Manabii wa Uongo: Kwa Matendo Yao Mtawatambua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manabii wa Uongo: Kwa Matendo Yao Mtawatambua

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiranja Mkuu, Mar 18, 2010.

 1. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mimi naabudu kwenye lile kanisa.
  Pale panapofanyika miujiza ishara na maajabu ya kila namna.
  Mwingine nae anaabudu pale pengine, tunapoambiwa wanaabudu miungu mingine.
  Je kweli sisi tunaabudu kwa namna ambavyo mungu wetu anataka tumuabudu?
  Mchungaji wengu ni mbaguzi, anawaweka mbele ya madhabahu walio matajiri na sisi massikini tunaambulia siti za nyuma na wakati mwingine kusimama.
  Haturuhusiwi kuvigusa wala kuvikaribia viti vya mbele vinavyokaliwa na wenye nazo.
  Mchungaji mwingine ni mbishi, hatii mamlaka iliyopo madarakani, anashupalia miundo mbinu isipite jirani na kanisa lake.
  Anawatesa watu kwa kuwafanya wakeshe usiku na mchana kwa miezi miwili mfululizo huku wakipigwa na mvua, jua, upepo, vumbi , mioshi ya magari na dhoruba zote.
  Mchungaji mwingine kazui yake ni kuponda tu huduma za watu wengine na kusema kwamba ishara na miujiza ya kwake peke yake ndio iliyotoka mbinguni.
  Mwingine ana skendo ya kuua mtu arusha na sasa amehamia dar es salaam baada ya soko kumuendea kombo.
  jamani hivi hawa sio manabii wa uongo?
  mbona matendo yao yanatutia mashaka?
  ona walivyo matajiri , wamejilimbikizia mali, hawana upendo hata kidogo kwa waumini wao.
  wanawanyonya wenzao.
  siku za mwisho watu watakuwa ni wenye kupenda mali na upendo wa kweli utapoa.
  naomba tuendelee kuyachunguza matendo ya waheshimiwa wetu huku tukiyalinganisha na maagizo aliyotuachia bwana wetu yesu kristo.
  inatubidi tubadilishe namna za ibada zetu na tuanze kumuabudu mungu katika roho nakweli, badala ya kuwa tunasema kuwa naabudu kanisa lile.
  mungu anawataka wamuuabudio halisi.
  wale wanaomuabudu katika roho na kweli.
   
 2. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  wewe ndiyo nabii wa uongo, nakushauri kitu kimoja, issue kamahizi ambazo hauna uhakika na unachokiongea, usiweke public, sijui umri wako. ni kwanini nasema hivi, huwezi jua, pengine hao watu ni watu wa Mungu kweli, na wewe ukapanda mbegu chafu kwa mamilioni ya wana jf hapa, wakamtukana Mungu, au wakamuacha Mungu au ukawa umezuia kazi ya Mungu kwa upande fulani, hauna uhakika, MZIGO WOTE HUO UTAUBEBA WEWE ULIYELETA HII MADA MBELE ZA MUNGU. kama Mungu atatukanwa, you will be accountable, kama watu hawataokoka kwasababu wewe umesema, you will be accoutable, kama watu watatukana wokovu wa Yesu, you will be accountable. na utavuna unachopanda. kumbuka, washindanao na Bwana watapondwa kabisa, Mungu anao uwezo wa kumponda kabisa mtu anayezuia kazi yake, sasa hii post yako angalia isijekuwa inapingana na mapenzi ya Mungu, kwasababu nakuhakikishia utapondwa kabisa. pia, hovyo, kaa tayari, lolote laweza kutokea kwako kuanzia sasahivi, pengine kwa kuleta hii mada hapa, utasababisha madhara mengi kwenye kazi ya Mungu. huwezi jua ndugu. ndio maana ni bora kuwa na busara na hekima.
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Mkuu mwana wa Mungu, mimi namuunga mkono mtoa hoja kuwa Mungu ametupa akili ya utambuzi na vile vile ameshatutahadharisha kabisa kuwa siku za mwisho wataibuka manabii wa uongo, sasa kwa nini tusihoji pale watumishi wanapotupa mashaka kwa matendo yao? Huoni kuwa Mwenyenzi Mungu atakuja kutuhoji jinsi tulivyoishi maisha yetu pamoja na akili alizotupa? Hakuna Mchungaji/shehe/padre/nabii yeyote atakaye simama kujibu maswali yako bali wewe mwenyewe na nafsi yako, kila mmoja ataubeba mzigo wake mwenyewe.. Isitoshe, siyo watumishi wote wa mungu ambao watu wanajihoji kuhusu matendo yao, hujiulizi kwanini?
  Eti Mtapondwa pondwa!!! acha vitisho vya kishabiki bana!
   
 4. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kwani vigezo gani ni vya kusema mtu ni nabii wa uongo au siyo , kwa uelewa wako? mimi hapa nilikuwa natoa ushauri, wala sitishi mtu, kwasababu sina impact yoyote kwako wewe pia. niliposema mtu atapondwa kabisa, nimekoti kwenye bible, kuna mistari inayosema hivyo. pia, usifikiri kuwa watumishi wa Mungu ni malaika, hata wakiteleza kidogo Mungu anawasamehe na wanaendelea kuwa watumishi wa Mungu, tatizo la watu wakiona kosa moja tu wanafikir basi Mungu ameshamtupa, si mtumishi wa Mungu tena, si hivyo, hao wote anaowataja hapo, ni watumishi wa Mungu, niemhakikisha, kuna maelfu ya watu wamemwona Mungu kwa maombi yao, nawashauri muwe makini na mada hii.
   
 5. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2010
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,695
  Likes Received: 752
  Trophy Points: 280
  KILANJA MKUU kaka umenena ya ukweli kabisa tena pasipo kukosea, huyo mwana wa Mungu ndio wale wamelishwa sumu na wachungaji wao kuwa ukimsema mtumishi wa Mungu hasa kwa kukosoa utendaji wake basi wewe ni muasi na kamwe hutaona ufalme wa Mungu. lkn biblia inasema wapimeni kama kweli ni manabii wa ukweli au wa uongo kwa matendo yao ndio tuwapime na tusipowajadili unafikili tutawajuaje. nasikitika kwamba waumini wengi wamelishwa sana sumu kiasi cha kuwa wanaitikia ndio bwana mkubwa kwa wachungaji wao, wengine ni watu wa heshima kabisa lakini ukimwambia mbona mchungaji wako au mbona nabii na mtume hapa anaonekana kwenda kinyume na biblia, heeee utasemwa wewe ni muasi, poleni wapwendwa kwa kukaliwa kichwani mi naita ukolono makanisani twende kilanja mkuu naamini tutafunguana macho
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Umelala doro wewe!
  Holier than thou!! yale yale tu!
  nshakueleza kwenye ile post yako kwenye jukwaa la starehe! kwanza sijui ulifuata nn kule.
   
 7. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Wewe ni msemaji wao?
   
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Pathetic!
  Get a life man! inaonekana huko kwenu na mitume wenu ndo wanawatishia msipotoa hela yote Mungu atakuponda!!~
   
 9. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  jamani, mbona mnamuandama huyu mamaa wakati amesema kitu cha maana tu. tatizo lenu ninini? wewe unayetukana unataka kunyosha kidole kwa mtu mwingine kama ni muovu, mbona nyinyi pia ni watumishi wa shetani vilevile? hapo mnadiscuss au mnashambulia, ajabu jamani.
   
 10. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Baada ya kusema hayo, tuambie wewe unataka tu-discuss au tushambuliane!
  Chagua upande!
   
 11. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Wakuu,

  I think it is imperative to go by the Word, and let the Bible translate the Bible and LET THE WORD speaks for its self.

  Now, let us go back to the Bible ambayo ndio our Book of Law.

  In the Book of Matthew Chapter 7 Vesre 1, Jesus said as follows: Do not judge, or you too will be judged. Now, who are we to judge Gods ellects?

  How often have we heard that warning, JUDGE NOT? Yet it is such an easy one to forget, especially when another person's sins seem to be so grievously wrong, so obviously wrong. Sometimes we can't help but ask ourselves, "How could anyone do such a thing?" Au sio?

  Verses to guide us:


  For with what judgment ye judge, ye shall be judged: and with what measure ye mete, it shall be measured to you again.

  And why beholdest thou the mote that is in thy brother's eye, but considerest not the beam that is in thine own eye?

  Or how wilt thou say to thy brother, Let me pull out the mote out of thine eye; and, behold, a beam is in thine own eye?

  Thou hypocrite, first cast out the beam out of thine own eye; and then shalt thou see clearly to cast out the mote out of thy brother's eye.

  Give not that which is holy unto the dogs, neither cast ye your pearls before swine, lest they trample them under their feet, and turn again and rend you.

   
 12. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Maxshimba umenene,
   
 13. N

  Ngala Senior Member

  #13
  Mar 18, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuwenai macho na manabii wa uongo. Je waliosadikishwa kule Mbeya kuwa mwisho u tayari wakaacha makaazi yao wakahamia porini wakisubiri mwisho wa dunia je mchunga huyo aliwatendea haki waumini wale na haitupasi kuhoji? DIA Walihamia Wasabato masalia waloaminishwa kusafiri kwenda ughaibuni bila pass eti kwa uwezo wake muumba je kwa nini wasipae kimiujiza hadi walikotaka badala ya njia za kibinadamu. Kuhoji hilo nalo twaogopa kupondwa? Hatutapondwa hata kidogo maana walo ndani hawajui kama wametekwa kiakili ni wajibu wetu kuwaokoa kabla KIBWETERE HAJAWAADHIBU na kwa kutenda hiio tutakuwa tumewatoa kwenye MOTO. BASI NATUTIMIZE WAJIBU WETU
   
 14. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kama kweli uko serious na kujua nani ni nabii wa uongo na nani ni Nabii wa Mungu,kwanza inabidi mcha Mungu,kwani vinginevyo mawazo yako yanatawaliwa na ibilisi na lolote utakalo taka kujua kuhusu Mungu ibilisi atakupotosha.
  Huwezi kupata mambo ya Mungu kwenye mtandao kwa kusikiliza mawazo ya watu,usi socialize mambo ya Mungu.Piga magoti omba Mungu akuoneshe nuru yake,ni mtumishi gani akuongoze na si kuleta ushabiki kwenye mambo ya Mungu.
   
 15. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  NABII WA UONGO WA KWANZA NI Muhamad saw, anayeabudiwa na waislam, kwasababu hamkiri Yesu kristo kuwa alikuja duniani kuokoa wanadamu. this is one of the ingredients kumtambua nabii wa uongo ni yupi.

  kwahabari ya wachungaji, hakuna haja ya kujadiili hili, Mungu ndiye anayejua, na Mungu ndiye mhukumu kwasababu wanamtaja Yesu. ile nilitaka kusema to clearly what the Bible says kuhusu roho gani ni ya nabii wa uongo na ipi ni ya nabii asiye wa uongo. hii mada imeletwa na mtu ambaye shetani anakaa ndani yake, spirit ya anti-christ iko ndani yake, na anatumiwa kupinga kazi ya Mungu.
   
 16. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  wateule muwe macho hizi ni siku za mwisho kwani yale yaliyotabiriwa sasa yametimia.

  nakubaliana na mtoa mada.
  namjua mchungaji mmoja maarufu nilkua nasali ktk ministry yake lkn nikaja gundua kuwa anatumia elimu aliyokuwa nayo kuwaibia wanaotafuta kuwa karibu na mungu.
  hata hivyo sielewi kwa nini watu wa mungu hawayaoni matendo mabaya ya manabii hawa kwani tuliambiwa tuwatambue kwa matendo yao.
  wanaoibiwa na watu hawa ni wale waliokosa maarifa ya kupambanua mambo kwani hata neno linasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
  wajinga ndio waliwao.
  mi mtu hawezi kuniambia eti nikeshe na kupigwa na jua kulinda mabango cjui kuzuia tanesco au kuibiwa mihela in form of sadaka wakati naweza kutoa sadaka yangu kwa kuwapa watoto wa mitaani chakula.
  mi nawashauri mkitaka kutoa sadaka tafuta wenye shida uwasaidie kulingana na mfuko wako na hii ndio itasaidia kuwaondoa manabii wauongo na kuwabakiza wachungaji kondoo wa ukweli maana wakikosa mapato watavua majoho.
   
 17. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  wengine wanaweza, wewe usiyeweza nyamaza kimyaa, fanya yanayokuhusu. usihamasishe wengine wanaopenda kufanya hivyo. mtoa mada ana yake, hana maana yoyote kwa kifupi. anatumiwa na antichrist roho chafu ya shetani inamsumbua, hata hajielewi.
   
 18. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  shetani akishindwa kubomoa imani za watu hutumia watu, angalia hekima na maarifa ni muhimu kwenye ktoa hoja kwenye kadamnasi hasa zinazo husu mambo ya kiroho, hakuna mwenye uhakika na namna gani nabii wa ukweli yuko, na namna gani nabii wa uongo anakuwa, nijualo mimi ni kwamba nabii ni mwanadam kama wanadamu wengine na unabii wake unakuwa anapokuwa na ujumbe toka kwa MUNGU si kila mahari anakuwa nabii, hata mwanafunzi hukamisha uanafunzi pale anapokuwa amevaa sare za shule na yuko shuleni,
   
 19. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #19
  Mar 19, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ni kweli watumishi wa Mungi ni kama wanadamu wengine na wanakosea, nyakati za biblia Daudi alikuwa mtumishi wa Mungu haswa alitenda kosa kumchukua mke wa Uria na kumuweka Uria mstari wa mbele akauliwa, lakini alipojua kosa lake alitubu, Mungu akamsamehe na bado akaendele kumtumia na wala hakumuacha, watu huwa wanaanguka lakini wanarekebisha makosa wanasimama tena.
   
 20. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Vita vyetu si vya nyama, ni dhidi ya mamlaka na falme katika ulimwengu wa kiroho nimequote. So please Watu wa Mungu, tuombeane bila kuchoka sisi ni mwili wa Kristu, sasa jicho linampinga goti, miguu na mikono haipatani, tumbo na sikio ndio hivyo, adui yetu sio George wala Nelson, au Joyce wala Asha, ni ibilisi yule muovu, wala hatutaokolewa kwa matendo yetu wala mavazi yetu wala kuhubiri kwa mimbari au kwa JF forum, ni kwa kuomba tu. Dont point finger to anyone remember God May not always Give us answers, But He Always Gives us GRACE FREELY someni Job 14 especial Job 14:1 yule Man anayezungumziwa ni binadamu wote. Be Blessed, Mwenye Sikio na Asikie
   
Loading...