Mamlaka ya Hali ya Hewa au Mamlaka ya Hali ya Hela?

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Leo tarehe 17, wiki mbili tangu kuanza kwa mwezi huu wa oktoba ambapo TMA walitabiri zingenyesha El Nino. Hakuna El Ninyo, japo manyunyu.

Sisemi haya kumaanisha natamani El Nino, la hasha. Hapa ninahoji uwezo wa hii Mamlaka ya hewa kama wanazo nyenzo na maarifa kamili ya kuweza kutupatia weather updates. Kuna haja ya kuhoji maana hawa wanaonesha udhaifu ambao kwa kweli ipo siku watakuja kusema hali ya hewa ni shwari hafu maafa yakatokea.

Ndiyo nahoji, mbona Wamarekani wanakuwa wanatabiri kutakuwa na kimbunga na kunakuwa na kimbunga kweli? Afu watu hawahawa wanakula hela za kodi zetu kama mishahara kwa kwa utabiri wa kienyeji namna hii.

Ndo sababu nahoji kama hii ya kwetu ni Mamlaka ya Hali ya Hewa au Mamlaka ya Hali ya Hela.
 
PAle mamlaka ya Hali ya Hela wote hawana sifa za kufanya ile kazi. Mwanzo walituambia kuwa Mwezi Sept 2012 mvua kubwa itanyesha, kisha walipoona mwezi Sept unaisha wakasema mvua zinakuja mwezi Oct. 2012.

Sasa na Oct inaisha wiki ijayo;

Sijui watakuja na Movie ipi tena.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Hakuna kitu pale. Akina Kijazi wanakula kodi zetu bure.

Utakuta kwenye utabiri wao wa kwenye tivi wanatabiri vyote, mfano,, "kutakua na mvua, ngurumo, jua au upepo katika baadhi ya maeneo" sasa hapa sijui wametabiri nini.

Kazi yao kushinda kwenye internet jukwaa la kikubwa tu.
 
Halafu mimi na huu ulofa wangu na hizi kodi kubwax2 nazokatwa,halafu kuna mabwege wamekaa wanakula tu hela zetu,hawana hata kazi moja ya maana wanayofanya zaidi ya upuuzi tu.natamani nipewe rungu niwanyuke hawa watu basi tu.
 
PAle mamlaka ya Hali ya Hela wote hawana sifa za kufanya ile kazi. Mwanzo walituambia kuwa Mwezi Sept 2012 mvua kubwa itanyesha, kisha walipoona mwezi Sept unaisha wakasema mvua zinakuja mwezi Oct. 2012.

Sasa na Oct inaisha wiki ijayo;

Sijui watakuja na Movie ipi tena.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
Tunaomba radhi kwa usumbufu mlioupata.
Sasa tunatangaza rasmi kwamba kutakua na mvua kubwa nchi nzima kuanzia tar06.11.012.ni mvua itakayonyesha usiku na mchana(day & night)kwa muda wa miezi4.
Kwahiyo wa mabondeni hameni.
Imetolewa na mamlaka ya hali ya hewa:
 
Tunaomba radhi kwa usumbufu mlioupata.
Sasa tunatangaza rasmi kwamba kutakua na mvua kubwa nchi nzima kuanzia tar06.11.012.ni mvua itakayonyesha usiku na mchana(day & night)kwa muda wa miezi4.
Kwahiyo wa mabondeni hameni.
Imetolewa na mamlaka ya hali ya hewa:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ni Waganga wa Kiennyeji. Wanafanya utabiri kwa kutumia tunguri na ndio maana wanasema ndivyo sivyo. Cha ajabu wanalipwa mishahara mikubwa na magari ya kutembelea kwa gharama za kodi yetu


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Back
Top Bottom