Mambo ya kuzingatia katika usafi wa jiko lako

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
MAMBO 10 YA KUZINGATIA KATIKA USAFI WA JIKO LAKO.

1. Hakikisha unasafisha jiko lako mara kwa mara kabla na kila baada ya kumaliza kupika. Usafi uwe wakina,futa sehemu zote kutoa vumbi na wakati wa kupiga deki piga kwa umakini kwa kusogeza v na kusafisha kila kona usifanye juu juu.

2. Jokofu pia ni sehemu ambayo ina ushawishi mkubwa sana wa bacteria ikiwa haina matunzo, hivy hakikisha unapitia mara kwa mara kuhakiki ni safi na imepangwa katika mpangilio sahihi. Panga bidhaa zako kwa mpangilio usirundike ili kuhakikisha usalama na kutunza uhalisia wa kila bidhaa,penda zaidi kuhifadhi mabaki ya vyakula katika kontena za mifuniko kabla ya kuhifadhi ktk jokofu ili kuepusha Muingiliano w harufu wa vyakula.

3. Panga jiko lako kwa mpangilio sahihi, hakikisha kila chombo kinakaa sehemu husika usiache vitu vinazagaa zagaa chini au ju ya jiko au counters bila mpangilio. Unapomaliza kupika basi jiwekee desturi ya kuondoa kila kitu na kurudisha pahala pake.

4. Jizoeshe kuwa na dustbin au mfuko wa kuweka taka jikoni wakati wa kupika. Zitupe takataka baada tu ya kumaliza upishi hata kama hazijajaa kisha osha na kausha vizuri dustbin yako.

5. Jenga desturi ya kufuta unapomwaga chochote kama vile maji,mchuzi ,mafuta, nk, usisubiri umalize kupika, uchafu utaganda na kuanza kujaza nzi na uzalishi wa bacteria. Hakikisha unafua vizuri kitambaa na kuani baada tu ya matumizi.

6. Osha vyombo, vifute na vipange sehemu yake husika kila unapotumia usisubiri vijae na kujaza nzi jikoni. Anika vizuri kitambaa baada ya kufuta vyombo na hakikisha unafua vitambaa vyako kila siku usiku, bora zaidi kufua na maji moto.

7. Tenga vibao na visu vya kukatia mboga mboga na nyama tofauti, nyama mbichi ina bacteria hivyo unapomix na matunda au mboga mboga unasambaza bakteria na kuiweka afya yako na familia yako rehani. Osha vibao kwa sabuni na Maji safi baada tu ya matumizi vifute vizuri kisha weka sehemu yake husika.

8. Mwaga maji machafu pindi tu unapomaliza kusafisha mboga mboga au nyama bila kusahau kusafisha mikono yako kabla ya kuanza kitu kingine.

9. Usiache vyombo vichafu wala mataka taka jikoni ,kabla ya kulala hakikisha umeacha jiko lako likiwa safi na katika mpangilio.

10. Zingatia usafi wako binafsi, wengi tunatabia ya kukurupuka unaamka tu na kukimbilia jikoni kabla ya kufanya usafi wa mwili wako kwa ujumla. Hakikisha unajikosha vizuri kabla ya kuingia jikoni,safisha mikono yako vizuri kwa sabuni,kabla ya upishi na baada ya upishi.
 
Back
Top Bottom