyiwa matibabu kutokana na maumivu aliyopata kwa kuchezewa rafu na Jonjo Shelvey kwenye mechi dhidi ya Newcastle United. Man United imefikia kwenye hoteli ya One&Only Royal Mirage Arabian Court.

Solskjaer amekuwa akisifika kwa kubadili upepo kwenye klabu ya Man United tangu alipochukua mikoba ya kuinoa timu baada ya Jose Mourinho kufutwa kazi.

Wachezaji wameambiwa hivi, ratiba ya chai asubuhi ni saa 3, lakini sio lazima, mchezaji anaweza kwenda kupata kifungua kichwa muda wowote anaotaka mwenyewe. Solskjaer amewaambia wachezaji wake hakuna kufanya mambo ya kulazimishana, akifanya hivyo kuangalia akili zao kama watajiweka sana na kujiendeesha kama watu wazima.

Mastaa hao wa Man United wameambiwa kwamba kutakuwa na mazoezi magumu siku moja kwa siku na mlo wa mchana itakuwa lazima kwa wachezaji kula pamoja na ule mlo wa usiku, ambapo chakula kitakuwa tayari kuanzia saa 2 usiku

Baada ya hapo, Solskjaer amewaamini wachezaji wake na kuwaambia watafahamu wenyewe muda wa kwenda kulala na si kulazimishana kama watoto. Kocha huyo raia wa Norway ameipeleka timu yake kwenye ziara hiyo ili kuwafanya wachezaji wao wacheze kwa ajili yake na kupata matokeo.

Hadi sasa Solskjaer ameisimamia Man United kwenye mechi tano na kushinda zote, huku ikiwa kwenye timu hiyo kwa siku 20 tu. Wachezaji wengi wameonekana kurudi kwenye ubora wao, akiwamo Romelu Lukaku, ambaye alisema: “Yeah, nadhani sio mimi tu bali ni kila mchezaji. Nadhani kwa sasa tumekuwa sisi wenyewe na hakika ni jambo zuri kwa kila mchezaji kufurahia kucheza na kushinda mechi ni kitu muhimu. Sisi ni Manchester United na tutajaribu kuingia uwanjani na kushinda kila mechi.”

Kocha Mourinho aliweka utaratibu mgumu kwenye timu hiyo na kuwafanya wachezaji kutokuwa na amani katika kuitumikia timu. Lakini, Solskjaer amebadili kila kitu na kuwaongoza wachezaji hao kama watu wazima bila ya kuwawekea masharti ya kijinga. Wachezaji wameruhusiwa kushikirikiana kijamii, licha ya kwamba safari yao hiyo ya Dubai imelenga zaidi katika kufanya mazoezi ya ndani ya uwanja ili kujiweka fiti kabla ya kwenda kumalizia msimu. Solskjaer amewapa uhuru wachezaji wake ili kutambua akili zao kama wanaweza kujiongoza wenyewe kama wachezaji profesheno.
 
This is a true definition of a football coach....
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…