Mameneja na Waratibu wa Mradi wa TACTIC watakiwa kutumia magari 14 katika kazi iliyokusudiwa

Mameneja na Waratibu wa Mradi wa TACTIC watakiwa kutumia magari 14 katika kazi iliyokusudiwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe amewaelekeza Mameneja na waratibu wa Mradi wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) kuhakikisha magari 14 aliyoyakabidhi yanakwenda kufanya kazi iliyokusudiwa ya usimamizi wa mradi huo ili wananchi wanufaike na barabara, masoko na stendi zinazojengwa kupitia mradi huo.

Prof. Shemdoe ametoa maelelezo hayo leo Februari 21, 2026, wakati wa hafla ya kukabidhi magari hayo kwa Mameneja wa TARURA wa Miji 12 ya kundi la kwanza la Mradi wa TACTIC, iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Millenium Tower Kijitonyama, Dar es Salaam.

“Magari haya yamenunuliwa kwa fedha za umma, hivyo yatunzwe na yakatumike kwa kazi za usimamizi wa mradi wa TACTIC na si nyinginezo,” amesisitiza Prof. Shemdoe.

Aidha, Prof. Shemdoe amewata wakandarasi walio kwenye maeneo ya utekelezaji wa miradi ya TACTIC, kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi kwa kuzingatia mikataba waliosaini ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati, na kuongeza kuwa Serikali haitosita kusitisha mikataba inayosuasua kwa mujibu wa sheria na vipengele vya mikataba husika.

Prof. Shemdoe amesema Serikali haina changamoto ya kukosa fedha za utekelezaji miradi, kwani pindi mkandarasi akiwasilisha hati ya maombi ya malipo analipwa kwa wakati, hivyo hakuna sababu ya wakandarasi kushindwa kukamilisha na kukabidhi miradi kwa wakati.

Kwa upande wake, Meneja wa TARURA Wilaya ya Sumbawanga Mhandisi Albert Kyando ameishukuru Serikali kwa kuwakabidhi magari yatakayowawezesha kusimamia miradi ya TACTIC kwa karibu na kuahidi kuwa watayatunza kama Prof. Shemdoe alivyoelekeza kwa maslahi ya umma na taifa.

Naye, Mmoja wa Madereva waliokabidhiwa magari hayo kutoka Jiji la Arusha Bw. Joshua Magati, amesema watayatunza magari hayo kama alivyoelekeza Prof. Shemdoe, na kuongeza kuwa watazingatia muda wa kuyafanyia ukaguzi na matengenezo pamoja na kuyatumia kwa kazi iliyokusudiwa ya usimamizi wa miradi ya TACTIC.

OWM - TAMISEMI, Dar es Salaam
 
Mkatunze hela zetu sio kukimbizana na vijana wa crown(walionunua kwa pesa zao na service wanafanya kwa pesa zao zisizo na kona kona kutoka wakati wa services ukifika)
-Pia mkatii sheria barabarani sio mjikute nyie ndio barabara zenu..fujo fujo..overtake hovyo hovyo pasipo kujali sisi tuliolipa kodi mkakalia hayo magari.

-Muwa na adabu na hayo magari mpakaki sehemu zinazowahusu sio saa tisa usiku uko nalo bar...vichochoroni huko.

- Na nyie wakuu wa vitengo mkiletewa mambo time za services mtoe hela kwa wakati..sio mnakalia pesa hizo ni gari za thamani sio mishumaa ya jero jero hiyo.Muwe na akili muendane na wakati..unavimbia hela za services ni za Mama yako au baba yako?Sio hela za ukoo hizo.

-Muone aibu kupaki magari mazuri then hayatembei kisa vitu vidogo vidogo.Yakiwashinda mje tuwasaidie namna ya kutunza magari kwa ufanisi.
 
Back
Top Bottom