HUO ndio ulimbukeni tulioiga kwa wakenya lakini sisi wa tz asili yetu twaamini kuwa binadamu wote ni ndugu tutajuanaje tusipoanza kusalimiana ukiimbiwa habari za jioni ukajibu salama unapungukiwa nini au aliyekusalimia unakuwa umemwongezea nini?. Acheni hivyo huwezi kujua nani atakufaa wakati wa dhiki. Vijana wawili walianza kukorofishana kwenye gari na kurushiana matusi ya nguoni kwenye gari alikuwemo Sajenti wa JKT akaamua kuwapeleka Polisi walipoulizwa particulars zao kumbe wote babu yao ni mmoja ambaye anaishi BAGAMOYO KWA HIYO KWA namna moja ama nyingine sisi sote ni ndugu
Ulimbukeni ndio huo wa kutaka kusalimia kila unayekutana nae! Eti kuwaiga Wakenya; kwani Wakenya ndo nani?! Watu wanatembea na mambo yao kichwani huku wengine wakiwa wana-digest mambo ya msingi...watu wakiwa katika state kama hiyo, we unaanza "habari za leo...!" Then, wht next?! Kusalimia tu; basi?! Kama unanisalimia ili uniulize jambo (kama unazani ni lazima kufanya hivyo), then fine lakini kunisalimia tu bila la ziada ni upuuzi! Utasalimia wangapi na utaitikia salamu za wangapi?! Unakuta mtu umetulia kwenye daladala tulii, hakujui humjui anaanza kukuongelesha tena kwa stori zisizo na kichwa wala miguu...; huko ni kupotezeana muda bana....!! u can't share stories with some1 u don' know his/her interests! By the way, uzoefu unaonesha kwamba ukikutana na mtu akaanza kukusalimia kwa adabu zote, kinachofuata hapo ni mzinga wa "niongozee nauli" utafikiri ni wewe ndie ulimleta hiyo sehemu!! Wengine ni wezi na matapeli tu....anatafuta namna ya kukuzoea ili akulize! madogo nao siku hizi hawajambo; ukisikia "shikamoo..!" kinachofuata hapo...."naomba shing mia!" All in all, unanisalimia ili iweje?! Kama ni kusalimia tu, basi...then utasalimia wangapi?!