Mamlaka za maji mnaturudisha nyuma

CORONAZ

Senior Member
Apr 26, 2020
181
337
Wana majina mazuri na marefu, Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka ya.. Kimuundo walipaswa wawe na Kurugenzi 2, ya maji safi na ya maji taka.

Hebu angalia mjini kwako, ni watu wangapi wanapata maji safi na wangapi wameunganishwa na mfumo wa maji taka (haswa maji taka)? Wamelala!

Mjini kila nyumba ina shimo la maji taka? Maghorofa? Shule? Hospitali? Hoteli? Kweli? Ukiuliza mipango, hamna?

Hebu angalia bili yako ya mwezi! Hawajajumuisha maji taka?

Gari la maji taka hapo ulipo linadai bei gani? Hii si huduma ilipaswa itolewe na mamlaka husika?

Tuwafanyeje hawa?
 
Nadhani kuna mahali unajichanganya; kwanza haziitwi Mamlaka za Majisafi na Maji Taka bali Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira, lakini pili hazishughuliki na mashimo ya maji taka yaliyopo majumbani.

Kazi za Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira ni kusambaza maji safi kwa ajili ya matumizi ya majumbani na kusafisha maji taka katika mabwawa maalumu kutoka majumbani.

Sasa maji taka kutoka majumbani yanaweza kufikishwa katika mabwawa ya kusafishia maji kwa kutumia magari ya majitaka au mfumo uliojengwa kupeleka majitaka.

Wale watu waliounganishwa na mfumo wa majitaka huambatanishiwa ankara za kutoa majitaka na wengine ambao hutumia magari kuondoa majitaka majumbani mwao hutozwa na makampuni husika ya magari au Mamlaka kama magari yao yametumika.
 
Kutokana na hali inayoanza kujitokeza ya kipindupindu Mamlaka zihakikishe zina madawa ya kutosha kutibu maji vinginevyo janga linakuja na hasa ukizingatia mafuriko yanayoendelea.
 
Nadhani kuna mahali unajichanganya; kwanza haziitwi Mamlaka za Majisafi na Maji Taka bali Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira, lakini pili hazishughuliki na mashimo ya maji taka yaliyopo majumbani.

Kazi za Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira ni kusambaza maji safi kwa ajili ya matumizi ya majumbani na kusafisha maji taka katika mabwawa maalumu kutoka majumbani. Sasa maji taka kutoka majumbani yanaweza kufikishwa katika mabwawa ya kusafishia maji kwa kutumia magari ya majitaka au mfumo uliojengwa kupeleka majitaka. Wale watu waliounganishwa na mfumo wa majitaka huambatanishiwa ankara za kutoa majitaka na wengine ambao hutumia magari kuondoa majitaka majumbani mwao hutozwa na makampuni husika ya magari au Mamlaka kama magari yao yametumika.
Wewe ni mhusika. Umejitahidi kupindisha. Hoja hapa kwanini watu wachimbe mashimo wakati walipaswa kuunganishwa na mfumo wa maji taka? Kwanini mifumo hii haiendelezwi mijini?
 
Wewe ni mhusika. Umejitahidi kupindisha. Hoja hapa kwanini watu wachimbe mashimo wakati walipaswa kuunganishwa na mfumo wa maji taka? Kwanini mifumo hii haiendelezwi mijini?
Mifumo yote miwili inakubalika kitaalamu kwa hiyo hakuna tatizo. Lakini siyo kila mahali unaweza kuunganisha mfumo wa majitaka kwa sababu ya maumbile (topography) ya sehemu husika, kwa maana ya milima, mabonde na tambarale.

Kubwa zaidi pambana na Serikali ya mama Samia itafute fedha kwa ajili ya ujenzi wa mifumo hiyo kwa kuwa makusanyo ya ankara za maji hayatoshi kwa ajili hiyo. Mamlaka za Maji zitakushukuru sana kama utashiriki katika kutoa msukumo wa upatikanaji wa fedha.
 
Nshaeahi kusema hawa jamaa hawana akili.

Kwenye hili eneo kuna mfumo wa kupata pesa nzur sana. Kutengeneza mtandao wa kutap maji taka kutoka majumbani.

Majiraka yenyewe ni resources
Kuyatape na kupata mapato kwa mwezi kwaenye majumba ni mrqdi wanafeli wapi hawa viumbe.

Mwigulu na wachumi wenzie ndio wanasubiri wale wanenepe tuuu??
 
Back
Top Bottom