saddyy
Member
- Dec 28, 2014
- 58
- 54
Mambo ya kufanya ili usimchoke mke wako;
1. Kuwa na ratiba maalumu ya kufanya tendo la ndoa na sio vurugu vurugu au kila wakati.
2. Mpendezeshe mkeo kwa mavazi na chakula bora kwani atakuwa na siha(afya) nzuri na hivyo kumona mpya.
3. Jambo la muhimu kuliko vyote ni maneno mazuri juu ya mkeo kwani humfanya awe mtulivu wa nafsi na atanawiri kwa kuridhika kwa maneno mazuri kutoka kwako na faraja unayompa na atakupenda kuliko kitu chochote.
4. Kumbuka kuwa upendo ni faraja ya maneno na kucheka na mkeo hata kama kuna jambo la kukutia hasira basi lifiche kwa mkeo na kama ni kuomba ushauri basi pia kwa upole.
5. Mfanye mkeo awe huru kukuambia anachopenda ili umridhishe, ilimradi tu liwe ndani ya uwezo wako.
6. Msifanye mapenzi kila mara, mtachokana.
7. Mwanamke unapomletea zawadi hufurahi sana kuliko kumpatia hela akanunue zawadi. aliyemletea mkewe mtandio wa sh 10,000 na aliyempa mkewe 50,000 akanunue kitu chochote. basi aliyeletewa mtandio atakuwa na faraja zaidi.
8. Kumbuka kuwa mwanamke ni kama mtoto mdogo, hupenda sana kudeka na hasa ukijua kudekeza na atakupenda sana ukifanya hivyo.
9. Uaminifu ndiyo kitu bora baina yenu, na uaminifu huja kwa kufuata dondoo za juu hapo.hizo ndizo siri za nyinyi kudumisha upendo wenu na hata mkiishi miaka 100 lakini mtaonana wapya siku zote.