Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Me mpk sshv bado najiuliza imekuwaje ANDREAS PEREIRA akapelewa Valencia kwa mkopo na LINGARD yupo kwny Kikosi cha kwanza cha united..bado nawaza na sipati jibu


Ugiligili
Nijaribu kukujibu ingawa kuna mdau ameelezea vizuri kwenye post zilizopita kuhusu Pereira kwenda Valencia kwa Mkopo.

Sasa kwa nini Lingard amebaki kwenye squad ya Man United?linaweza kuwa swali zuri.

Kwanza tuelewe hawa ni wachezaji wawili wanaocheza nafasi tofauti uwanajani,Andres Pereira ni kiungo mkabaji (CM)ambapo kwa sasa kwenye timu kuna Nemanja Matic, Paul Pogba,Under Herera, Fellain na Mkongwe Carric,kwa kuangalia haraka haraka unaona kabisa Matic na Pogba wakianza kikosi cha kwanza huku Fellain akiwa plan B ya Mou as Regulator au Catalyst kwenye eneo la kati, kusaidia kushambulia na kusaidia kukaba kwa wakati mmoja na ikiwezekana kufunga huku Herera na Mkongwe Carric wakitokea Banch au wakianza kikosi cha kwanza kutokana na aina ya Match ila sioni hili likitokea kwenye EPL na UEFA mana ndiyo target yetu msimu huu kushinda yote au kushinda moja na moja kufanya vizuri.

Huku match chache zenye kuhitaji Viungo wakabaji watatu wakianza Pogba,Herera na Matic huku Caric akiwa Bench,sioni match hizi zikiwa nyingi msimu huu au sioni kama kutakuwa na haja ya kuwa na CM watatu kutokana na kikosi chetu so ni mara chache sana.

Kwa Mipango ya kocha naona tumkitumia sana Herera kwenye UEFA na makombe ya FA na Calling Cup kama ilivyoluwa kwa Ramos msimu uliopita,huku Caric akitumika sana kwenye match zenye kuhitaji wachezaji wazoefu na yeye akicheza sana kwenye FA.

Naona kikosi cha Kwanza kwenye EPL kikiendelea kuwa hichi hichi tulichoanza nacho mabadiliko machache yakiwa katika eneo la ushambuliaji.

Hivyo Mwalimu ameona kuna nafasi finyu ya kumtumia Pereira kwa sasa kwenye mipango yake na huku akitaka kumuona uwanjani akicheza na ndio mana amemtoa kwa Mkopo akiwa na matumaini ya kumrudisha Mwakani kama ataparform vizuri huko Valencia kumbuka kuwa kule kuna uwezekano akacheza kikosi cha kwanza ambacho ni kitu kizuri kwenye carrier yake, uzuri Adres Pereira ameshatuonesha kuwa ana uwezo na kumbuka uchezaji wa Pereira hauna tofauti kubwa na uchezaji wa Matic,kukaba,kushambulia na kupiga pasi za mwisho lakini anakosa uzoefu na match fitness kama Matic hivyo anahitaji kucheza match nyingi zaidi kitu ambacho asingeweza kukipata kwa sasa pale United.
Ni imani yangu kuwa Mou ana Malengo na Pereira msimu ujao mana hatutokuwa na Carric,huku Herera na Matic umri umeshaenda,tuondoe wasiwasi juu ya Pereira na tufatilie uwezo wake akiwa Valencia,nadhani sasa nitaanza kuingalia Valencia,Pereira alinionesha kitu kwenye match za maandalizi hivyo nalazimika kuendelea kumfatilia naona akija kuwa Matic mpya or Countihno kama atabadilishwa nafasi uwanjani.

Tuje kwa Jesse Lingard,kwa nafasi yake uwanjani Lingard ni kiungo mshambuliaji akitokea pembeni hasa Wing ya kushoto,kwa kuangalia kikosi chetu kwa sasa hatuna Mawinger,tunaye Ashley young na Antony Martial tu na Huyu Lingard kwa upande wa kushoto na hatuna Wing upande wa kulia lakini tukiwa na Viungo washambuliaji wengi na ndio mana unaona tukiwatumia left n right back wetu kama Mawinger wakati timu inashambulia,muangalie Valencia,°Darmian, Rojo,shaw au Blind na ndio mpira wa kisasa ambao unaachana na Mawinger wa asili wanaopiga cross na kutumia sana mabeki wa kushoto na kulia kama Mawinger huku ukijaza Viungo wengi wa ushambuliaji uwanajani hasa kuanzia namba 7,8,10 na 11.

Lingard anapata nafasi ya kubaki kwa nafasi yake kama nilivyoeleza hapo juu wapo wachache,lakini pia Lingard ana uwezo wa kukaba kiasili kama ilivyo kwa Young tofauti na Antony Martial katika nafasi wanayocheza na saa nyingine Mou akimtumia kama Mkata upepo katika eneo la Mbele kwa timu pinzani inayoshambulia kutokea pembeni na Mou ni muumini wa wachezaji wenye uwezo wa kukaba.

Na Lingard ni mchezaji wa wastani mwenye kipaji sio aina ya hawa watoto wanaotokea Ameriaka ya kusini au Africa,ni imani yangu Mou atamtumia sana kwenye mashindano ya F.A na Calling Cup kama Winger,sifa ya ziada Lingard kama ilivyo kwa Fellain ni wachezaji wenye kutekeleza kile kitu ambacho kocha huwaagiza uwanajani,hucheza kwa maelekezo ya kocha na kwa nidhamu ya Hali ya Juu.

Tuishie hapa kwa Leo ingawa naona kwenye maelezo yangu nimegusia kidogo uwepo wa viungo wengi wa ushambuliaji na wings wachache,nitakuja kuuelezea kwa nini hili afu Tuwe na mjadala wa kuwachambua makocha na vikosi vyao kwenye EPL.

Kwa uchache ndio aina ya soka lilopo kwa sasa duniani, na waasisi wa mtindo huu ni Barca ya Guadiola ambayo ilikop mtindo wa total football ya AFC Ajax ya uholanzi kwenye miaka ya 1980's na kuuongezea vionjo,Van Gaal akiwa mmoja wa waasisi wa mfumo huu pale barca ingawa hakupata nao mafanikio ila aliweka miundombinu mizuri kwenye La Masia, mtindo ambao ulikuja kusumbua sana dunia ya mpira ulipokubali na hata barca walisumbua sana kwenye Pick yao kumbuka Barc ile iliyotufunga mara 2 kwenye fainal na sisi tukiwa kwenye uwezo wa Hali ya juu na soka let u la Kiingereza,kumbuka Shughuli ya Iniesta na mwenzake ambao wao wawili tu walikuwa na uwezo wa kupiga pasi zaidi ya 600 kwa match moja,timu inakuwa haina kabisa wings na inakuwa na mshambuliaji mmoja tu.

Guys kwa Man United ya sasa baada ya Match 10,tutakuja kuongea mengine hapa Mou anakisuka kikosi hatari sana msimu huu,Chemistry ikikubali na viungo wetu wa ushambuliaji wakiwa wepesi naiona united ikija kuwa timu tishio pale Uingereza.

Shukrani.
Scofield.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Well said
 
Me mpk sshv bado najiuliza imekuwaje ANDREAS PEREIRA akapelewa Valencia kwa mkopo na LINGARD yupo kwny Kikosi cha kwanza cha united..bado nawaza na sipati jibu


Ugiligili

mkuu hata lingard katolewa sana kwa mkopo pia sio mchezaji mbovu yupo vizur hatupaswi kumdharau ana spid usisahau anatoka ktk academy lazima awepo kuwafanya madogo waliopo kwenye academy wafikirie kupata namba timu ya wakubwa kwa kuwaona wenzao wapo timu A namba anayocheza perreira ina watu wazito wakat lingard anaweza hata kucheza 7,10,11 andres perreira alimwambia mourinho anapenda zaidi no.10, 8 na 6 kocha anampenda sana perreira ila hiyo nafas ina watu wagumu sana hata Tomy Mctominay kapanda anacheza hizo namba nasikia ni kama matic au fellain alivyo mtata.

kwa hiyo ni bora alivyotolewa kwa mkopo kujiendeleza kuliko kumweka bench kizur zaid wamemuongeza na mkataba ulio na option ya kumuongeza mwaka mmoja.

unaona madogo kama wakina Solanke wa chelsea wanakimbia wenyewe wote makinda wanatolewa kwa mkopo halafu timu ina nunua wachezaji wapya sera za manchester united nzur sana mafanikio ya timu huchangiwa na academy kwa kiasi kikubwa hata migomo kwa wachezaji huwa hamna.
 
Rashford in England vs Slovakia 2-1 win yesterday:

- Involved in most of England's dangerous situations.
- 1 goal from outside the opponent's box
- 1 assist
- One of the most exciting players on the pitch.
- Still only 19
 
Dah we jamaa analysis zako nazielewaga sana yani unachambua mpaka naona nimekubali.

Xmass Boy.
 
BUFFON AMUWEKA WAZI ALIYEMVUTIA KUWA GOLKIPA.

Golkipa wa kimataifa wa Italia, na klabu ya Juventus Gianluigi Buffon ameweka wazi kwa mara ya kwanza, yeye ni shabiki mkubwa wa timu ya taifa ya Cameroon kutokana kuwa shabiki mkubwa wa Golkipa wa timu hiyo kuanzia miaka ya 1990, kipindi ambacho Kombe la Dunia lilifamyika kwenye ardhi ya nchi hiyo, akiwa na miaka 12 tu,

"Kipindi nina miaka 12, Nilimuona N'kono akicheza, nikavutiwa sana na yeye, na walipoifunga timu yetu ya taifa ya Italy wakati ule kwenye kombe la dunia, tokea siku hiyo nilikuwa shabiki mkubwa wa Cameroon, na nikafanya maamuzi ya kuwa golkipa kwenye maisha yangu ya soka" - Buffon alipoongea na jarida la michezo la Italia leo hii.

alikuwa tayari kavutiwa na Thomas N'Kono wa Cameroon na Walipofungwa na Cameroon kwenye mchezo wa kombe la dunia basi akaamua rasmi kuwa golkipa kwenye maisha yake ya soka.
 
Oooooh shit


king Ngwaba can you just tell me what Rodgers was trying to tell us here?



Slippy Gerald, you served football.

You wanna know? Simple! FSG doesn't care about any Trophy! Wanachoangalia ni Je Account imesoma Digits ngapi! Happy??
 
Dah we jamaa analysis zako nazielewaga sana yani unachambua mpaka naona nimekubali.

Xmass Boy.
Shukrani sana kaka,tuendelee kuwa pamoja tunapopata muda basi najaribu kushare hasa kile ninachokifahamu kuhusu mpira hasa Man United,kwangu ukiniuliza kitu ninachokijua vizuri basi ni Man United.

Najitahidi kufahamu falsafa yake,Malengo na umakini kama taasisi/kampuni mana jikoni wapo wengi kuifanya united kuwa hii tunayoiona.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenena mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Red colour will soon dominate the world of football

Zile presha za akina moyez na van gaal wake tumeanza kuzisahau sasa maana sio kwa depth ya kikosi chetu mwaka huu wetu kweli
Yeah sure pale EPL nawaona Liverpool tu ndio watakaoambulia angalau sare hii round ya kwanza.

Na totenham kidogo ndio watakaotusumbua angalau kuambulia sare na sio kuondoka na Point,ila hawa wengine sioni atakayetoka salama.

Na kadri muda unavyooenda Mou anakwambia ndio anavyozidi kuona makali ya wachezaji wake.

Now tunatafuta Match Fitness na Chemistry ya wachezaji wetu,baada ya Match kumi moto utakuwa sio wa kusogelewa.

Bado natamani kuona tukifungwa na kusawazisha na hatimaye kushinda,bado natamani kuuona ule ushindi wa dakika za mwisho kama enzi za Sir.

Mou amewaambia wachezaji wake hasa washambuliaji na viungo msimu hataki Pressure,ni kumaliza mchezo ndani ya dakika 30 za mchezo kipindi cha kwanza,ili kutoa nafasi kwa timu kurelax na sisi mashabiki kuendelea kuagiza vinywaji bardi kwa raha na wengine kuendelea kununua Popcorn au kusoma Mwanasport.

Mabeki wameambiwa wahakikishe De Gea anakuwa likizo ndani ya mchezo,amefanya kazi kubwa sana misimu mitatu iliyopita now anatakiwa kupumzika akiwa uwanjani ikiwezekana awe ananingia na simu au magazeti aendelee kuperuzi kuhusu yanayoendelea duniani hasa ya kuapishwa kwa wabunge wa CUF,watengeneze ukuta kuuzidi ule wa Rio na Nemanja.

Pale kati,Matic ameomba pale aachiwe yeye,Pogba ametuhakikishia furaha na nadhani tumeanza muona Pogba wa Juve (New Scolse),yale magoli ya Nje ya 18 yalikuwa adimu tangu aondoke CR7 now sasa tutaanza kuyaona.

Yale magoli ya ajabu ajabu ya Dimitri berbetov soon Ibra ataendelea kutukumbusha.

Rashford sitaki hata kumuongelewa alichowafanya jana Slovakia sio mchezo naona Mou ataanza kufikiria kumpanga kati kama namba 10 na Mikh kurudi namba 7 tuone pasi za mwisho za kideo,mana sio attack zake.

Bado Form kwa Mikh na Matta hawa wakiwa on fire basi hamna haja ya kumuangalia Isco na Assecio mana ni wachanga kwa hawa mafundi,Mkubwa Fella Leo simzungumzii kabisa namuacha apumzike mana hata sijui ile namba anayocheza pale ni ngapi lakini ndio hivyo ibaki kuwa kiungo Holding Midfield wa juu.

Banch sitaki kuligusa mana Match ijayo tutaanza muona Ibra akiwa Banch.

Mou anatamani match zingekuwa zikichezwa kila baada ya siku mbili.

Mou anasema "We're on Fire).

[HASHTAG]#This[/HASHTAG] is our season.
##GGMOU.

Scofield.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesomekaa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MAN UTD: DE GEA AMEWEKA WAZI KUWA, KUWA MAN UTD NI KAMA NDOTO KWAKE.

Golikipa namba moja wa Man Utd, David De Gea alipohojiwa na televisheni ya klabu hiyo amesema kuwa

"Unapozidi kukua, unaanza kuwa na ndoto ya kuwa hapa, kuwa kwenye klabu kubwa na ya juu, kwahiyo ni ndoto kuwa kwenye klabu kama Ma utd" - De Gea aliiambia MUTV.

Hii vita Van gal alipambana vizur sana angekuwa bwege angampoteza kirahisi sana pia shukrani zake kwa kumpandisha rashford kamleta martial Mourinho kaja kumsahaulisha kabisa de gea kurud spain vigezo vyake kama madrid wangemtaka de gea basi tony kroos,bale au varane na hela mmoja lazima aende united au wakikataa watoe hela kuanzia £ 66 baadae kabadilika £100 madrid wakatulia
 
Najaribu kuwaza tuu Kwa saut ivi mou hawez kuja kutuacha kama alivyozoea akibeba vikombe anasepa? Anaweza kuwa Wa kudumu kama farg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…