Mambo ya kiungwana ambayo mtu akiyafanya huonekana wa ajabu machoni pa wajinga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo ya kiungwana ambayo mtu akiyafanya huonekana wa ajabu machoni pa wajinga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by IrDA, Mar 2, 2012.

 1. IrDA

  IrDA JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Jamani kuna mambo ambayo ni ya kistaarabu kabisa lakini mtu akiyafanya huonekana mshamba machoni pa wajinga na hata kuchekwa.Leo nimepanda daladala kutoka kariakoo kuelekea mbezi,kwakuwa ilikuwa jioni daladala lilikuwa limejaa kiasi.

  Sasa daladala lilipofika kituo cha fire likasimama akaingia dada mmoja hivi kama wa miaka 25.Dada yule akasalimia,"habari za jioni jamani",mimi na watu wengine wachache wakajibu. Ila kilichonishangaza abiria wengine watu wazima kabisa wakaanza kumcheka na wengine wakisema eti yule dada anatafuta bwana,wengine eti jini,wengine eti mshamba wa kuja.

  Kwa kweli niliwashangaa sana kwani niliona salamu ni kitu cha kawaida.Tulipofika big brother yule dada akashuka, ila kabla ya kushuka akamshukuru dereva na kisha kondakta.Safari hii karibia basi zima wakaangua kicheko,na wengine wakisisitiza na kurudiarudia maneno waliyosema mwanzo.

  Akya nani walinikasirisha na kunishangaza sana,nikaona bora nilianike wazi hapa jf labda wapo watu wanaoyachukulia mambo haya kama ya ajabu au ushamba yaani 1.kusalimia uliowakuta kwenye daladala pale uingiapo,au hata aliyekaa pembeni yako angalau
  2.Kumshukuru dereva pamoja na konda kwa huduma waliyokupatia hata kama umelipia

  Jamani tubadilike watanzania,tusifanye vitu kwa mazoea tu....
   
 2. Bakulutu

  Bakulutu JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 1,895
  Likes Received: 313
  Trophy Points: 180
  sisi watu weusi..basi tuu..NASHUKURU NDUGU.sitakubali kuwa kama wao!
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Mara nyingi miji husababisha uungwana na taadhima kushuka. Kwa hiyo mtu "aliyelelewa vizuri" akifanya alichofundishwa kuwa ni jambo la heshima, waliopunguziwa taadhima na misukosuko ya mji humuona "mshamba".
   
 4. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kumsalimia "SHIKAMOO" mtu aliyekuzidi umri maeneo kama Mlimani City,Bank,na Hotel maarufu duuuh...utaonekana kama unaomba msaada...
   
 5. S

  Sikwepeshi Senior Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Teh teh teh me napita tu!!
   
 6. D

  DOMA JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Jingine ni kuwahubiria watu neno la Uzima
   
 7. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2012
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ama kweli huu mji unakua. Hata ushoga ni fasheni. Natamani nimuona huyo dada mstarabu. Watanzania tunapenda kuiga mabaya na kuyatukuza mazuri tuliyokua nayo sasa ni ushamba. Ah jamani.!!!!!!!!
   
 8. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  he he he ustaarabu zero kwa waafrika
   
 9. OPTIMISTIC

  OPTIMISTIC Senior Member

  #9
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Watu wengi upendelea mazoea. Lakini mbona wauza madawa na sabuni mabasi ya mikoani hatuwashangai?
   
 10. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Hata ukifanya kazi na ukashika nafasi nyeti bila kuiba_unaonekana mshamba.....na hii ndio nchi tunayoishi...hatari sana.
   
 11. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Mnh! Kwa hilo hata mimi namshangaa.....hata wewe ukinisalimia wakati mimi sikujui; nitakushangaa tu!! Si hivyo tu, nitajiuliza kwanini umenisalimia....na kama hiyo siku nimeamka vibaya, am sure; nitakumaindi tu!! Ukija ofisini kwangu ukanisaalimia; nitakuelewa coz' nafahamu unahitaji huduma lakini tumekutana barabarani; hunijui sikujui halafu unaanza habari za salamu...sio siri, nitakuwa alerted!
   
 12. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Dar hovyo,unamuuliza mtu njia anakudanganya upotee,sijuhi atafaidi nini nikipotea. Hii ya kutosalimiana mwanzoni nilidhani ndio u-born town,kumbe ujinga tu. Huku mikoani mtu anasalimia gari zima,tabasamu usoni hata kama ni tarehe 19 ya mwezi. Siku inakuwa safi.
   
 13. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  Haahaa,umenikumbusha siku moja kariakoo nilipomuuliza mzee mmoja wa makamo hv anielekeze mtaa wa nyati, yule mzee akanionyesha mtaa flani na kuniambia "nenda mtaa huu moja kwa moja huko utaona Nyati,simba,swala, twiga,pundamilia chui na kila kitu" huku mzee yuko serias, yaani nilichoka hata kuuliza tena! Wabongo c watu!!!?
   
 14. R

  RUTARE Senior Member

  #14
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HUO ndio ulimbukeni tulioiga kwa wakenya lakini sisi wa tz asili yetu twaamini kuwa binadamu wote ni ndugu tutajuanaje tusipoanza kusalimiana ukiimbiwa habari za jioni ukajibu salama unapungukiwa nini au aliyekusalimia unakuwa umemwongezea nini?. Acheni hivyo huwezi kujua nani atakufaa wakati wa dhiki. Vijana wawili walianza kukorofishana kwenye gari na kurushiana matusi ya nguoni kwenye gari alikuwemo Sajenti wa JKT akaamua kuwapeleka Polisi walipoulizwa particulars zao kumbe wote babu yao ni mmoja ambaye anaishi BAGAMOYO KWA HIYO KWA namna moja ama nyingine sisi sote ni ndugu
   
 15. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Heshima ni kitu muhimu sana,mtu kusalimia uliowakuta kwa sisi waislam tunasema hayo ni mafundisho ya mtume wetu alitufundisha,unapowakuta watu kwanza watolee salam,salam ni uungwana na ni ishara ya malezi mazuri,lkn wabongo sisi kama tumerogwa kupenda vya wazungu tu,
   
 16. COURTESY

  COURTESY JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 2,018
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  hahahaha huyo mzee burudani sana,wazee wa mjini utawaweza
   
 17. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Kwa tabia yako hiyo nahisi hauwezi kuomba msaada wa aina yeyote na kwa mtu yeyote yule duniani! Kusalimiwa imekuwa nongwa tena!
   
 18. Angel Nylon

  Angel Nylon JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 4,471
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Huku kwetu Znz naona bado ipo2 ingawa naamini baada ya muda itatoweka mana naanza ona dalili nafkiri kwa sababu ya mchanganyiko, wakuja washakua nusu bin nusu na wenyeji.
   
 19. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  kuna mtu aliwahi kuuliza kituo cha magari ya Muhimbili maeneo ya Kariakoo, akaambiwa ajitupe barabarani atafikishwa Muhimbili bila kulipa senti tano! Dar watu wana stress sana, ndo maana muda wote wamenuna.
   
 20. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,088
  Likes Received: 7,315
  Trophy Points: 280
  Kushabikia Chama ni Uungwana tu,
  But kushabikia CCM zama hizi ni Ujuha!!!!!!!
   
Loading...