Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Kariakoo imewashinda?

Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Kariakoo imewashinda?

pole sana mkuu,huyo jamaa alikudharau sana ila me nimeshazoea kutodai risiti maana kila duka huwa hawatoagi risiti machache sana yanatoa na wakikupa kama imefutika hivi kwa hyo me nikaona niachane nazo labda mzigo wanavyoingiza kuna makodi mengi

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kweli mkuu ni kasumba ya uwizi iliyojengeka ukiuliza risit mbona haiko sawa, utasikia hiyo si ya njiani tu..!
Inashangaza kama wanapata hasara kwanini wasifunge hizo biashara zao.?
Ni uwizi mtupu.
Ndio maana mataifa mengine tunapewa sifa mbovu mbovu tu unaenda mahali unaulizwa wewe mswahili nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo risiti hawakupi bila ya wewe kukubali na wateja wanaopewa hizo ni wale wateja wa Siku nyingi kwenye hayo maduka wanajuana na wauzaji hawawezi kukupa hyo risiti kama hakujui.
 
Sio kweli hata kidogo, sio suala la kupunguziana linalosababisha utoaji wa risit pungufu, hii ni hulka na tabia ya watu binafsi wanaoona wakitoa risiti kamili watapata hasara.
Mbona michezo hii haichezwi na wahindi ama wageni walio na biashara kwenye Nchi yetu? Hata hapo hapo kariakoo, shida iko zaidi kwenye maduka ya wakinga na Wachaga mna matatizo gani?..

Sent using Jamii Forums mobile app
Wahindi hawafanyi hii michezo? Unauhakika?
 
Narudia tena kuleta huu uzi hapa je TRA eneo la kariakoo limewashinda? Hii tabia ya kiburi ya wafanyabiashara kutoa risiti isiyoendana na mauzo ndio utaratibu mlio uruhusu? Kama mnajifanya hamna habari hivi ni kweli hamna kitengo cha uchunguzi?
Hivi mzigo wa laki tano unapewa risiti ya tsh 50,000 hiyo ni sawa?

Hii tabia inakera sana kwa sisi ambao sehemu nyingine tunalipa kodi kwa uhalali kwa nini wengine wafaidike kwa migongo yetu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini uende kariakoo? Nenda Tailand, China, Uturuki na kwingine mwenyewe kwani kuna mtu amekushikia bunduki kununua dukani kwake ndugu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hiyo ni kasumba tu tuliyolishwa na wanasiasa kwa makusudi yao ya kisiasa, sio kweli kuwa kodi inatumika ndivyo sivyo wengi wanaosema kodi inatumika ndivyo sivyo ndio hao hao wasiolipa kodi na humu Jamii Forum ndio chimbo lao.
Nimezunguka Nchi hii karibu mikoa yote hiyo miundo mbinu inayojengwa ingejengwa vipi kama kodi ingekuwa haitumiki inavyotakiwa?
Na ni kwanini wanaopinga kutoa risit stahiki ni hawa tu wa kariakoo?

Huu ni uzi wangu wa Tatu nazungumzia kariakoo tu, yaani ni wao tu wasio pata faida Nchi nzima?
Mkuu nimekusanya ushahidi wa kutosha kuna watu wakiendelea na malumbano humu, na kashfa zao nitawaumbua na bila shaka watafilisika..
Nilikerwa sana na aliyenirudishia pesa yangu eti kisa nimedai risiti halali kwa pesa niliyotoa, akiniambia

"kimzigo cha laki nane tu nikupe risiti yote kama utaki acha"!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hawa dawa yao ni kuwachoma tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hawa dawa yao ni kuwachoma tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Bado Taifa lina watu kama nyinyi ama kweli sio samaki wote wenye harufu waweza kuwa wameoza.
Ahsante mkuu, kwa kuona upande mzuri wa Uzi wangu.

Inashangaza sana hawa watu, bado watu wakiborongo kwenye michezo wanadai sio wazalendo, kukitokea upungufu wowote kwenye taasisi za serikali wanapiga kelele hakuna uzalendo, sijui huo uzalendo wanao uimba kutwa ni upi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado Taifa lina watu kama nyinyi ama kweli sio samaki wote wenye harufu waweza kuwa wameoza.
Ahsante mkuu, kwa kuona upande mzuri wa Uzi wangu.

Inashangaza sana hawa watu, bado watu wakiborongo kwenye michezo wanadai sio wazalendo, kukitokea upungufu wowote kwenye taasisi za serikali wanapiga kelele hakuna uzalendo, sijui huo uzalendo wanao uimba kutwa ni upi.


Sent using Jamii Forums mobile app
watanzania bado ni wanafiki sana!! Wanashadadia mtumishi kutumbuliwa kwa kuiba laki 8 wakati wao kila siku wanaiibia nchi kwa kutolipa kodi!! Cha ajabu zaidi hawa wasiolipa kodi kila siku wanadai mazingira bora ya biashara, wanadai miundombinù mizuri, wanadai madawa hospitalini, Unajiuliza hivi vitu vinatoka wapi kama watu hawalipi kodi!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom