manara aongezewa mashtaka 11 na kuwa 17


P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
39,863
Likes
8,686
Points
280
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
39,863 8,686 280
KADA wa CCM, Haji Manara jana alipandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka mengine 11 ambayo yanafanya jumla ya mashtaka yanayomkabili kufikia 17.


Katika mashitaka hayo hayo mapya, Manara anatuhumiwa kwa wizi wa kuaminika kwa kujipatia fedha kwa njia ya kuweka rehani mali ambazo si zake.


Mwendesha mashtaka, Inspekta Batseba Kasanga alidai mbele ya hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Benedictor Beda kuwa mtuhumiwa alitenda makosa hayo yote eneo la Magomeni.


Kasanga alisema kati ya Desemba 22 mwaka jana mtuhumiwa alijipatia Sh1 milioni kutoka kwa Mohamed Nassoro na kuweka rehani gari aina ya Toyota Pajero T731 AVM ambayo si mali yake.


Alidai kuwa tarehe 23 ya mwezi huo alijipatia Sh2.5 milioni kutoka kwa Shehe Ally na kuweka rehani gari aina ya Toyota Carina T346 BSW na kwamba Desemba 31 Manara pia alijipatia jumla ya Sh 3 milioni toka kwa Eustace Bajwala na kuweka rehani gari aina ya Toyota Camri T188 BAS.


Katika makosa mengine 18 Januari mwaka huu mtuhumiwa alijiptatia Sh6 milioni kutoka kwa Mohamed Abdallah na kuweka rehani gari aina ya Toyota Corolla T 881 BDT na 14 Januari mtuhumiwa alijipatia kiasi cha Sh3.5milioni kutoka kwa Abeid Abubakari na kuweka rehani gari aina ya Rav 4 T160 ASF.


Mwendesha mashtaka huyo pia aliendelea kueleza Mahakamani hapo kuwa Januari 5 mwaka huu Manara alijipatia 3milioni kutoka kwa Baruan Issa na kuweka rehani gari aina ya Toyota Rav 4 T156 ASF na kufanya kosa kama hilo tarehe 9 ya mwezi huo huo kwa kujijipatia Sh3.7 milioni kutoka kwa Hamad Rashid na kuweka rehani gari aina ya Toyota Rav 4 T 759 AES.


Aliendelea kuyataja makosa mengine ambapo mwezi 16 Novemba mwaka jana mtuhumiwa alijipatia Sh3.2 milioni kutoka kwa Dotto Lugwisha na kuweka rehani gari aina ya Toyota Rav 4 T 998 AES na 18 Januari mwaka huu mtuhumiwa alijipatia Sh2.7 milioni kutoka kwa Selemani Mange na kuweka rehani gari aina ya Toyota Corona T 895 AXA.


Mtuhumiwa huyo huyo alijipatia 3.5milioni kutoka kwa Haji Abdallah na aliweka rehani gari aina ya Toyota Rav 4 T 269 ARY na Januari 14 Manara alijipatia Sh2,080,000 kutoka kwa Flaviani Magori na kuweka rehani gari aina ya Nisan Station Wagon T621 ATU.


Kasanga alieleza Mahakamani hapo kuwa magari yote ambayo mtuhumiwa alikuwa akiyaweka rehani hayakuwa ya kwake hali iliyofanya wamiliki halali wa magari hayo kuwakamata walalamikaji katika shauri hilo.


Manara alikana makosa hayo yote na upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana hadi kesi hiyo itakapotajwa tena mwezi 5 Aprili.
 

Forum statistics

Threads 1,236,240
Members 475,029
Posts 29,251,215