Viongozi wa kampuni ya Prezzdar washtakiwa kwa ubadhilifu na uchepushaji

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Shauri la Uhujumu Uchumi namba 1638/2024 limefunguliwa Januari 10, 2024 Jamhuri dhidi ya Bw. Edward Jonas mashenene, Anurphus Mpanju, Ronald Semtanda, Resperius Ishengoma, Desidery Falician Ndibalema na Elgidius Eldelfonce Kamugisha ambao ni Wakurugenzi na Watendaji wa kampuni ya Prezzdar iliyoko jijini Dar es salaam.

Shauri hili limefungulia mbele ya Mhe. Rahim Mushi Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, Kinondoni.

Wakurugenzi hawa wameshtakiwa kwa kufanya Ubadhirifu na Uchepushaji wa kiasi cha shilingi Shs. 10,035,000 kinyume na kifungu cha 28 (2), 29 & 30 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 kama ilivyorejewa Mwaka 2019, fedha za Manispaa ya Kinondoni zilizotokana na makusanyo ya ushuru wa masoko.

Pia wameshtakiwa kwa kosa la kuongoza genge la uhalifu paragrafu 4 (1) (a) Jedwali la kwanza na 57(1) na (60) Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura 200 Rejeo la 2022

Kesi hii imeahirishwa hadi Januari 24, 2024 kwa ajili ya kusomewa hoja za awali.
 
Mleta taarifa za mahakamani hututendei haki kwakweli! Taarifa zako ni fupi mno ndio maana kuna watu wanajadili makabila badala ya content! Jitahidi kuboresha tafadhali.
 
Shauri la Uhujumu Uchumi namba 1638/2024 limefunguliwa Januari 10, 2024 Jamhuri dhidi ya Bw. Edward Jonas mashenene, Anurphus Mpanju, Ronald Semtanda, Resperius Ishengoma, Desidery Falician Ndibalema na Elgidius Eldelfonce Kamugisha ambao ni Wakurugenzi na Watendaji wa kampuni ya Prezzdar iliyoko jijini Dar es salaam.

Shauri hili limefungulia mbele ya Mhe. Rahim Mushi Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, Kinondoni.

Wakurugenzi hawa wameshtakiwa kwa kufanya Ubadhirifu na Uchepushaji wa kiasi cha shilingi Shs. 10,035,000 kinyume na kifungu cha 28 (2), 29 & 30 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 kama ilivyorejewa Mwaka 2019, fedha za Manispaa ya Kinondoni zilizotokana na makusanyo ya ushuru wa masoko.

Pia wameshtakiwa kwa kosa la kuongoza genge la uhalifu paragrafu 4 (1) (a) Jedwali la kwanza na 57(1) na (60) Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura 200 Rejeo la 2022

Kesi hii imeahirishwa hadi Januari 24, 2024 kwa ajili ya kusomewa hoja za awali.
Mbona kiasi kidogo sanaa
 
Back
Top Bottom