Eyes of Tanzania
Member
- Jan 22, 2017
- 10
- 29
Hivi majuzi tumethibitishiwa kwamba Mh. Judge Donnely wa Mahakama Kuu ya USA hapo New York ameweza aliwasikiliza hoja za wanaharakati na kuamua kusimamisha kwa muda Amri ya Rais Donald J Trump hadi uhalali wa amri hiyo uchunguzwe. Amri hiyo ilihusu zuio la Rais kwa watu wanaoingia USA kutoka katika nchi zinzotuhumiwa na Marekani kwamba zinazalisha magaidi (terrorists)
Ninaomba kuuliza kwa Wataalamu wa sheria ktk ukanda huu wa Afrika ya Mashariki, Je kuna Mahakama yeyote yenye Mamlaka ya kusimamisha/kutengua amri ya Rais kama itadhihirika kwamba imekwenda kinyume na Katiba?