Mambo yasiwe mengi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,606
729,498
Si jambo la kificho tena kwamba kuna kuyumba kwenye maamuzi na ubaguzi wa kuchagua huku kama taifa tukikosa msimamo na mtazamo sahihi katika yale yatokanayo na mikakati maono na vipaumbele vya taifa
Ni kama vile tuko kwenye sera moja tu ya kuhakiki nyaraka binafsi na za kitaasisi, kufanya teuzi na kutengua, kushika hapa na kuachia pale hata kabla hatujamaliza kukaza vema pale tuliposhika
Sijaona ukamifu kwenye lolote mpaka sasa... Tusifanye hosteli za chuo kama mfano na zile ndege kwakuwa maamuzi yake hayakuwa ya kitaasisi bali amri ya mtu mmoja tu.... Kuna walakini mkubwa utatokea huko mbele
Hili lililoibuka la wafanyakazi waliokuwa wanatumia majina ya wengine kufukuzwa kazi maramoja na kunyimwa haki zao zote litaleta janga kubwa mno... Tutegemee vifo vingi na familia nyingi kuyumba, tutegemee kuona watoto wa mitaani na machungodoa wezi na vibaka wakiongezeka... Maana watoto watafukuzwa shule kwa wazazi waliofukuzwa kazi kushindwa kulipa karo... HILI LITAZAMWE UPYA TAFADHALI.... wale wazee wenye nguvu hekima ya kushauri wafanye hivyo haraka .....
Yale yaliyoahidiwa wakati wa kuomba ridhaa ya kuongoza yatimizwe bila upendeleo bila kengeza bila jazba bali kwa hekima heshima na weledi... Kutumia nyaraka zisizo zako na kujimilikisha ni kosa la jinai na si mambo ya kitaaluma.. ....
Niishie hapa Kwanza

As a leader please deliver every promise.....without prejudice....!!?
 
Nilichukua fomu mwenyewe. Nina jiamini na hapa maneno ni mawili tu. Ka Taaaa. Ushauri wako weka kwako hapa ni kutumbua tuuuu.
Mkuu, kama umehusika au una ndugu yako aliyekutwa, mwambiye atii mamlaka na kabla ya 15th May awe kishaondoka. Ysije mkuta ya chura, kukaa majini lakini weupe hana.
 
tapatalk_1490437105033.jpeg

Naomba nisiongeze neno hapa....
 
Si jambo la kificho tena kwamba kuna kuyumba kwenye maamuzi na ubaguzi wa kuchagua huku kama taifa tukikosa msimamo na mtazamo sahihi katika yale yatokanayo na mikakati maono na vipaumbele vya taifa
Ni kama vile tuko kwenye sera moja tu ya kuhakiki nyaraka binafsi na za kitaasisi, kufanya teuzi na kutengua, kushika hapa na kuachia pale hata kabla hatujamaliza kukaza vema pale tuliposhika
Sijaona ukamifu kwenye lolote mpaka sasa... Tusifanye hosteli za chuo kama mfano na zile ndege kwakuwa maamuzi yake hayakuwa ya kitaasisi bali amri ya mtu mmoja tu.... Kuna walakini mkubwa utatokea huko mbele
Hili lililoibuka la wafanyakazi waliokuwa wanatumia majina ya wengine kufukuzwa kazi maramoja na kunyimwa haki zao zote litaleta janga kubwa mno... Tutegemee vifo vingi na familia nyingi kuyumba, tutegemee kuona watoto wa mitaani na machungodoa wezi na vibaka wakiongezeka... Maana watoto watafukuzwa shule kwa wazazi waliofukuzwa kazi kushindwa kulipa karo... HILI LITAZAMWE UPYA TAFADHALI.... wale wazee wenye nguvu hekima ya kushauri wafanye hivyo haraka .....
Yale yaliyoahidiwa wakati wa kuomba ridhaa ya kuongoza yatimizwe bila upendeleo bila kengeza bila jazba bali kwa hekima heshima na weledi... Kutumia nyaraka zisizo zako na kujimilikisha ni kosa la jinai na si mambo ya kitaaluma.. ....
Niishie hapa Kwanza

As a leader please deliver every promise.....without prejudice....!!?
Mkuu ubaguzi huu utaliangamiza taifa kwa kasi ya ajabu. Kutakuwa na matokeo mengi. Huwa nauliza hawa wanaofanya haya maamuzi wanaishi Tz au nje ya Tz wana ndugu jamaa majirani wakuwashauri au ni hofu ya ukoloni mamboleo?!! Tz si ile Mwalimu Nyerere aliiacha Tz imekuwa si ya wote Tz imekuwa ya kundi fulani Tz imejawa hofu Watanzania wameshikwa na mshangao Watanzania wanalia mioyoni Watanzania hawaijui kesho. Watanzania wamekuwa watoto wachanga tusiojua kitu. Uonevu makaripio dhuluma unyanyasaji umaskini ugonjwa vifo njaa ukiwa ni maisha ya Mtanzania wa leo! Ni Mungu tu ajuaye kesho yetu!!
 
rickshaw-car.jpg

Tanzania juu ya guta? Pls mambo yasiwe mengi tunaweza kujikuta siku moja tunatembelea mikono
 
Back
Top Bottom