wewe ndiyo nabii wa uongo, nakushauri kitu kimoja, issue kamahizi ambazo hauna uhakika na unachokiongea, usiweke public, sijui umri wako. ni kwanini nasema hivi, huwezi jua, pengine hao watu ni watu wa Mungu kweli, na wewe ukapanda mbegu chafu kwa mamilioni ya wana jf hapa, wakamtukana Mungu, au wakamuacha Mungu au ukawa umezuia kazi ya Mungu kwa upande fulani, hauna uhakika, MZIGO WOTE HUO UTAUBEBA WEWE ULIYELETA HII MADA MBELE ZA MUNGU. kama Mungu atatukanwa, you will be accountable, kama watu hawataokoka kwasababu wewe umesema, you will be accoutable, kama watu watatukana wokovu wa Yesu, you will be accountable. na utavuna unachopanda. kumbuka, washindanao na Bwana watapondwa kabisa, Mungu anao uwezo wa kumponda kabisa mtu anayezuia kazi yake, sasa hii post yako angalia isijekuwa inapingana na mapenzi ya Mungu, kwasababu nakuhakikishia utapondwa kabisa. pia, hovyo, kaa tayari, lolote laweza kutokea kwako kuanzia sasahivi, pengine kwa kuleta hii mada hapa, utasababisha madhara mengi kwenye kazi ya Mungu. huwezi jua ndugu. ndio maana ni bora kuwa na busara na hekima.
Mwana wa Mungu, jua biblia inasema mtawatambua kwa matendo yao. Ikiwa yeye ameona matendo yao hayaendani na matendo ya watumishi sahihi wa Mungu, ana haki ya kusema. tafadhali usimhukumu. ikiwa wewe ni mmoja wa wale mnaowekwa viti vya mbele basi ujue wapo ambao hawathaminiwi wanawekwa viti vya nyuma kama alivyosema.