Mambo ninayotamani tuyarekebishe

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,515
11,277
Kuna baadhi ya mambo, ama Tabia kwenye Jamii yetu ambazo kiuhalisia hazina Afya kwa mustakabali wa Nchi yetu Kiuchumi, Kijamii, na wala kimaendeleo.

Ni mengi, lakini kwa uchache nimeweza kuyawaza haya na iwapo Serikali yetu na Sisi Raia kwa ujumla wetu tukijitahidi kuyarekebisha naamini tutaijenga Tanzania Bora na yenye matumaini kwetu na vizazi vyetu vijavyo;

1. Natamani Shule Binafsi hapa nchini ziache hii Tabia ya kulazimisha Watoto wadogo wakae (Bwenini) Boarding kwa hoja ya kuwaandaa na Mitihani.

Ni kama Utaratibu unazidi kukomaa miongoni mwa Shule nyingi za Binafsi kulazimisha Wazazi na Watoto kuwa Mtoto akifika Madarasa ya Mitihani (Yaani la Nne na la Saba) basi ni lazima mtoto akae Bwenini ili apate muda mwingi wa Kusoma na kujiandaa na Mitihani.

Na Mzazi ambaye hataki ni aidha akubali kumpeleka Mtoto wake saa 12 Alfajiri na kwenda kumchukua saa mbili za usiku. Nimejiuliza masaa yote 14 Mtoto anakuwa anafundishwa tu? Muda wa yeye ku refresh anaupata wapi?

Sikatai, huenda ni Jambo zuri; lakini kwa Umri ule ninahofu kuwa Mtoto anapaswa aendelee kuwa Chini ya Uangalizi wa Wazazi wake. Maana Mashuleni kuna hatari ya kuchota tabia zisizofaa kwakuwa bado akili haijakomaa vizuri.

2. Natamani Serikali ilazimishe wamiliki wa Shule Binafsi kuwa na Sport facilities kabla ya kuwapatia Kibali cha kuanzisha Shule. Binafsi ninaamini sana kwenye Physical activeness ya Watoto na ule muda wa Mapumziko wawe wanautumia kwenye kucheza zaidi na kuchangamka kuliko ilivyo sasa.

Nimeshuhudia baadhi ya Mashule; Siku za Ijumaa pekee ndiyo huwa siku za Michezo, na hubeba wanafunzi na magari ili kuwapeleka kwenye Viwanja kwa ajili ya michezo. Naona muda mwingi watoto wanautumia kwenye Basi kuliko hata Uwanjani kwenyewe.

Kuhusu hizi Shule Binafsi; natamani sana kuwe na vigezo sahihi vya uanzishwaji wake ambavyo vitakuwa na manufaa kwa Watoto, Wazazi na Nchi kwa Ujumla wake. Natamani sana Serikali Iboreshe mazingira ya Utoaji elimu kwenye shule za Serikali ili kupunguza utitiri wa Shule Binafsi ambazo hazina viwango. Maana elimu inageuka Biashara badala ya Huduma..

3. Natamani sana Mazingira ya Biashara hapa nchini yarahisishwe na Utolewaji wa Vibali na leseni za Biashara yaboreshwe kwenye Mamlaka zetu za Kiserikali, inaumiza sana moyo kuona Mfanyabiashara analazimia Kwenda Manispaa kupata Leseni na Service Levy kwa nyakati Tofauti, kisha Kodi TRA, Fire Certificate Idara ya Zimamoto, TBS, TMDA, OSHA, BRELA n.k n.k..

Natamani sana hizi compliance ufanyike Utaratibu wa kumwezesha Mfanyabiashara aweze kumaliza kwenye Ofisi Moja ama walau Mbili tu kuliko kutengeneza mazingira magumu yanayochochea Rushwa maana inakuwa ngumu kwa mtu kumudu mizunguko yote hiyo.

4. Natamani sana ule Utaratibu wa Zamani ambapo mtu akitaka kuoa ama Kuolewa basi yeye na Familia yake wanashikamana na kufanikisha shughuli yao, kwa uwezo wao bila kulazimika kuomba omba Michango ambayo kwa namna moja au nyingine inapelekea migongano na hasira pindi mtu asipokuchangia.

5. Natamani sana Serikali ione umuhimu wa kuunda Sheria inayokataza Mifugo kutembea holela kwa kigezo cha kutafuta malisho. Na badala yake kila Mfugaji alazimike kuwa na eneo litakalomudu kulisha Idadi ya mifugo aliyo nayo. Na utaratibu uliopo sasa wa Kuingiza mifugo kwenye mapori tengefu na kwenye mashamba ya watu wengine ukomeshwe kabisa.

Movement ya Mifugo iwe ni ndani ya eneo miliki ya Mfugaji husika pekee. Na akitaka kuwahamisha kutoka eneo moja kwenda jengine iwe ni kwa Utaratibu maalum na ikiwezekana atumie chombo cha Usafiri.

Ninaamini kwa kufanya hivi itasaidia kurejesha uoto wa asili na kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na movement holela za Mifugo. Pia itamaliza tatizo za migogoro ya mara kwa mara baina ya Wakulima na Wafugaji.

6. Tutaendelea
 
Naona Kenya wameamka Usingizini kuhusu hili suala la Watoto wadogo kuwekwa Bweni.
 
Back
Top Bottom