Mkuu hiyo ni kasumba tu tuliyolishwa na wanasiasa kwa makusudi yao ya kisiasa, sio kweli kuwa kodi inatumika ndivyo sivyo wengi wanaosema kodi inatumika ndivyo sivyo ndio hao hao wasiolipa kodi na humu Jamii Forum ndio chimbo lao.
Nimezunguka Nchi hii karibu mikoa yote hiyo miundo mbinu inayojengwa ingejengwa vipi kama kodi ingekuwa haitumiki inavyotakiwa?
Na ni kwanini wanaopinga kutoa risit stahiki ni hawa tu wa kariakoo?
Huu ni uzi wangu wa Tatu nazungumzia kariakoo tu, yaani ni wao tu wasio pata faida Nchi nzima?
Mkuu nimekusanya ushahidi wa kutosha kuna watu wakiendelea na malumbano humu, na kashfa zao nitawaumbua na bila shaka watafilisika..
Nilikerwa sana na aliyenirudishia pesa yangu eti kisa nimedai risiti halali kwa pesa niliyotoa, akiniambia
"kimzigo cha laki nane tu nikupe risiti yote kama utaki acha"!
Sent using
Jamii Forums mobile app