Mambo muhimu ya kufanya katika maisha

May 29, 2020
30
24
Habari zenu wakuu leo nitatoa mambo muhimu ya kuzingatia katika maisha yako

1) UKARIMU.
ukarimu ni jambo dogo sana kwa kulitamka lakini ni jambo lenye mzizi mkubwa katika matumizi.

2)KUJALI.
Kujali sio lazima kuwa na pesa lakini jambo la kujali linaweza kukufanya uinuke katika maisha na sio kukuingiza pesa lakini jambo la kujali linaweza kukupa maarifa kutoka kwa mtu uleyemjali kwa wakati huo.

3)SUBIRA.
subira ni njema zaidi na subira unapaswa kuiweka kwa kila jambo kwani subira hufanya kazi ya kuupa nguvu moyo pamoja na mafadhaiko yako.

4)HESHIMA.
heshima haitumiki kutoka kwa mdogo kwenda kwa mkubwa pekee na heshima sio salamu pekee bali heshi hutumika kwa watu wa lika zote na jinsia zote yaani jambo la kuheshimu kila mtu litakufanya uonekane mwenye muonekano wa maana mbele ya jamii.

5)MANTIKI.
Hili jambo linahusika katika maongezi namaanisha maranyingi katika maongezi unapaswa kutumia mfumo wa IQ ili kuongoza maongezi na utaonekana mwenye busara kwenye jamii.

Imeandikwa na: mfalme
 
Back
Top Bottom