Manchester United (Red Devils) | Special Thread

 
Haiingii akilini Man U kununua mechi ya Wolves badala ya kununua ya Arsenal au Chelsea. Utasema hao nao wanataka ubingwa, basi angenunua ya Aston Villa ambaye ubingwa hawezi ila anatafuta nafasi nzuri tuu za juu. Wolves wasingeuza mechi kwa sababu hawatapenda kushuka daraja baada ya msimu mmoja. Kwa hiyo propaganda za Wenger hazitamfikisha mbali bora acheze mpira tuu.
 
Dakika ngapi watazidishiwa leo na refer mpaka warejeshe......?
 
Damien Duff anaongeza la 3,Dk ya 77 Fulham 3 Man Utd 0..Mnalo leo
 
hata 5 wanaweza kutufunga, nadhani hili ni fundisho kwa SAF na ni bahati mbaya kwamba wachezaji wengi i majeruhi.
 
hata 5 wanaweza kutufunga, nadhani hili ni fundisho kwa SAF na ni bahati mbaya kwamba wachezaji wengi i majeruhi.

Usikate tamaa mda bado sana na zile za kwenu si mtazitumia.
 
duuh poleni wakuu humu ligi ngumu mwaka huu kelele za 2 horse race haziwafikishi popote hizo bado mapema sana kuanza kuaongea uchafu.
 
SAF kachemsha ... beki yake haikuwa makini, anaweza kuwa na excuse ya majeruhi. Maana hata kwenye orodha ya wachezaji wa akiba beki alikuwa mmoja tu (Fabio).

Pia kiungo kilipwaya sana, kiasi kwamba hakukuwa na coordination kati ya safu ya ulinzi na safu ya mashambulizi. Sijui Anderson alikuwa ni kiungo ama beki, Scholes ambaye alisababisha goli la kwanza alipwaya sana.

De Laet alizidiwa sana na hakuwa na ujanja, angalau Fabio Da Silva alipoingia kukawa na nafuu.

Pole Man U kwa kuwa jamaa walio juu ya meza kesho wanaweza kuzidi kutanua pengo la point. Majeruhi wenu wapone haraka ili mambo yawe mswano.

Kama hali ya majeruhi itaendelea kuwa kama ilivyo sasa, kuna haja ya kumshauri SAF atumie window ya January kupata beki mmoja ama wawili, vinginevyo hali inaweza kuwa mbaya sana.

Kwa mwendo huu na timu kama hiyo mwezi February ukifika, AC Milan wanaweza kuchekelea ushindi/kusonga mbele hata kabla ya kuingia uwanjani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…