Mambo ya kumsifu Rais /Marais yanatokea wapi?

Wakati wa Mwalimu Nyerere hatukusikia wala kuona hivi vituko vinavyotokea siku hizi,hata alipokuja Ali Hassani Mwinyi, Mkapa na yalianza kuchomoza kidogo wakati wa Kikwete na yamekuwa na kukuzwa kupita mipaka kwa Hayati Magufuli na sasa ndio usiseme Raisi Samia akikohoa utaona kwenye vyombo vya habari amekohoa kwa mbwembwe, yaani sasa ni kusifia kwa kwenda mbele.

Hii tabia inawafanya hawa wachaguliwa kujiona wamekamilika na wanaweza kufanya wanalo taka kama tuonavyo, wakati wake Mzee Julius Nyerere ulikuwa huoni mihemko ya kusifiwa sifiwa, sijui kajenga hili kafanya lile mangapi ameyafanya katika nchi hii? Leo mtu akifungua choo basi makelele nchi nzima.

Inakuwa ile hadithi ya mfalme, tuacheni ujinga huu,mimi naona ni ujinga ,ushamba na kutokujielewa tunafanya nini na tunakwenda wapi, hii haina tofauti na ile tabia ijulikanayo siku hizi ya kujipitisha, wanaosifu wanasifu kila kitu alimradi na wao waonekane mwisho mtakuja kusifia ujinga.

Hii tabia imeanza rasmi baada ya ccm kuanza kuzidiwa dhahiri na vyama vya upinzani,hasa awamu ya mwisho ya JK. Hivyo wanaccm wakaanza kujenga tabia ya kumsifia rais ili kuonyesha ni mchapa kazi. Alipoingia madarakani Magufuli maana aliingia kwa uchaguzi kuchezewa, yeye akatengeneza vikundi vya propaganda kabisa ya kumsifia, hii ilienda sambamba na kuhakikisha wapinzani hawaruhusiwi kufanya siasa, na yeye hakosolewi. Eneo hili sukuma gang hawakutaka mchezo kabisa hadi wakawa mpaka wanateka, kuua na kubambikia kesi wanaomkosoa Magufuli.

Sasa tabia ile imeota rasmi mizizi ndani ya ccm. Kila rais akiingia anakuwa na genge lake la kumsifia. Kwa sasa Msoga line ndio wanaendesha kundi la kumsifia Mama. Kila hela ya umma ikitoka inaitwa ni ya mama Samia. Ila inflation iliyopo sio ya Mama Samia bali ni sababu ya vita vya Ukraine! Sababu hasa ya ccm kufanya hizi siasa za ghiliba dhidi ya umma, ni kwakuwa hawako madarakani kwa ridhaa ya wananchi, hivyo wanashurutisha kukubalika.
 
Rais wa nchi ni mtumishi wetu sisi Watanzania ndio tuliomuajiri kwa kura zetu, ndio tunaomlipa mshahara, kumlisha na kumvisha kupitia Kodi zetu.

Rais wetu ana pande mbili, kwa upande mmoja rais ni mtu taasisi, hana feelings wala hawezi kukosea, huyu ni mtukufu rais na pale Ikulu ni mahali patakatifu.

Kwa upande wa pili rais wetu ni binadamu, a human being, ameumbwa kwa nyama, ana hisia and has feelings and emotions na anasikia maumivu, anaumia or sometimes hata kulia.

The human part of her, akifanya vizuri, she needs appreciation, gratitude and encouragement. Hivyo kumsifu, kumpongeza, kumshangilia na kumfagilia ni poa tuu, Ila anapofanya vibaya, tumkosoe...

The same applies to Samia. Kwenye mazuri tusifu, yakitokea yakuhitaji ukosoaji, tukosoe kwa heshima, nidhamu na staha.
P

Ulimuweka ww madarakani kwa kura, ila uchaguzi wa 2020 haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Na kwa taarifa yako viongozi wa kiafrika ukiwakosoa kwa hiyo unayoita staha wala hawajali. Lakini ukiwakosoa kwa lugha kali ambazo wao na nyie wapambe wao huzipa tafsiri kuwa ni kutukanwa, lazima watatekeleza japo hubaki na uhasama,na sehemu kubwa hupiga marufuku ufanywaji wa siasa, hubambikia kesi wapinzani wao, huhujumu shughuli za kuwaingizia vipato wapinzani wao, huwateka hadi kuwaua. Tuna mifano hai ya haya tena hapa hapa Tanzania.
 
Lakini huyu kaajiriwa kwa katiba. Unaweza niambia alishinda kwa kura ngapi?
Alishinda kwa kura zilezile walizopata na Rais hayati JPM kwa sababu walipigiwa kura pamoja yeye akiwa ni mgombea mwenza !!
 
Alishindaje wakati tuliimizwa chagua ccm chagua magufuri na sio chagua ccm chagua samia?

Naomba idadi ya kura alizopata samia
 
Katiba ni ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Hiyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mali ya nani?. Mwenye JMT ndio mwenye katiba.
Sababu wewe ndio umesema rais anapigiwa kura ili kushika iyo nafasi.
Sio mimi ndio nasema, rais anapigiwa ili kushika hiyo nafasi, bali wenye katiba ndio wamesema, katiba ni andiko tuu, ili kuweka kumbukumbu, kuwa wenye katiba waliamua kumuajiri rais wetu kwa kumpigia kura ili ashike nafasi hiyo.
P
 
Alishindaje wakati tuliimizwa chagua ccm chagua magufuri na sio chagua ccm chagua samia?

Naomba idadi ya kura alizopata samia
Hapo ilikuwa lugha gongana !! Hakuna uchaguzi kama hakuna mgombea mwenza ! Tena awe wa kutokea upande wa pili wa muungano !! Hiyo ndio sheria na taratibu zinazofahamika, mengine huwa ni madoido tu na mbwembwe za kujimwambafai !!
 
Samia alikua mgombea urais au mgombea mwenza?

Je kura zinapigwa kwa mgombea mwenza au mgombea urais
 
Hua nasema, Uongozi wa magufuli umeonesha tuna viongozi wa namna gani....huyu mama ni muendelezo wa Kansa aliyoiacha yule roho mbaya.
 
Wakati wa Mwalimu Nyerere hatukusikia wala kuona hivi vituko vinavyotokea siku hizi,hata alipokuja Ali Hassani Mwinyi, Mkapa na yalianza kuchomoza kidogo wakati wa Kikwete na yamekuwa na kukuzwa kupita mipaka kwa Hayati Magufuli na sasa ndio usiseme Raisi Samia akikohoa utaona kwenye vyombo vya habari amekohoa kwa mbwembwe, yaani sasa ni kusifia kwa kwenda mbele.

Hii tabia inawafanya hawa wachaguliwa kujiona wamekamilika na wanaweza kufanya wanalo taka kama tuonavyo, wakati wake Mzee Julius Nyerere ulikuwa huoni mihemko ya kusifiwa sifiwa, sijui kajenga hili kafanya lile mangapi ameyafanya katika nchi hii? Leo mtu akifungua choo basi makelele nchi nzima.

Inakuwa ile hadithi ya mfalme, tuacheni ujinga huu,mimi naona ni ujinga ,ushamba na kutokujielewa tunafanya nini na tunakwenda wapi, hii haina tofauti na ile tabia ijulikanayo siku hizi ya kujipitisha, wanaosifu wanasifu kila kitu alimradi na wao waonekane mwisho mtakuja kusifia ujinga.
Njaa kali
 
Rais wa nchi ni mtumishi wetu sisi Watanzania ndio tuliomuajiri kwa kura zetu, ndio tunaomlipa mshahara, kumlisha na kumvisha kupitia Kodi zetu.

Rais wetu ana pande mbili, kwa upande mmoja rais ni mtu taasisi, hana feelings wala hawezi kukosea, huyu ni mtukufu rais na pale Ikulu ni mahali patakatifu.

Kwa upande wa pili rais wetu ni binadamu, a human being, ameumbwa kwa nyama, ana hisia and has feelings and emotions na anasikia maumivu, anaumia or sometimes hata kulia.

The human part of her, akifanya vizuri, she needs appreciation, gratitude and encouragement. Hivyo kumsifu, kumpongeza, kumshangilia na kumfagilia ni poa tuu, Ila anapofanya vibaya, tumkosoe...

The same applies to Samia. Kwenye mazuri tusifu, yakitokea yakuhitaji ukosoaji, tukosoe kwa heshima, nidhamu na staha.
P
we mzee hunaga kitu cha maana tena
 
we mzee hunaga kitu cha maana tena
Watu wote wanaanzaga hivi, kwanza siku wanazaliwa, wanakuja duniani wakiwa watupu, baadaye wanapata cha maana cha kufanya, na wakati wao ukipita, wanakuwa hawana tena kitu cha maana, na mwisho wa maisha, tunaondoka watupu na kurejea kule tulikotoka, kama tulivyokuja, na vitu vyote tulivyovipata kwenye dunia hii tunaviacha na kuondoka watupu kama tulivyokuja!.
P
 
Kusifia sifia sana kiongozi kunapunguza kuwajibika kwake...

Na sijui kwa nini huwa hawakemei kusifiwa sifiwa ilihali mambo wanayoyafanya ni sehemu ya wajibu wa dhamana walizopewa/pata...
 
Wakati wa Mwalimu Nyerere hatukusikia wala kuona hivi vituko vinavyotokea siku hizi,hata alipokuja Ali Hassani Mwinyi, Mkapa na yalianza kuchomoza kidogo wakati wa Kikwete na yamekuwa na kukuzwa kupita mipaka kwa Hayati Magufuli na sasa ndio usiseme Raisi Samia akikohoa utaona kwenye vyombo vya habari amekohoa kwa mbwembwe, yaani sasa ni kusifia kwa kwenda mbele.

Hii tabia inawafanya hawa wachaguliwa kujiona wamekamilika na wanaweza kufanya wanalo taka kama tuonavyo, wakati wake Mzee Julius Nyerere ulikuwa huoni mihemko ya kusifiwa sifiwa, sijui kajenga hili kafanya lile mangapi ameyafanya katika nchi hii? Leo mtu akifungua choo basi makelele nchi nzima.

Inakuwa ile hadithi ya mfalme, tuacheni ujinga huu,mimi naona ni ujinga ,ushamba na kutokujielewa tunafanya nini na tunakwenda wapi, hii haina tofauti na ile tabia ijulikanayo siku hizi ya kujipitisha, wanaosifu wanasifu kila kitu alimradi na wao waonekane mwisho mtakuja kusifia ujinga.
Elimu! Elimu! Elimu yetu ni duni kupindukia.
 
Samia alikua mgombea urais au mgombea mwenza?

Je kura zinapigwa kwa mgombea mwenza au mgombea urais
Ukipiga kwa Rais wa chama Fulani automatically umemchagua na mgombea mwenza wake ! Maana huwezi kusema nampigia kura yangu Rais tu , hiyo haiwezekani !!
 
Back
Top Bottom