Mamia kupoteza ajira vituo vya mafuta

Kuna jamaa angu apa arusha yuko engen ameniambia kutokana na hali tete ya mauzo wamepewa zamu ya week mbili kazini week mbili likizo wakazi mwanzo aikua ivo maboss wake wanadai mauzo yako chini
 
Mkuu ni kweli usemayo lakini kumbuka uchumi kuuvuruga ni suala la miezi 6 hadi mwaka inatosha lakini kuurudisha kuwa credible, sensible pamoja na kuondoa economic panic hii inayoendelea na hatimaye kurudia hali yake ni suala linalochukua muda sana (ndivyo ilivyo ukitoa recovery path ya Asian crisis 1997).

Hii ni kwa sababu kurudisha uchumi katika hali yake kunategemea na strong government machinery (govt credibility), ikiwa pamoja na uwezo wa mapato yake yasiotokana na kodi (kwasababu tax revenue pia itayumba), uwezo wa kuhimili bailout mechanism (au uwezo wake wa kukopa) na strong manufacturing sector; sifa ambazo hatuna. Angalia Zimbabwe na Venezuela. Zimbabwe walitumia miezi tu kuharibu uchumi wao lakini kawaangalie hadi kesho hawajui watoke vipi. Zimbabwe iliyokuwa London ya Afrika na food basket leo inanuka harufu.

Kwa kifupi nadhani serikali imechemka kwa kuwa "too ambitious" katika kutekeleza sera zake pasipo kuzingatia scientific evidence kwa kila hatua inayochukuliwa. Tulisema sana huko nyuma kwamba huwezi kutekeleza baadhi ya sera kwa pamoja kwa pupa kiasi hicho, ni ima hizo sera zipokezane au iwe gradual basis. Utekelezaji wa sera kwa pamoja ni kitu cha hatari sana katika uchumi iwapo umakini hautazingatiwa kwa sababu sera sio namba kwamba 2+2=4!!!. Simetimes ni suala la try and error.

hili suala la uhakiki usioisha lina athari sana katika uchumi kwasababu watumishi wa umma hawajui nini kitatokea kesho hivyo wako "too sensitive" katika kutumia kitu ambacho kinaongeza panic.

Kuna mambo saba ya muda mfupi yanaweza kufanyika ili ku-rescue hali inayoendelea. Lakini wacha waisome namba.
Kiongozi kuongoza nchi ni jambo gumu sana, any way nakubali mawazo yako.
 
Kiongozi kuongoza nchi ni jambo gumu sana, any way nakubali mawazo yako.
Nakubaliana na wewe. Gumu sana. Lakini kiongozi yoyote akiwa shirikishi na kuruhusu mawazo hata ya walio chini yako mara nyingi uongozi unakuwa rahisi na wenye baraka. Kisa cha Queen of Sabah (sheba) kinatoa fundisho zuri sana umuhimu wa kutaka ushauri katika mambo hata kama wewe ni malkia.
 
Nakubaliana na wewe. Gumu sana. Lakini kiongozi yoyote akiwa shirikishi na kuruhusu mawazo hata ya walio chini yako mara nyingi uongozi unakuwa rahisi na wenye baraka. Kisa cha Queen of Sabah (sheba) kinatoa fundisho zuri sana umuhimu wa kutaka ushauri katika mambo hata kama wewe ni malkia.

Mkuu viongozi wengi wa Africa ni tofauti na wa mabara mengine.
 
Back
Top Bottom