Mkuu huo ni ushamba. Nimewasikia mashabiki wengi wa Man United, Arsenal na Liverpool wakiwabeza mashabiki wa Man City kwa kejeli nyiiingi kama vile eti mashabiki uchwara, mashabiki wa jana, sijui mara wamefuata mafanikio tu, mara ooh kabla mlikuwa timu gani.....maneno mengi mbofu mbofu. Kwani wewe kama ni mshabiki wa Man United au Arsenal toka mwanzo wa dunia ina kuuma nini mtu akijitambulishakuwa mshabiki wa Man City? Kwa taarifa yako hata wewe kuna siku ambayo ulianzia kuipenda hiyo timu unayoishabikia leo. Kila kitu kina mwanzo mkuu.....stop being a hater. Kwenye michezo, timu yoyote inayofanya vizuri ni wazi itaanza kujenga fan base... Ina maana niogope kujitambulisha kuwa mimi ni mshabiki wa Mbeya City au Azam? Kisa utakuja kunikebehi eti mimi ni mshabiki uchwara? Mpira nimeujua jana? Waachane jamani mashabiki wa Man City waendelee kufurahia kiwango bora cha timu yao kwa sasa huku wakiendelea kutoa dozi nene kwa wapinzani wao kila kukicha. Hongereni Man City kwa kucheza soka zuri na la kuvutia....Ndo maana katika mitaa ya hapa Dar jezi za Man City zimeanza kuwa nyingi kuliko za Liverpool hahahahah!