Mambo ni mazito sana kwa Dkt John Magufuli...

Mambo ni mazito sana kwa Dkt John Magufuli...

Namuamini sana Rais Magufuli na dhamira yake kwa nchi yetu. Naamini ndoto yake kubwa ni kuibadilisha nchi ili iweze kupiga hatua na kuheshimika. His vision is clear. Bahati nzuri ana uthubutu na sio mtu wa kubabaishwa na yeyote.

Lakini, bila shaka anacheza vibaya siasa zake. Mwenyewe anasema yeye siyo mwanasiasa lakini sio kweli. Huwezi kuongoza nchi usiwe mwanasiasa. Huwezi kuongoza chama cha siasa halafu usiwe mwanasiasa. Hizo ni political statements tu. After all, we are all political animals.

Amevuruga watu. Wafanyabiashara. Matajiri. Wahisani. Wanasiasa wenzie na wanahabari.

Pengine anajua kuna waovu humo humo na ana taarifa zao nyeti, lakini hao mpaka wamefikia hapo sio wajinga. Mtu mwenye pesa ana nguvu. Kumkabili kunahitaji akili zaidi kuliko kiburi hata kama uko sahihi. Hili ni funzo.

Kikwete alionekana mjinga aliposema mafisadi wakiguswa bila tahadhari nchi itatikisika. That was an ugly but very honest opinion. Tunayaona sasa. Shida siyo kupambana nao, bali unapambanaje?

Namshauri Dkt. Magufuli apaki kiburi chake. Asigombee tena 2020. Atafute wataalamu watakaochezesha vizuri maneno ili aonekene shujaa kwa uamuzi wa kuamua kupisha. Sio lazima aondoke kwa aibu. Tunajua kusamehe. Tutamsamehe na kumpongeza kwa kujaribu.

Vinginevyo, anaweza kuwa the worst president ever. Japo kwangu he remains the best - in faith.
Another fisadi uliyezibiwa mianya ya upigaji. Eti asigombee 2020. Are you serious kweli? mzee baba imekula kwako utatubu sana hamna cha maana ulichoongea hapo JPM unaye bado mpaka 2025 so jiandae kisaikolojia. Fanya kazi hamna tena pesa za magumashi.
 
Mkuu 2030 hafiki, anajikaza tu lakini pale alipo amenyoshwa na system vibaya mno.

Great depression imemkuta baada ya Ripoti ya CAG, mkulu anaziba huku, watu wanatoboa kule.
Hii sio kweli. Ni sehemu ya upotoshaji.

Yeye ndie anachungulia Hazina kuna nini, anachota na kupeleka ambako Bunge halijaelekeza!

Ukiukwaji wa taratibu zilizowekwa hauweza kumwacha salama anayekiuka na kufanya aonavyo mwenyewe.
 
President Magufuli might achieve some goals but not all.Its difficult and cumbersome situations especially when the government is out of cash.
 
Wana falsafa wamenena na kusema kuwa ' will au testament ' ya mtu hufanya kazi vizuri zaidi baada ya yeye kutangulia katika haki.
Mambo anayofanya Mh. Rais kwa sasa ni will ya kwake, itaonyesha maajabu na kuleta manufaa makubwa baada ya yeye kumaliza muda wake wa kikatiba kuongoza Inchi.
Manabii na mitume hawakueleweka wanachofanya mpaka walipoondoka hapa Dunuiani. Watawala wa wakati wa wakati ule waliwaua lakini watawala wa sasa wanawaamini na kuyafuata mafundisho yao.
Kila kitabu na zama zake, sisi wa kizazi hiki tuwe wavumilivu na wenye kuvuta subira ili kitabu hiki kitumike hadi wakati wake utakapokwisha.
Naamini kizazi kijacho kitampa Rais wa sasa sifa kubwa na kumwona kama Kiongozi maarufu Afrika kuwahi kutokea.
Rais moja Kaburu wa South Africa aliwahi kufanya utafiti kuhusu Mwafrika Mweusi wakati anafanya PHD yake na kuainisha kuwa kwa kusema " The most intelligent black African can't think beyond one year".
Tuombe maoni kwa wenzetu wanaoweza kufikiri kwa muda wa zaidi ya mwaka moja.
 
Yaani unaleta utani kwenye ushauri wa maana kama huu? Nimegundua hamumpendi Magufuli na hamjali mambo gani yatamtokea huko mbeleni kwa mwendo (reckless) anaondesha hili gari.
Kwenu nyie ya Mugabe, Bashiri nk you don't care kwa sababu kwa sasa ndio mnatafuna zile anazosema CAG hazionekani?
 
Mkuu tunakushukuru sana kwa kukubali kuwa Rais wetu ana nia njema kabisa na Taifa letu.

Basi kwa moyo huo huo wa kusema ukweli tunakuomba kura zako kwake 2020, ili aendeleze hayo mema aliyoyaanza.
 
Hata huyu alidharau ushauri Leo wale alio watupa gerezani ndio wamempokea na kumnyoa nywele
kwinyara___BwapgkWAdVA___.jpeg
 
Mafisadi mnalialia subir dawa iwaingie.

hospital zinajengwa Kila wilaya

Treni Za mwendo Kazi hizo
Ndege zinaruka kila mkoa
flyover hizo
umeme wa uhakikia waja

Nk

Mafisadi kamata sweka ndani
 
Alianza vizuri sana ila aliharibu alipoanza kuchuja nani walimnyima kura....kimara bomoa,mwanza acha,hakuna ajira koz wanachuo walinizomea .....
 
Ccm ,wanahamisha magoli ,hata kama mada ,ikiwa ya kujenga wao wapo kama mbuzi
 
Kwa akili ya haraka haraka tu, tena ndogo, unavyoona Jiwe ni wa kuondoka 2020? Huyu tunaye mpaka 2030!! Mark my words!!
...............Mkuu 2030 hapana bana ni 2025,mbona unataka kuleta balaa aisee?
 
Back
Top Bottom