Mamilioni ya DECI yalikuwa yanatunzwa ofisini-Shahidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mamilioni ya DECI yalikuwa yanatunzwa ofisini-Shahidi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Mar 18, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,236
  Likes Received: 414,667
  Trophy Points: 280
  Mamilioni ya DECI yalikuwa yanatunzwa ofisini-Shahidi


  Na Rehema Mohamed

  SHAHIDI namba sita katika kesi ya DECI, SP Suleman Nyakulinga amesema fedha zilizokuwa zikikusanywa katika matawi ya mikoani zilikuwa zikihifadhiwa
  ofisini.SP Nyakulinga aliyasema hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya hakimu Bw. Stuwati Sanga wakati akitoa ushahidi wake.

  Alidai kuwa kutokana na hali hiyo waliwashawishi wakurugenzi wa matawi hayo kupeleka fedha hizo benki na ndipo walipofanikiwa kuzizuia zaidi ya sh. bilioni 12 katika akaunti zilikowekwa.

  Fedha zilizozuiwa zipo katika akaunti ya benki ya NMB, Dar es Salaam Comunity Banki, Akiba na CRDB.

  Washitakiwa katika kesi hiyo ni Wakurugenzi wa DECI, ambao ni Bw. Jackson Mtares, Bw. Dominick Kigendi, Bw. Timotheo Ole Loitg’nye, Bw. Samwel Mtares na Mhasibu na Msemaji wa kampuni hiyo, Bw. Arbogast Kipilimba.

  Vigogo hao wanakabiliwa na mashtaka ya kuendesha na kusimamia mradi wa upatu na kupokea amana kutoka kwa umma bila leseni. Kesi itaendele tena kesho.
  [​IMG]
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,236
  Likes Received: 414,667
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Alidai kuwa kutokana na hali hiyo waliwashawishi wakurugenzi wa matawi   hayo kupeleka fedha hizo benki na ndipo walipofanikiwa kuzizuia zaidi ya   shbilioni 12 katika akaunti zilikowekwa.
  Kama huu ushahidi ni wa kweli hawa watu siyo wezi.......................mwizi hawatunzii aliowaibia kiasi kikubwa cha fedha namna hiyo..................
   
Loading...