Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mimi pogba jamani namuona kama kwa nafasi anayocheza ni mchezaji ambaye hajakamilika pamoja na mabao mawili na improvement aliyoonyesha. Jamaa ni Giant ila Mara kadhaa alikuwa anaenda chini kilegevu sana,Kuna wakati watu hawatumii nguvu kabisa kumnyang'anya mipira anabaki anadondoka na kulala tunashambuliwa, anapoozesha mashambulizi na kasi ya timu yake hasa wanapokuwa wanavuka katikati. Nahisi anacheza sana na Kamera na mashabiki kuliko na wenzake uwanjani. Unakuta wenzake wametoka na mpira mbali ambako wameupata kwa jasho na damu wanampa yeye afanye engineering yeye anakaa nao anawasubiri waje wapinzani hata wawili watatu ili wapigane mavikumbo ndio atoe pasi(mpira Wa kizamani) hadi ananyang'anywa. Kwenye game ya Spurs alifanya hivyo wenzie walifanya kama kumsusia hivi wakamwacha apimane mibavu na maadaui aliowakaribisha mwisho akatoa tu mpira nje huku akionyesha hajaridhika. Anapewa Arm band hafu anacheza vile! Inabidi aache utoto muda si mrefu atakuwa kama Neymar manake vingi wanalingana.
 
Shaw karudi naona martial kidogo kipindi cha pili alibadilika aendelee kujiamini tu soon atakuwa poa
Martial ana kiwango ila shida ni confidence. Akirudisha confidence atakuwa powa kama mwanzoni
 
Ana show offs nyingi.. Same Mbape, Neymar bora hata hawa ni forwards. Hii inamfanya anapoteza mipira muhimu na timu kupwaya sometimes.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…