Mkurugenzi Mtendaji wa Manara Tv na Mgombea Udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kariakoo Ndugu Haji Manara
ameondoa taharuki kufuatia taarifa zilizosambaa kuhusu hali yake ya kiafya, akihakikisha kuwa yupo vizuri na wala haumwi.
Akizungumza hii leo Oktoba Mosi, 2025 Ndugu Manara amesema, "Ndugu zangu na mashabiki zangu wamepata taharuki kwa kile alichokiandika huyu dada (Maimartha) ,Sijui nimemkosea jambo gani? Kaandika mimi nimekuwa chizi, nimekuwa mwendawazimu, nimefungwa kamba za miguu na mikono" Alisema Manara na kuonyesha kusikitishwa na kitendo hicho huku akikiri kukosewa na dada huyo.
"Amenikosea mimi, amewaletea taharuki familia yangu bila sababu, wamelia sana. Maimartha kama unaona kuna jambo nimekukosea kwa dhati nimekukosea, Naomba radhi" Alisema Manara.
Ndugu Manara amesema kutoonekana kwake kwa siku mbili ni kutokana na kujikita kusoma vitabu mbalimbali, "Niko nyumbani kwangu Masaki nasoma vitabu tu, nimejipa siku mbili tatu za kusoma vitabu tu. Kutoonekana kwangu leo hakumaanishi nimepata wazimu au nimeumwa Malaria, Hapana." Alisema Manara.
Ndugu Manara kupitia video hii ameonekana mwenye afya njema huku akionekana akisoma vitabu mbalimbali vya historia kikiwepo kitabu cha Mama SHUJAA WA MFANO, "Sengimba wa Wahehe, Samia na Watanzania kilichoandikwa na Mwandishi Dkt. Mkumbo G. Mitulaya.
Lakini pia amekuwa akipitia vitabu vya Historia ya Jiji la Dar es Salaam hususan Kariakoo ikiwemo Shajara maarufu ya Mwana Mzizima, kitabu kilichoandikwa na Mtunzi Mashuhuri wa Historia Alhaj Abdallah Mohammed Tambaza yenye historia ya kina ya mji huo, kwani kama kiongozi hawezi kuongoza bila kujua historia ya eneo lake.
Aidha, Manara amefunguka kumsamehe mwandishi wa habari, Maimartha, kwa kile alichodai kuwa kueneza taarifa za uongo mtandaoni kuhusu afya yake, na kwa heshima amemuomba Mungu amsamehe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Manara Tv na Mgombea Udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kariakoo Ndugu Haji Manara
ameondoa taharuki kufuatia taarifa zilizosambaa kuhusu hali yake ya kiafya, akihakikisha kuwa yupo vizuri na wala haumwi.
Akizungumza hii leo Oktoba Mosi, 2025 Ndugu Manara amesema, "Ndugu zangu na mashabiki zangu wamepata taharuki kwa kile alichokiandika huyu dada (Maimartha) ,Sijui nimemkosea jambo gani? Kaandika mimi nimekuwa chizi, nimekuwa mwendawazimu, nimefungwa kamba za miguu na mikono" Alisema Manara na kuonyesha kusikitishwa na kitendo hicho huku akikiri kukosewa na dada huyo.
"Amenikosea mimi, amewaletea taharuki familia yangu bila sababu, wamelia sana. Maimartha kama unaona kuna jambo nimekukosea kwa dhati nimekukosea, Naomba radhi" Alisema Manara.
Ndugu Manara amesema kutoonekana kwake kwa siku mbili ni kutokana na kujikita kusoma vitabu mbalimbali, "Niko nyumbani kwangu Masaki nasoma vitabu tu, nimejipa siku mbili tatu za kusoma vitabu tu. Kutoonekana kwangu leo hakumaanishi nimepata wazimu au nimeumwa Malaria, Hapana." Alisema Manara.
Ndugu Manara kupitia video hii ameonekana mwenye afya njema huku akionekana akisoma vitabu mbalimbali vya historia kikiwepo kitabu cha Mama SHUJAA WA MFANO, "Sengimba wa Wahehe, Samia na Watanzania kilichoandikwa na Mwandishi Dkt. Mkumbo G. Mitulaya.
Lakini pia amekuwa akipitia vitabu vya Historia ya Jiji la Dar es Salaam hususan Kariakoo ikiwemo Shajara maarufu ya Mwana Mzizima, kitabu kilichoandikwa na Mtunzi Mashuhuri wa Historia Alhaj Abdallah Mohammed Tambaza yenye historia ya kina ya mji huo, kwani kama kiongozi hawezi kuongoza bila kujua historia ya eneo lake.
Aidha, Manara amefunguka kumsamehe mwandishi wa habari, Maimartha, kwa kile alichodai kuwa kueneza taarifa za uongo mtandaoni kuhusu afya yake, na kwa heshima amemuomba Mungu amsamehe. View attachment 3482025