Mambosasa: Jeshi hilo limebaini uwepo wa vikundi vya watu wanaofanya mikutano ya siri ili kuhamasisha vurugu na maandamano

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
2,941
2,000
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Lazzaro Mambosasa, amesema jeshi hilo limebaini uwepo wa vikundi vya watu wanaofanya mikutano ya siri ili kuhamasisha vurugu na maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Amesema jeshi hilo limejipanga vyema kuhakikisha halitoi nafasi ya kufanyika kwa vurugu ili kuheshimisha Demokrasia nchini na maamuzi ya wananchi.

Amevitahadharisha vikundi hivyo viache mara moja mipango hiyo kwani vitakutana na adha kubwa ya Vyombo vya Dola.

Kadhalika Mambosasa, ameongeza kwa kuwataka wananchi watoe taarifa kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pindi wanapobaini ama kuhisi uwepo wa watu wanaohamasisha vurugu ili kudhibiti hilo mapema.
 
Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
11,478
2,000
Watoe taarifa kwa Njia ya Whatsapp... ingependeza zaidi...

Fungueni..... in Haji Manara's voice!
 
abdulhamis

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
957
1,000
Chadema kama kwel mmechaguliwa na Wana nchi na mmeibiwa kura bas mbowe aandamane Hai sugu mbea Zito kigoma Yan fanyeni maandamano nchi nzima sio wote mjikusanye Dar mtakua ni kakikund ka wahun mnataka mfanye vurugu
 
Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
6,762
2,000
Screenshot_20201029-210120.png
 
Mhujumu Uchumi

JF-Expert Member
Sep 14, 2014
1,333
2,000
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Lazzaro Mambosasa, amesema jeshi hilo limebaini uwepo wa vikundi vya watu wanaofanya mikutano ya siri ili kuhamasisha vurugu na maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Amesema jeshi hilo limejipanga vyema kuhakikisha halitoi nafasi ya kufanyika kwa vurugu ili kuheshimisha Demokrasia nchini na maamuzi ya wananchi.

Amevitahadharisha vikundi hivyo viache mara moja mipango hiyo kwani vitakutana na adha kubwa ya Vyombo vya Dola.

Kadhalika Mambosasa, ameongeza kwa kuwataka wananchi watoe taarifa kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pindi wanapobaini ama kuhisi uwepo wa watu wanaohamasisha vurugu ili kudhibiti hilo mapema.
Apeleke usengh wake zero brain kabisa huyu bwana.
Jeshi liliajiri form four failure matokeo yake ndo haya.
Asubiri aone tutachofanya kenge yeye
 
Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
6,119
2,000
Sasa kama anataarifa si aende huko walipo akawakamate anatuambia sisi ili iweje?

Akili za kitoto hizi,
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom