We Sex, acha ujuha jibu hoja za Lawi. Kikubwa alikuuliza, kwanini mmelemewa au kuzidiwa na vitoto vya kisomali huku mnajiita super power?
Kwamba, uchumi wa nchi upo mikononi mwa wachache mnoo, kwamba kuna gap kubwa kati ya walionacho na wasionacho?
Kwamba; kama sio resources za Tz, mfano mbuga za wanyama na chakula Kenya si mngekufa njaa?
Kwamba, Tanzania haiko tu vizuri ktk ulinzi wa ndani bali hata katika kupigania usalama na ulinzi wa nchi zingine km DRC dhidi ya wavamizi kutoka Kigali na Kampala
U-super power wa Kenya unaozungumzia ni upi??
Yaani ninyi kwa kiherehere kujitia mnajua kila kitu mnaongoza duniani...
Kama ujuha basi wewe ni juha yule mfalme, yaani wewe mtu akiongea positive khs kenya ni mkenya, kuhusu uganda ni mganda,nk kwa taarifa yako mimi mtanganyika asilia,
Ni wapi kuna vita ya kenya na somalia?! Kwa akili yako itakuwa kuhusu wale wahuni, majambazi, magaidi alshabab! Ngoja nikufundishe, wale ni wahuni tu kama wahuni wengine, US super power la dunia kilitokea nini Boston marathon?! Hapa kwetu pale Arusha watu wameuwawa kwa milipuko sehemu tofauti tofauti.
Uchumi mikononi mwa wachache?! Huo ndo ubepari wenyewe ambao ndo unatawala dunia, ujamaa ulishindwa. Hata US, China, india na hapa bongo mambo yako hivyohivyo.
Kufa njaa?! Nadhani umeropoka bila kufikiri, hizo mbuga za wanyama hata zikifungwa leo hakuna atayekufa na njaa kwa sababu ya mbuga za wanyama iwe kenya ama tz, kuna nchi kibao zipo bila mbuga za wanyama lakini hawafi kwa njaa, kwanza kenya yenyewe ina mbuga za wanyama, eti bila chakula cha tz kenya wangekufa njaa?! Hapa umeandika kipuuzi kabisa, ni sawa na mtu wa kijijini kuandika bila chakula chetu nyie wa mjini si mngekufa njaa wakati hapo hapo amekamilisha nyumba ya kisasa na kulipia watoto school fees kwa pesa ya kuuza mazao mjini, hii ni ajabu kwelikweli. Kila siku wakulima hapa nchini wanalalamikia serikali iwatafutie soko la mazao yao soko likipatikana mfano kama huko kenya wakulima wanafurahi ni kuongeza juhudi za uzalishaji cha ajabu mswahili kama wewe ambaye hata haulimi unakuja hapa eti bila mahindi yetu wangekufa njaa!! Ulilima wewe? Unajua maana ya kilimo cha biashara wewe? Hicho chakula tz ilitoa bure? Haya ngoja nikusaidie maarifa ni kwamba kuzalisha na kuuza ndani na nje ndo siri ya maendeleo ya uchumi, uliza china.
Kwamba tanzania ikoje?! Kwa nini umetaja tanzania na kuisifia tu! Au kwa akili yako ndo super power wa EA?! Usalama gani upo tanzania kama ndege ya kijeshi inaweza kutua na kubeba wanyama huku wanausalama wanakoroma katika usingiz mzito, kama askari anaweza kualisha raia alipuliwe na anapewa zawadi ya cheo, kama raia anatekwa, kuteswa na kuwataja wahusika lakini hakuna hatua inayochukuliwa, mabomu kwenye nyumba za ibada na mikutano ya siasa, viongozi wa dini kumwagiwa tindikali na kuuwawa hadi FBI wakaja hapa, hivi tumeshindwa kulinda tembo wetu tutaweza kulinda wakongo? Ule ni uhuni wa viongozi wetu, wanaiba tu pale congo.
Usuper power uko wapi?! Kama kawaida huku uswahilini hawajui haiti wanajua US, kule mbele hajui dar wala kampala wanajua nairobi, kenya.
Nairobi ni kati ya malango makuu ya kuingia africa, kenya ina uchumi mkubwa kuliko nchi yoyote EA, kenya sasa sio nchi ya dunia ya tatu ni nchi ya kipato cha kati, kenya ndo inaongoza kwa kuexport miongoni wa nchi za EA, nilikuwa napata shida sana kuset saa yangu nikichek time zone sioni dar wala dodoma kwa EA nilikuwa naona nairobi tu ndo naselect (nilikuwa), huwa naangalia sana vyombo vya habari vya kimataifa hususani utabiri wa hali ya hewa nakodoa sana macho nione hali ya hewa ya hapa kwetu lakini mara nyingi naambulia nairobi, kiukweli ni super power ya EA