SoC01 Mambo ya kufanya yatayo leta mabadiliko

Stories of Change - 2021 Competition

mcheza ngoma

New Member
Sep 2, 2021
3
1
Uchumi na Biashara
kama tutatengeneza mifumo bora dhidi ya wafanya biashara wadogo (Machinga na mama ntilie) tunaweza kukuza uchumi wetu pamoja na biashara. Mfano Serikali inapo anzisha miji inapo tenga maeneo kwa ajili ya masoko, shule ,hospitali, vituo vya mabasi, nyumba za ibada nakazalika itenge eneo kwa ajiri ya wafanya biashara hawa ili mji ukikua wawe na eneo lao maarumu, pia tutaweza kupunguza msongamano wa wafanya biashara hawa mababarani. kwa kufanya hivyi biashara itapanuka serikali itakusanya mapato na uchumi wa nchi utakua. Ongezeko kubwa la machinga lazima ligeuzwe kua fursa , fursa itakayokuza biashara pamoja na kuongeza uchumi wa nchi.

Afya
Nipende kuishauri jamii kurudisha mfumo wa maisha ya asili, Maisha ya asili yanaweza kutusaidia kuimalisha afya zetu pamoja na kupunguza ongezeko kubwa la magonjwa kama kisukari pamoja na shinikizo la damu(Presha). Mfano wa maisha ya asili ni pamoja na matumizi ya madawa asilia, kilimo bila kutumia mbolea zenye kemikali, uvuvi bila kutumia sumu na ufugaji bila kutumia madawa. Dawa hizi tunazo zitumia kwenye kilimo,uvuvi na ufugaji zimekua zikileta athari kubwa kwenye miili yetu, Watu wa zamani walikua na afya njema kwa sababu hawakutumia vyakula vyenye kemikali .

Maendeleo ya jamii
Maendeleo kwenye jamii zetu yataletwa na utawala bora, Utawala wenye kufuata misingi ya sheria , Haki na Katiba . Mfano matumizi sahihi ya mapato kutoka kwenye vyanzo mbalimbali ndiyo yatakayo pelekea ongezeko katika upatikanaji wa huduma za maji safi, umeme, zahanati, madawa, shule, barabara nakazalika. Rai yangu kwa wananchi kutumia haki yao kikatiba kuchagua kiongozi atakae leta maendeleo kwenye jamii zao.

Utawala bora na Uwajibikaji
Uondoshwaji wa sheria zinazo wakinga viongozi hasa wakuu wa nchi kutoshtakiwa kwa kuvunja sheria utaleta utawala uliokua bora. Viongozi wengi wamekua wakitumia vibaya madalaka yao lakini hawashtakiwi sababu kubwa ni sheria zinazo walinda, Kama tutaondoa sheria hizi kiongozi atakae tenda kosa au kutumia vibaya madalaka yake atawajibishwa kwa mujibu wa katiba. Na hapo ndipo tutakapo fikia malengo ya dhana ya utawala bora na uwajibikaji

Demokrasia
Demokrasia bora ni ile yenye uhuru, usawa na haki. Mfano Tanzania ili tuwe na demokrasia bora lazima tuhame kutoka kwenya mfumo wa demokrasia shirikishi kwenda kwenye mfumo wa demokrasia ya moja kwa moja. Mfumo wa demokrasia shirikishi huminya haki ya wananchi kufanya maamuzi hasa katika masuala yanao wahusu, Mfano sheria mpya zilizo tungwa kama tozo ya miamala pamoja na Kodi ya majengo kupitia manunuzi ya luku. Sheria hizi zimeleta athari kubwa sana wananchi hasa wenye maisha ya chini na laiti kama wangepewa nafasi ya kufanya maamuzi wasinge kubali sheria hizi zipitishwe na huo ndio mfumo wa demokasia ya moja kwa moja , mfumo unao toa nafasi kwa wananchi kufanya maamuzi kwa masuala yanao wahusu.

Kilimo
Sekta ya kilimo ni muhimili wa uchumi ndani ya nchi, Lakini wakulima wengi wameendelea kuwa masikini na sababu kubwa ni mifumo iliyo wekwa dhidi yao. Mfano mfumo wa bei elekezi kwenye mazao ya biashara kama korosho, karafuu, pamba, tumbaku, chai nakazalika umekua ukiminya haki ya haki ya mkulima kwenye uuzaji wa mazao. Wakulima wamekuwa wakipangiwa bei na serikali kupitia bodi mbalimbali bei ya kuuza mazao yao na ni kinyume na haki, Uwepo wa soko huru utaleta mabadiliko kwani mkulima ataweza kuuza mazao yake kwa bei na wakati anao utaka.

Sayansi na teknolojia
Uanzishaji wa Maabara hasa katika shule za msingi utaleta mabadiliko, Kwani wanafunzi wataanza kujifunza sayansi ya vitendo wakiwa madaraja ya chini kabisa na sio ile ya nadharia ambayo imekua ni kikwako kikubwa. kama serikali itaweza kutoa elimu au sayansi ya vitendo kwa kiwango kikubwa kuliko sayansi yanadharia itachochea upatikanaji wa wanasayansi mengi ambao watakuja kuleta mabadiliko kwenye sayansi na teknolojia.

Haki za binadamu
Migogoro ya kisiasa imekua ni chanzo kikubwa cha ukosefu wa haki za bunadamu kwenye mataifa mengi duniani. vita vya wenyewe kwa wenyewe au mataifa mawili tofauti vimekua ni chanzo cha ukosefu wa amani , uhuru wa watu kufanya kazi, kumili mali, kusoma pamoja na kuishi umekosekana na hizo ndizo haki zao za msingi. Umalizwaji wa migogoro hiyo utaleta amani, uhuru na haki.

lakini pia utambuzi mdogo wa haki za binadamu umekua ni chanzo cha ukosefu wa haki za binadamu, hasa kwa wananchi wale waliopo kwenye nchi zenye amani kama Tanzania. Elimu juu ya utambuzi wa haki za binadamu inabidi itolewe mijini pamoja na vijijini ilimradi watu waweze kuzitambua haki zao.

Mapenzi/ Mhusiano
Elimu ndogo ya mahusiano pamoja na mapenzi katika umri mdogo vimekua ni chanzo kikubwa cha kuvunjika mahusiano mengi hasa ndoa. Elimu ya Jando na Unyago inabidi itolewe kwa vijana wengi kabla hawajaingia kwenye mahusiano kama ndoa hatua hii itasaidia kudumisha ndoa .

Lakini pia ukomavu wa akili unahitajika ili kuweza kuhimili mikiki mikiki ya ndoa . Mahusiano mengi yatadumu kama wahusika watakua na vitu hivyi viwili yaani elimu pamoja na akili

Mwisho
Makala hii ndogo imeorodhesha mambo yatakayo chochea mabadiliko kwenye upande wa Uchumi na Biashara, Afya ,Maendeleo ya jamii, Utawala bora na uwajibikaji , Demokrasia, Kilimo, Sayansi na Teknolojia, Haki za binadamu pamoja na Mapenzi na mahusiano
 
Back
Top Bottom