Wakati wa Mwalimu Nyerere hatukusikia wala kuona hivi vituko vinavyotokea siku hizi,hata alipokuja Ali Hassani Mwinyi, Mkapa na yalianza kuchomoza kidogo wakati wa Kikwete na yamekuwa na kukuzwa kupita mipaka kwa Hayati Magufuli na sasa ndio usiseme Raisi Samia akikohoa utaona kwenye vyombo vya habari amekohoa kwa mbwembwe, yaani sasa ni kusifia kwa kwenda mbele.
Hii tabia inawafanya hawa wachaguliwa kujiona wamekamilika na wanaweza kufanya wanalo taka kama tuonavyo, wakati wake Mzee Julius Nyerere ulikuwa huoni mihemko ya kusifiwa sifiwa, sijui kajenga hili kafanya lile mangapi ameyafanya katika nchi hii? Leo mtu akifungua choo basi makelele nchi nzima.
Inakuwa ile hadithi ya mfalme, tuacheni ujinga huu,mimi naona ni ujinga ,ushamba na kutokujielewa tunafanya nini na tunakwenda wapi, hii haina tofauti na ile tabia ijulikanayo siku hizi ya kujipitisha, wanaosifu wanasifu kila kitu alimradi na wao waonekane mwisho mtakuja kusifia ujinga.