Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,459
- 872,114
MAMBO YA KUJUA KABLA HUJATEKWA
Dr. Albanie Marcossy, PhD.
Naandika kwa kutumia uzoefu wangu, ufuatiliaji na tathmini nilizozifanya juu ya maandiko mbali mbali ya kiusalama na matukio ya utekanaji Afrika Mashariki na Maziwa Makuu kwa Nchi za Tanzania, Kenya, Sudan Kusini, Congo DRC na Uganda. Pia narejea matukio ya uvunjifu wa amani nchini Burundi na Mauwaji ya Kimbari niliyoshuhudia maeneo ya Gitarama, na Southern Province yote nchini Rwanda 1994. Katika nchi hizi nilianza kufuatilia kutekwa na hatimaye kuuwawa na kutupwa porini Mwanasiasa Kiongozi Robert Ouko nchini Kenya. Nimefuatilia hata haya yanayotokea Tanzania sasa ikiwemo kupotea kwa watu, kuokotwa miili iliyotia mashaka kwenye fukwe za bahari na mitoni. Kutekwa, kuteswa na kuokotwa kwa watu kadhaa na hata madai ya kutekwa na kupotezwa watu kwenye maeneo yenye utata huko Kibiti, Mkuranga, Lindi na Mtwara. Niliishi pia kwa muda mjini Mtwara wakati wa sakata la gesi.
Na tangu hapo nilijifunza mambo mengi ambayo leo nazungumzia juu ya ushiriki wa vyombo rasmi vya usalama kwenye Utekanaji na matukio yanayoendelea nayo. Niwakumbushe tu kuwa nilifika Somalia 1991 nikitafuta kazi wakati nchi hiyo ikiingia kwenye machafuko na wakimbizi kuongezeka. Na pia nimepata nafasi ya kuitembelea nchi hiyo Mara kadhaa haswa eneo lililojitenga la Somaliland.
Mara zote nchi inapoingia kwenye sintofahamu na haswa tashwishi ya watu kupotea/ kupotezwa, kutekwa/kujiteka, kulazimishwa kukimbia makazi yao na hata kuikimbia nchi yao jamii inaingia WASIWASI NA WOGA. Amani hupotea na heshima miongoni mwa watu inalindwa moja kwa moja kwa mtutu wa bunduki. Fedha hutumika kununua silaha na kujenga vikundi vya kihalifu. Wenye fedha au silaha na wakati mwengine wenye ujuzi tu wa namna ya kupambana huunda makundi yao. Au hata kuwanunua watendaji wa vyombo vya usalama wawapatie ulinzi na kutekeleza mambo yao kwa namna yao.
Hapo ndipo makundi huhasimiana na au hata kupigana waziwazi. Makundi haya hutokana na nguvu kinzani au nje ya mfumo wa Dola au ndani yake kutokana na tofauti mbalimbali na maslahi ya watu.
Endapo kiongozi au viongozi wa ngazi zozote watatumia watendaji kuunda timukazi au vikosi rasmi toka ndani ya mfumo wa dola kutekeleza matakwa yao kuwateka, kuwapoteza au kuwatisha watu, tathmini na historia inaonesha kuwa vikosi hivyo na au watendaji hawa wakishang'amua kuwa wanafanya mambo ya maslahi kwa mtu na ni kinyume cha sheria na utaratibu wa kuendesha nchi, basi wao pia huunda timu zao ndani na nje ya timu za viongozi na kufanya mambo Yale yale kwa maslahi yao. Hii isichanganywe na zile kadhia ambapo watendaji wa vyombo vya usalama hufanya matukio ili kubadirisha au kushinikiza kiongozi mwenye maamuzi kufanya maamuzi wanayoyataka.
Inapofika hali hii, hapo sasa kuna njia kadhaa:
1. Hujiunda ndani ya kundi kuunga kundi dogo ambalo litaelewana zaidi na au kuwapiku wenzao kutenda matakwa ya Bwana Mkubwa, au kujitendea nao mambo yenye maslahi yao tu. Hawa nao huteka, kuua, kuumiza na au kutishia ili wapate watakacho bila kutumwa.
2. Watendaji walio nje ya makundi ya utekaji nao hujiunda makundi yao. Wakati mwengine hujiweka chini ya umiliki wa mtu au kiongozi hasimu na yule mtumaji wa awali. Hawa Mara nyingi hulipa kisasi.
3. Kundi Mchanganyiko. Hili huundwa na watendaji walio ndani ya makundi yaliyo endana na viongozi. Lakini pia hujumuisha watendaji nje ya wale kwenye makundi. Hawa ni hatari zaidi kwa kuwa hata malengo yao ni mchanganyiko. Wanapata taarifa za ndani kwa urahisi na huenda hata hufanya malipizi kwa kuwa wanajua kwa uhakika kinachotokea.
4. Makundi ya wastaafu na Raia. Haya ni makundi yanaundwa ili RAIA kujilinda. Haswa hutokea baada ya raia kujiridhisha au hata kuwa na mashaka kuwa vyombo vya Dola vinashiriki kuwateka au vimeshindwa kuwalinda. Makundi haya ni rahisi kudhibitiwa kwa kuwa wastaafu wengi wanayo mawasiliano na wanaweza kutumika na mfumo rasmi.
5. Makundi ya RAIA wenye hasira kali. Hawa huunda makundi yao VANGUARD. Liwalo na Liwe: Mbwai na inde Mbwai!! Pamoja na ujuzi mdogo walio nao lakini ni watu hatari sana kwa kuwa hujihisi wako sahihi na WANA haki ya kujikinga. Wakipata mwongozo watu Hawa ni hatari zaidi kwa Dola kwa kuwa hawana woga wa zana, Hawana woga kwa sheria na wala hawajui mipaka.
Makundi haya yote yameshashuhudiwa nchini Congo DRC, Sudan Kusini, Uganda na Somalia. Hivi karibuni nchini Kenya ilionekana dhahama ya Mungiki. Al Shaabab ni matokeo ya haya. Utahesabu sana: Islamic Courts, Mayimayi, Interahamwe, Mbandidu, Mabanda, Banyamulenge, na hata SUNGU Sungu wa Kanda ya Ziwa Tanzania walishaanza kuelekea huko. Katika nchi mbalimbali za maziwa makuu na mashariki, makundi mengi yamezagaa kwenye viwango mbalimbali.
Tunapata kujua kuwa: Kwa vyovyote iwavyo, ushiriki wa vyombo vya dola, iwe kwa kutumwa au kujituma, kwenye kadhia ya kupoteza amani ya RAIA na kukandamiza haki zao, huzaa matatizo makubwa kuliko nchi inavyoweza kutarajia. Watu wa kwanza kuathirika na kadhia hii ni Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Siasa, na Wafanya biashara wakubwa kwa wadogo. Uwezekano huwa Mkubwa sana kuundwa makundi yatayopinga uonevu huu; nayo yatatumia nguvu na mbinu kukabiliana na viongozi wanaoonea RAIA. Machafuko mengi tunayoshuhudia Afrika yanaanzia hapo. Maadui wa nje wanapata nafasi rahisi kabisa kuwapa mafunzo, silaha na pesa ili wafanyie malengo yao.
Kwa bahati njema matokeo ya kadhia hii huzaa ajira kwa raia. Machungu kwa kupoteza amani lakini mwisho wake mchungu zaidi kwa viongozi na wafanyabiashara.
Mwandishi wa makala hii amenusurika kwenye majaribio nane (anayoyafahamu) yanayofanana na utekwaji. Ametembelea na kutafiti kwenye nchi zote alizozitaja pamoja na kushirikiana na serikali na mashirika ya kiraia kwenye nchi hizo katika kuimarisha utawala bora na demokrasia.
Tujifunze. Ukijua haya kabla hujatekwa itakusaidia kujua kundi kililokuteka nawe ufanyeje kujinasua ukiwa hai.
Nakupenda ukiwa salama.
*Please share: kitisho hakijaisha!*
Dr. Albanie Marcossy, PhD.
Morogoro
7.11.2018.