Nimeandika sana huko nyuma juu ya huu usajili,ilikuwa ni lazima kwa Mou na Man U kumsajili Matic,ni jambo lililokuwa linasubiri muda tu kutimia na hatimaye limekuwa kweli leo.
Matic is Red am happy.
A realy and best defensive midfielder is in Carrington now.
Niandike kidogo,kuhusu Matic.
Kwa misimu takribani minne hadi sita iliyopita Man United tulikuwa na tatizo la mchezaji kiungo namba sita(holding midfilder),ilifika kipindi tulilazimika kumtumia Scholes kama namba sita wetu.
Na hata tulipomsajili Carric bado tatizo hili lilikuwa linatusumbua na Sir Fergie aliondoka bila kututatulia hili tatizo.
Tume jaribu kwa Herera,Blind kidogo na Pogba last season angalau kidogo lakini ilitulazimu kutumia Viungo wengi hivyo kuleta shida kwenye upangaji wa timu.
Kiuchezaji Matic namfananisha na Ton Krose wa Real Madrid au Khedira.
Kumbuka kuna kipindi Man United ilitaka kumsajili Ton Krose tukamkosa.
Matic ni world clasic player kwa sasa na moja ya wachezaji Wenye shughuli nzito uwanjani lakini wasionekana kutoka na majukumu waliyonayo.
Ukitaka kuiona shughuli yake mwisho wa mchezo angalia mchezaji aliyetembea km nyingi.
Ukitaka kuiona shughuli ya Matic iangalie Chelsea ya misimu miwili iliyopita,pale kati walikuwa salama kweli kweli na kuwafanya akina Hazard kuwa wamoto Zaidi.
Huyu ni mwanaume na mpiganaji aliyekamilika katika nafasi ya kiungo wa ukabaji anayeyajua vema majukumu yake,ana uwezo wa kuzuia na kupandisha mashambulizi.
Wachezaji wa namna hii wapo wachache kwa sasa Duniani, na timu nyingi zinasumbuliwa na aina hii ya wachezaji,Madrid wanajivunia kuwa na Ton,Barca pia.
Uzuri Zaidi anafiti katika mifumo ya Mou na Mou anajuwa shughuli ya Matic awapo uwanjani.
Matic ana mapafu na aina ya upiganaji wa Paul Ince,asiyechoka na ni mpiganaji haswaa.
Sasa Viungo wetu wa Ushambuliaji na washambuliaji watakuwa huru Zaidi.
Niliwahi kusema ili tuone uwezo wa Pogba lazima asajiliwe Matic ili Pogba apunguziwe majukumu na kuwa free,sasa tunaenda kuona shughuli ya Pogba,Rashford na Lukaku.
Nitafurahi Zaidi kama Mikh akiwa vizuri katika kiwango chake,ili pale mbele panoge Zaidi.
Timu kama Barcelona tumeshapata dawa yao,.
Naisubiri Supercup kwa hamu Zaidi, ila ubaya wake hatakuwepo Baily.
Madrid wajipange Zaidi Man United inapata muonekano mpya zaidi na kuzidi kuimarika.
Hofu yangu ni kwa Man City naiona ikisukwa kiufundi zaidi.
Welcome Fundi na King katika dimba la chini Matic.
Inshallah Mungu atupe uzima,msimu ujao sio wa kumiss match hata moja kwa Man U.
[HASHTAG]#GGMU[/HASHTAG].
Sent using
Jamii Forums mobile app