Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kwanini usijibu maswali unayoulizwa badala ya kutoa maelezo huku maswali ukiyatulilia mbali?

Maana wewe huyo huyo unadai kua mid za Utd zimefanya vzr na kujitahidi sn.... Na Mimi nakuuliza hapo hapo ni wachezaji gani ktk hizo mid wana viwango vya hao wachezaji niliokutajia?

Jibu maswali bhana ili kufanya mjadala wenye afya.

Matatizo ya Mou akiwa Chelsea ni mengi mno Na nimeshaeleza sn na kuna mdau mmoja kasema wazi kua Mou ana kitu ambacho watu Wa EPL hawataki akipate


Jibu maswali bhana
 


Wanataka nikose haki yangu........


Yani Mourinho ni baba yangu kweli angalia avatar yangu hapo juu inaongea....
aiseee !!!! Kweli una mapenzi ya dhati nilifikiri alivyotoka kwenu ungekacha kumbe ndo umezidisha ongea na best Mou wa Juve akuachie Hili jina....... ila mbona Mimi hunipendi hivyooo
 

Mkuu, naona umeongea mengi yenye tija, tukubali au tukatae lawama nyingi ni za kocha.....timu aliyoiacha mou pale Chelsea na hii ya Conte ina tofauti gani. Tatizo la Mou na LVG wote ni wabishi " it's his way or no way attitude" timu kama Man Utd sio ya kukaa kumpa muda kocha huwezi pisha mbona Conte alionekana wild card na ana perform vizuri wapo makocha wengi tu wanataka kufundisha Man Utd.
Mou ana muda wa kubadilika na kupata matokeo ila inabidi akubali kuwapa game wachezaji kutokana na michuano na opponents kama alivyokuwa anafanya SAF au makocha wengi, kila siku watu tunasema Fellain sio mchezaji wa kucheza Man utd ila tunazidi kuona. Wacha watu wacheze position zao then hawaperform piga benchi.
Kisingizio cha muda kimepitwa na wakati......Kocha ana omba muda kufundisha Sunderland and Co ila Man Utd tuna resources za kutosha .
 
Maswali yako majibu unayajua
Yaani wewe unauliza Scholes, kulikuwa na Scholes mmoja tuu.

Nakujibu ila hufuatiliii majibu yangi, nakwambia ubovu tulionao kwenye midefield
Kwanza siyo tatizo linalo isumbua man u
Pili, siyo sababu ya kutufanya tushindanie u 6 na west brom. Hata kama tuko wabovu kiaje.

Sasa ukiongelea vitu nje ya footbal mi nazichukulia kama fununu tuu. Ila nnacho jua alifeli ku organize timu yake, kama anavo feli now.
 
Chelsea wana ukuta Wa uwezo Wa Schols.

Kante Na Matic wamethibitisha hilo ndio maana Chelsea imecheza games 8 Na kufunga goli 22 Na kufungwa goli 2 tu. Na Sasa kipa wetu kazi Yake ni kulala tu.....
 

kwenye RED hapo Povu lazima mtoe hehehehehe

hamna namna....!!!! kipindi hiki mmekuwa wadogoooo
 
Najua unaipenda Arsenal, kule hakuna hofu
na Mungu fundi kweli
 

wape moyo sio vibaya kuwafariji kipindi hiki kigumu

akufaaye kwenye DHIKI..............!!!!
 
Ubishi hauji kwa tu bure bure lazima uwe Na sbbu za msingi.

Conte pia japokua ameshinda michezo kadhaa lkn timu Yake haiko imara vzr kuna makosaengi pia kwa Conte Na Chelsea. Unaweza kurejea game ya Chelsea na Spurs pale darajani spurs walikua bora kuliko sisi Ni uzembe wao tu vinginevyo walipaswa kukill game first half tu. Unaweza kusema ni uwezo binafsi au bahati tu tukawafunga lkn spurs they were better than us.

Tukija kwa city hapo Etihad ndio usiseme. Kuna mengi tunapaswa kuyafanyia kz Na kuinprove kila baada ya game. Hasa hizi big game maana huwezi kua bingwa bila kuwapiga washindani wako hawa top four.
 
Chelsea wana ukuta Wa uwezo Wa Schols.

Kante Na Matic wamethibitisha hilo ndio maana Chelsea imecheza games 8 Na kufunga goli 22 Na kufungwa goli 2 tu. Na Sasa kipa wetu kazi Yake ni kulala tu.....

Kipa wenu anafanya kazi sana, uzuri ni kuwa mechi zenu huwa sikosi ili usinidanganye, huyo Matic hamfikii Scholes kwa lolote, timu yenu kocha ana teknik, halafu wachezaj wana morali. Ndio mna kiungo bora kuliko man utd.

Ila man utd haina kiungo kobovu kias kwamba tufeli hivi
 


Best yangu Mourinho nilimuahidi nimpe shamba LA minazi kule vikindu aniachie hilo jina kakataa.


Wewe nakupenda chana km kuliko Mourinho
 
Tehe tehe

Hutoi majibu

Matatizo ya Utd ni viungo
 
Kuendelea kujadili kile kinachoendelea ndani ya club ya Manchester United ni sawa na kujaribu kuupanda mlima kilimanjaro kwa kutumia mikono. Pale timu ilipofikia ndio uwezo wa JOSE MOURINHO ulipoishia. Hii sio MAN U ya misimu mitatu ama minne iliopita. Kuingiza mchezaji kwenda kulinda goli moja ni dalili za kuishiwa na ukikomo wa kile ukifanyacho. Msimu huu msitarajie Miujiza yoyote ile.
 

hapo kwenye RED ni uongo

same group of players waliopo sasa ukimrejesha SAF anatoboa

SAF alikuwa na uwezo mkubwa wa kutengeneza timu za ushindi hata wachezaji wa viwango vya KAWAIDA

tunaofutailia mpira tuna recognize uwezo wa SAF

waweza argue kuwa 2008 na 2009 ndo Manure kwa miaka ya karibuni walikuwa na full of superstars na powerhouse

ila 2010-2013 vikosi vya SAF vilikuwa vya kuunga unga ila anapata matokeo

SIAMINI kabisa matatizo ya manure ni WACHEZAJI maana hawa hawa ni wachezaji wazuri tu kuna kitu lazima kitoke kwa MWALIMU na HAKIPO
 
Matic Na Kante ni viungo wenye uwezo mkubwa km kina Claudio makelele Na Scholes. Km hukubari huo ni mtazamo wako.

Ndio wachezaji wanajituma lkn sio kwamba eti kocha ana mbinu nyingi hapana. Game yetu Na Spurs Conte Na timu yetu tuliwekwa mfukoni though tulishinda etihad ndio usiseme.

Sema ni kwamba morari ya wachezaji imeongezeka Na kitu kinachoibeba Chelsea sn msimu huu wana nafasi ya kujiandaa ya kutosha kukabiliana Na timu yoyote maana hawako ktk UEFA Na kombe moja wameahatolewa. Sasa wanapata muda mzuri sn tofauti Na City au Spurs. City kwa Mara ya kwanza walikua Na muda Wa wiki nzima kujiandaa Na mchezo ktk hii last week kabla ya kuwavaa Chelsea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…