Mambo mengi ya kujifunza kwenye mlipuko wa Beirut

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,161
10,882
Japo Rais Trump amesema mlipuko wa Beirut ni kitu maalum kilichopangwa lakini waLebanoni wenyewe wanaamini imetokana na shehena ifikayo tani za ujazo 2750 za Ammonia nitrate iliyotaifishwa tangu mwaka 2013 kwenye meli iliyotoka Urusi kuelekea Msumbiji.

Mtu mmoja wa Beirut mji ambao umezoea milipuko kutokana na vita anasema amesikia milipuko mingi lakini huu wa safari hii hajawahi hata kuudhania kuwa unaweza ukatokea kutokana na kishindo chake ambacho kimesababisha hali kama ya tetemeko la ardhi mpaka maaneo ya mbali na Beirut.

Afisa mmoja aliyeteuliwa kuiongoza bandari hiyo iliyoegeshwa meli hiyo baada kujua hilo alichacharika sana kuandika barua za ya 6 ngazi za juu kwa miaka kadhaa kila anapoona hajasikilizwa kutaka shehena hiyo iondolewe haraka bandarini hapo kwa usalama wa bandari na mali zilizopo.

Cha ajabu kutokana na mazingira ya rushwa jambo lililokithiri Lebanon shehena hiyo kwa amri ya mahakama ikapakuliwa kwenye meli na kuhifadhiwa kwenye ghala hapo hapo bandarini na bila uangalizi maalum.

Nahodha wa meli hiyo iliyoitwa Mv Rhosus baada ya kuzuiwa bandarini na kwa kujuwa shehena iliyokuwemo aliomba aruhusiwe kutoka haraka na mabaharia wake.Hatimae baada miezi 6 na kwa msaada wa wanachama wa ubaharia wakaruhusiwa kupanda juu.

Inawezekana wale wanaoijuwa ammonia nitrate wakaamua kufanya uovu na pia inasemekana mlipuko ulitokea wakati mafundi wa kuunganisha vyuma walipokuwa wakiendelea na kazi zao karibu na ghala hilo.
Kwa vyovyote vile mlipuko huo umekuwa mkubwa na kupelekea maafa ambayo hayajawahi kushuhudiwa nchini humo.

Watu wanaotajwa kufa ni 135 na watu 5000 kujeruhiwa. Maduka ya kuuza dawa ya jiji hili yamepewa ruhusa ya muda ya kuhudumia wagonjwa kutokana na hospitali kuzidiwa na majeruhi. Hali hii inalingana kwa mbali na hali ilivyokuwa Hiroshima mwaka 1945.

Inawezekana idadi za waathirika zikawa kubwa sana kuliko hapo kwani meli bandarini zimeteketea na majumba ya ghorofa makubwa yameanguka yaliyo karibu na bandari.Maghala yaliyokuwa na mali za kila aina yamebomoka na mengine kuwa majivu.Ratiba za safari za meli na kazi za kila aina jijini hapo.

1596744793562.png
 
nafikiri walikuwa mbali na eneo kishindo na mlipuko ulikoweza fika

Aiseeeh nimejiuliza tuu, kwa uharibifu uliofanyika hiyo inahesabiwa kama natural calamity au man made calamity?

Na insurance company zitahusika na compensation ya uharibifu uliofanyika kurejesha hali kama ya mwanzo kwa mali na huduma zilizokatiwa premium insurance?

Au ndo jumuiya ya madola itoe misaada kerejesha hali kama ya zamani? Je serikali yao ina mfuko wa dharura wa maafa?
 
Japo Rais Trump amesema mlipuko wa Beirut ni kitu maalum kilichopangwa lakini waLebanoni wenyewe wanaamini imetokana na shehena ifikayo tani za ujazo 2750 za Ammonia nitrate iliyotaifishwa tangu mwaka 2013 kwenye meli iliyotoka Urusi kuelekea Msumbiji.

Mtu mmoja wa Beirut mji ambao umezoea milipuko kutokana na vita anasema amesikia milipuko mingi lakini huu wa safari hii hajawahi hata kuudhania kuwa unaweza ukatokea kutokana na kishindo chake ambacho kimesababisha hali kama ya tetemeko la ardhi mpaka maaneo ya mbali na Beirut.

Afisa mmoja aliyeteuliwa kuiongoza bandari hiyo iliyoegeshwa meli hiyo baada kujua hilo alichacharika sana kuandika barua za ya 6 ngazi za juu kwa miaka kadhaa kila anapoona hajasikilizwa kutaka shehena hiyo iondolewe haraka bandarini hapo kwa usalama wa bandari na mali zilizopo.

Cha ajabu kutokana na mazingira ya rushwa jambo lililokithiri Lebanon shehena hiyo kwa amri ya mahakama ikapakuliwa kwenye meli na kuhifadhiwa kwenye ghala hapo hapo bandarini na bila uangalizi maalum.

Nahodha wa meli hiyo iliyoitwa Mv Rhosus baada ya kuzuiwa bandarini na kwa kujuwa shehena iliyokuwemo aliomba aruhusiwe kutoka haraka na mabaharia wake.Hatimae baada miezi 6 na kwa msaada wa wanachama wa ubaharia wakaruhusiwa kupanda juu.

Inawezekana wale wanaoijuwa ammonia nitrate wakaamua kufanya uovu na pia inasemekana mlipuko ulitokea wakati mafundi wa kuunganisha vyuma walipokuwa wakiendelea na kazi zao karibu na ghala hilo.
Kwa vyovyote vile mlipuko huo umekuwa mkubwa na kupelekea maafa ambayo hayajawahi kushuhudiwa nchini humo.

Watu wanaotajwa kufa ni 135 na watu 5000 kujeruhiwa. Maduka ya kuuza dawa ya jiji hili yamepewa ruhusa ya muda ya kuhudumia wagonjwa kutokana na hospitali kuzidiwa na majeruhi. Hali hii inalingana kwa mbali na hali ilivyokuwa Hiroshima mwaka 1945.

Inawezekana idadi za waathirika zikawa kubwa sana kuliko hapo kwani meli bandarini zimeteketea na majumba ya ghorofa makubwa yameanguka yaliyo karibu na bandari.Maghala yaliyokuwa na mali za kila aina yamebomoka na mengine kuwa majivu.Ratiba za safari za meli na kazi za kila aina jijini hapo.

View attachment 1529336
Mi nikajua umeorodhesha hayo mambo sasa
 
Mi nikajua umeorodhesha hayo mambo sasa
Kamlipuko kadogo tu walebnan mnapiga kelele, waulizeni wenzenu Japan ( Hiroshima & Nagasaki ) watu waligeuzwa majivu na athari zake mpaka Leo bado zipo,watoto wanao zaliwa hapo wengi wana outism( usonji).

Nuclear sio ya kuchezea
 
Baada ya silaha za nuclear kupigwa ban Sasa super powers wataamia kwenye amonia nitrate,
Nafikiri Hilo lilikua jaribio kuona namna gani inafanya kazi
Kwani ata miji ya Hiroshima na Nagasaki ilipopigwa na mabomu ya nuclear haikuwahi kutumika hapo kabla kwahiyo marekani moja ya lengo lao ni kujua ina impact kiasi gani nuclear inapotumiwa kwenye milipuko
 
Umetiririka na hadithi nilitegemea mwisho uainishe Mambo ya kujifunza kutokana na Hilo tukio Kama kichwa Cha habari kinavyoeleza.
 
Kilichonishangaza ni vile watu walianza kurekodi video kabla ua mlipuko mkubwa walijuaje kuwa jambo hilo lingetokea? Au ulianza mlipuko mdogo ndipo wakaanza kurekodi? Maana mwanzoni kabisa unaonekana moshi ukifuka kabla ya kishindo
Ulianza mlipuko mdogo. Lakini siku hizi watu wanapenda kurekodi kila wanacho kiona.

Kwahiyo hata hili lilitarajiwa.
 
Back
Top Bottom