Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Kariakoo imewashinda?

Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Kariakoo imewashinda?

Kuna tatizo kidogo la ku upload risit huenda ni shida ya network ikikaa sawa mtaziona ziko kama 30 kwa maduka tofauti tofauti na bidhaa tofauti nitaweka na picha za hizo bidhaa.. pia kiwango cha mzigo ulionunuliwa.
Mkijua kukosoa wenzenu nanyi pia muwe tayari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha umbea
Hata ukiweka hauwezi saidia kitu
 
Sisi hatukerwi maana hakuna mnachkfanyia kodi zetu
 
TRA wanajua sema na wao ndo kitega uchumi chao..yaan kariakoo ndo eneo lao la kuhujumu uchumi vizuri...so mbwa hawezi kumla mbwa.
Hili ndilo waziri wa fedha na mkuu wa Nchi wanalopaswa kulifahamu sidhani kama watumishi waaminifu kwenye Taifa hili wameisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes, unapunguziwa bei unapewa receipt ya hela ndogo ukitaka upewe receipt ya malipo halali bei inapanda.

Mtoa mada anataka kutuharibia tukienda tuuziwe vitu kwa bei kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kweli hata kidogo, sio suala la kupunguziana linalosababisha utoaji wa risit pungufu, hii ni hulka na tabia ya watu binafsi wanaoona wakitoa risiti kamili watapata hasara.
Mbona michezo hii haichezwi na wahindi ama wageni walio na biashara kwenye Nchi yetu? Hata hapo hapo kariakoo, shida iko zaidi kwenye maduka ya wakinga na Wachaga mna matatizo gani?..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Narudia tena kuleta huu uzi hapa je TRA eneo la kariakoo limewashinda? Hii tabia ya kiburi ya wafanyabiashara kutoa risiti isiyoendana na mauzo ndio utaratibu mlio uruhusu? Kama mnajifanya hamna habari hivi ni kweli hamna kitengo cha uchunguzi?
Hivi mzigo wa laki tano unapewa risiti ya tsh 50,000 hiyo ni sawa?

Hii tabia inakera sana kwa sisi ambao sehemu nyingine tunalipa kodi kwa uhalali kwa nini wengine wafaidike kwa migongo yetu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ondoeni Wamachinga milangoni mwetu tutoe lisiti halali
 
Ingependeza zaidi ungeleta mifano na majina ya maduka pia..
 
Sio kweli hata kidogo, sio suala la kupunguziana linalosababisha utoaji wa risit pungufu, hii ni hulka na tabia ya watu binafsi wanaoona wakitoa risiti kamili watapata hasara.
Mbona michezo hii haichezwi na wahindi ama wageni walio na biashara kwenye Nchi yetu? Hata hapo hapo kariakoo, shida iko zaidi kwenye maduka ya wakinga na Wachaga mna matatizo gani?..

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaongelea wachina na wahindi wa wapi wewe.!
 
Ukitaka kodi halali mzigo wa laki tano inabidi uongeze aslimia kumi na nane....

Kwa maana hiyo ulipe 580,000 ama laki sita...
 
Mleta mada nimependezwa nawe Kwa jinsi ulivyojaribu kuonesha uzalendo!
Kariakoo sijui wataacha lini hiyo kasumba!
WaTZ tuwe tunadai risiti za manunuzi za mashine na kisha kuisoma risiti kuona kama iko Sawa na kiasi cha pesa Mtu alicholipa!
 
Back
Top Bottom