Mambo ya Jinsi na Jinsia Yanavyotazamwa Katika Jamii ni Makosa

Nundu_Tanzania

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
811
349
Mambo ya jinsi na jinsia tangu kale yamekuwa mambo ya tafiti nyingi. Kwa karne nyingi mambo ya jinsi na jinsia hayakuwa yanaeleweka wazi.

Kuna mitazamo mbalimbali katika jamii kuhusu mambo ya jinsi na jinsia. Katika jamii nyingi mambo ya jinsi na jinsia yanadhaniwa kama mambo yaliyobuniwa na watu fulani kwa malengo yao fulani fulani ambayo, hatahivyo hayaelezwi hayo malengo ni yapi!

Jinsi ni maumbile ya mtu kuwa mume au mke. Tunazaliwa watu waume na watu wake. Hii iko hivyo na inabaki kuwa hivyo, ndio jinsi.

Jinsia ni majukumu, ni shughuli ambazo hawa watu wa jinsi ya kiume na kike wanatekeleza; mgawanyo wa kazi. Jinsi ya kiume inafanya kazi hizi na jinsi ya kike inafanya kazi hizi, ndio jinsia.

Suala la jinsi kwa lenyewe bila kuacha mambo yote ya unyanyasaji, hasa jinsi ya kike katika jamii ambazo bado hazijamjua Mungu, halieleweki wazi.

Kwa jinsi tunapata jinsia; mgawanyo wa majukumu yaani kazi unategemea kwa kiasi chote jinsi.

Mwanamume na mwanamke hawa wote wana hadhi sawa. Lakini hawajaumbwa kufanya majukumu sawa. Wote mume na mke wameumbwa na kuletwa duniani kufanya kazi. Lakini kuna mgawanyo wa kazi kati ya mume na mke.

Majukumu aliyonayo mtu mwanamume hayawezi kuchukuliwa na mtu mwanamke. Namna hii ya mwanamume na mwanamke kuwa na mgawanyo wa majukumu siyo jambo lililobuniwa na mtu au kikundi cha watu, lakini ni jambo la akili.

Nature; asili imemweka mume kuwa hivyo alivyo na mke kuwa vile alivyo. Hawa wawili wanahitajiana lakini kamwe mwanamke hawezi kuchukua nafasi ya mwanamume na mume naye vivyo hivyo.

Akili imewafanya mume kuwa na majukumu haya na mke kuwa na majukumu haya. Hivyo yasieleweke na yasichanganywe na unyanyasaji na dhuluma wanazotendewa jinsi fulani.

Masula ya uchimi kwa mfano, akili imemfanya mtu mume kwa ajili ya uchumi sawa ambavyo imemfanya mtu mke kwa ajili ya malezi. Hii maana yake ni kwamba anayeandaa mfumo wote wa uchumi na maisha ni mtu mume ambaye hatahivyo, hawajibiki tu kuandaa mfumo wa maisha, lakini zaidi kufundisha mfumo huo kwa mtu mke ili utekelezwe.

Mtu mke siyo tu kwamba ni wa muhimu lakini kwa kweli ni wa lazima katika maisha.

Mtu mke ni msaidizi wa mtu mume hivyo ni wa muhimu na wa lazima hivi kwamba kile mtu mume anakifikiri, anaandaa, anabuni na kukifanya hakitaweza kuwa cha manufaa kama mtu mke hajafundisha na kushirikishwa inavyokubalika kiakili.

Ni muhimu kufahamu hatahivyo, kwamba ubongo wa mwanamke na mwanamume unatofaitiana katika kufanya kazi. Kwa sababu hiyo tusichanganye na kuelewa kama mtu mume anaweza kuchukua nafasi ya mtu mke naye mtu mke anaweza kuchukua nafasi ya mtu mume.

Mwanamume lazima atambue ana wajibu na majukumu makubwa, makosa yanayoweza kuwa ya kutokuelewa, ujinga na uvivu, kwa vyovyote vile hayahalalishi mwanamke kuchukua nafasi ya mwanamume.
 
Back
Top Bottom