vCTRMA
JF-Expert Member
- Jan 12, 2016
- 306
- 102
Nisahihi mawazo mazuri,......ila kuingia katika utakatifu unasema uende ktk njia ya msalaba,...YESU alikufa msalabani ili kutukomboa,.ukisema kuwa kukombolewa dhambi kwanjia ya msalaba ni kwamba YESU hakufanya/hakutukomboa msalabani,.....sio sahihi YESU alishakufa msalabani kwa ajili ya dhambi zet,...unavyosema hivyo nisawa nakwamba kuvaa msalaba kuamini kuwa Yesu yupo msalabani na unavyouomba huo msalaba ambao umechongwa na watu ni sawa na ibada ya sanamu,......kusoma biblia ni sahihi lazima uwe na mafunuo ili uweze kuielewa,Ndugu, na kuelewa vyema sana, tena sana Ndugu yangu.
Kuingia kwenye njia Takatifu ya Msalaba kuna hatua zake ( madaraja). I mean, the more unavyokua mtiifu na humble mbele za Mungu kupitia Yesu ndipo unapanda daraja la uelewa.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuokoka ( wokovu ) na kukombolewa. Pia kati ya kuokoka na kuchaguliwa. Haya ni madaraja ambayo yanakuwa na hatua zake za Uelewa katika Ufalme wa Mungu.
Ni vyema ukatambua kwamba, Mungu/ Yesu ; yupo interested sana kwenye Mioyo yetu. Kama tukipewa Uelewa kidogo, ni lazima tuutumie kuuliza maswali ili tupate nguvu za kuendelea kuutafuta uso wake mpaka hatua ya mwisho ya kufunguliwa mlango wa mbinguni.
Hapa utaona Uelewa ni muhimu sana katika hatua zote.
Nataka kusema kwamba , daraja la kuokoka ( salvation) ( ambalo ni la pili, si la kwanza kama watu wanavyofikiri - katika ufalme wa Mungu) linaweza kumfanya MTU kuchaguliwa kama itampendeza Mungu ( kupitia Yesu)
Kuna watu wengi sana huwa wanaifikia hatua hii, lakini huwa hawawezi kuchaguliwa kutokana na Tamaa za miili yao pamoja na nguvu zilizopo kwenye Mazingira yao.
Hii ni sehemu ambayo huwaandaa watu kwenda kuvuna walichopanda. Na wengi huishia kula au kuvuna matunda ya miti ya Hisia ( sio ile waliyoipanda). I mean, wanaikana miti yao na kutamani kwenda kuvuna miti ya Ulimwengu huu.
Ushauri; Jichunguze njia zako; Tubu , rudi msalabani. Kumbuka , asiye elewa maana hana maana. Namaanisha, unaweza kuisoma Biblia nzima na kuikariri, lakini usielewe kilichoandikwa. Hili ni tatizo linalikusumbua kwasasa...,
Tafuta mzuri na Mungu/ Yesu ..... Mazingira unayoyatumia kusoma maandiko ya Mungu ndio yanakufanya usilielewe vyema neno lake. Hii itakufanya kuwa mjuaji tu lakini sio Muelewa.
Mungu akubariki sana. Damu ya Yesu ukutakase!
kusoma biblia ili mtu ajionyeshe ni sawa na bure
kusoma bible ili kupinga watu ni sawa na bure,.mtu hawez kuelewa iko hivyo
kusoma biblia kama stori=nothing
tukumbuke ya kwamba biblia tunasoma as a guidance,.tu7nasoma tuenende katika njia MUNGU anazozitaka,tujue ya kuishi ktika njia za MUNGU kwa kupitia mafunuo ambayo MUNGU atatupa
kusoma biblia kinyume na matakwa ya MUNGU=Nothing
ila biblia lazima isomwe na wateule na ijae ktk nafsi,mwili na roho ili iwe ni nguzo ya maisha yao kwa kila jambo,.
kwenye red hapo,...mazingira gani hayo labda?
kama biblia MUNGU ananifunulia mwanadamu ni nani hata apinge?