Mambo ya Zanzibari haya: Mkahawa au Mgahawa?

Mambo ya Zanzibari haya: Mkahawa au Mgahawa?

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,899
Reaction score
15,126
Haya tena,

Mambo kwa wenzangu na miye, hukoo kulikotokea Mapinduzi-Zenj!

Huu mgahawa upo airport nami nikashangaa unaitwa MKAHAWA. Kwetu siye mkahawa ni ule mti wenyewe wa kahawa.

Wale waswahili wa kunizidi nipeni maoni!
 
Na mti unaotoa matunda/mbegu zinazotengenezwa kahawa/coffee unaitwaje?

Kwani ajabu vitu viwili au zaidi vikawa vina neno moja?

Rejea kwenye maneno yafuatayo

1. Paa

2. Kaa

Kamusi linasema "mkahawa" ndio sahihi
 
Kutoka kwenye kamusi la Madan

Mkahawa, * n. mi- coffee-house, restaurent, cafe. Also sometimes heard as mgahawa

Kwa maana hiyo basi, "mkahawa" ndio Kiswahili sanifu

Ahsante
Kweli safiri uone mengi!!
 
Huku Zanzibar hata OFISI inaitwa AFISI....aahhaa ushanfahaamu vizuri
 
Angalia hapa; Tanganyika tunasema 'nilipoanza shule'. Wao ' nilipotiwa skuli''

Kunatofauti kwenye kiswahili chao na cha huku.
 
View attachment 100135
Haya tena , mambo kwa wenzangu na miye, hukoo kulikotokea mapinduzi-Zenj!

Huu mgahawa upo airport nami nikashangaa unaitwa MKAHAWA.
Kwetu siye mkahawa ni ule mti wenyewe wa kahawa.
Wale waswahili wa kunizidi nipeni maoni!!!

Kiswahili sahihi ni mkahawa na sio mgahawa. Ni pahala ambapo kahawa huwa inapatikana.
 
Back
Top Bottom