Daaaaaaahh saudari umenikumbusha mbali enzi zile mi nilpewagwa mkwara tokea niko mtaani sijaanza form one,nilikutana na jamaa mmoja aliyakuwa form two na akajua kuwa nilikuwa nimechaguliwa pale shuleni kwao loooohh usipime kanipigisha bonge la mkwala afu nilivyoingia kwa shule sasa akakuta mi mwenyewe uso wa mbuzi,kiburi kama nimechanjiwa ilibidi jamaa akubali kushindwa na mpaka leo ni full heshima.
Aaah ligi mtindo mmoko. Unamjua mzee Mtambuzi wewe? Angekuja na huyo mwalimu mkuu angeipata fresh!
Okay mkuu nimekupata mi nikajua ulikacha oldonyo sambu seminari kwenye kazi ya utumishi
Swahiba si useme ukweli tu.
Haaaaaahaaaaaahaaaaaa swahiba naona sasa tunaelekea kuaibishana tu na ulivyo mkorofi sikuzote!sa niseme ukweli upi tofauti na huo niliousema?Afu nilikuwa na kiburi kwa sababu baba yangu alikuwa keshaniambia yeyote akinichikoza bila sababu atadeal naye perpendiculary kwa hiyo fulll makujiamini.
Ngoja nijinyamazie zangu.
Nakumbuka enzi hzo kuna njuka alikuja kuanza form one,tulimpa tocha za kufa mtu mpaka tukamvunja mkono, kumbe hatukujua ni mtoto wa Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mjini.
Unajua nini kilitokea....
Jibu unalo.
kama unatka kula bisi bisi za makalio jaribu kumfanyia mtu hizo mambo siku hizi bila kujali ni mdogo au mkubwa,ushamba nao ulichangiaHapo unakuta mbabe kakaa pembeni ndo anawaambia waite mvua mpaka ije, ole wake mvua isije ndo mtamtambua.
nakumbuka kuna dogo alikuwa bonge /njuka akawa anapiga mkwara eti babake kamanda wa polisi kinondoni kwa hakuna wa kumfanya kitu walimwagia urojo wa biogas usiku kama ndoo nane alivyoamka huo usiku hakurudi tena
Siku wanayokuja form one wote usiku wa manane lazima wakatwe mkia bweni zima kwa kutembezewa kipigo cha chaga na mikanda wakati taa imezimwa.
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
kwa tuliosoma kilimanjaro miaka ya tisini ilikuwa mkiingia wanafunzi mia moja baada ua likizo ya pasaka wanarudi hamsini wengine mambo yanawashinda.
Du sasa unamlaumu DINGI kwa kukupeleka Sekondari na kukuachia 200? je anekupeleka Sokoni akakufungulia kibanda cha kuuza nyanya kwa mtaji wa 2,000,000/ si ungeshazimaliza?We Dingi alikuwa noma balaa yaani alinipeleka mwenyewe halafu akaniachia tsh 200 pocket money yaani km mtu akupe shs alfu mbili leo hii ndo pocket money. Nikamwambia haitoshi akasema si unakula bure! Khaa kweli nilikonda mno term ya kwanza sikumaliza nikahama shule!
acha kabisa Asnam tena kipindi hicho unapata mama wa shule na baba wa shule ambaye ni mwanamke pia umfulie, umpigie pasi, umchukulie chakula akiumwa umuuguze na mshee ulivyotoka navyo kwenu lol sijui hata nlikua na akili gani jaman ila hofu tu ya shuleenzi za form one boarding miaka hiyo ilikua ni mateso sana sitaki kurewind mkanda kabisa naweza lia machozi hapa kwa jinsi nilivyosota loh ukizingatia nilikuwa mdogo jumlisha utoto sina hamu.