Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 aliteuliwa kuwa nahodha wa klabu kufuatia kuondoka kwa Wayne Rooney wakati wa majira ya joto, lakini ushinda dhidi ya Burton Albion kwenye kombe la EFL ndiyo mechi pekee ya kimashindano ambayo Carrick alivaa kitambaa cha ukapteni.
Carrick alifafanua Ijumaa iliyopita kuwa kutokuwepo kwake kutokana na matatizo ya moyo , lakini nyota huyo anaendelea vizuri na Mourinho amethibitisha kuwa kuna nafasi katika klabu kwa ajili yake hata baada ya kuachana na mpira.
"Michael kama mtu ni muhimu zaidi kuliko Michael kama mchezaji. Hivyo tutampa muda wa kupumzika, kupona na kutafakari. Kwa kufanya uamuzi kama anataka kuendelea kucheza, au anataka kuacha," aliwaambia waandishi wa habari.
"Anajua kwamba kwenye ofisi yangu kuna kiti kwa ajili yake ikiwa anataka, kama anataka. Kiti chake kipo pale ofisini .Nataka hivyo, bodi nayo inataka hivyo , wamiliki wanataka hivyo.
"Lakini anataka kuwa mchezaji hadi mwisho wa msimu na sasa anajisikia vizuri kurejea kwenye mazoezi. Chaguo moja zaidi kwetu.Tunahitaji wachezaji na ikiwa Michael atataka, nitafurahi na hilo."
Carrick alijiunga na United mwaka 2006 na amecheza michezo 460 katika klabu kwenye mashindano yote.