Mambo matatu ya kurekebisha ndani ya CHADEMA

Ukishasema propaganda basi huna haja ya kuzikimbia ila kuzikabiri, ni ajabu kubadiri mlengo wako ambao uko sahihi kwa wakati husika kisa kuepuka propaganda ambazo hupikwa kwa kuzingatia wakati
 
Mbowe hawezi kukubali kabisa wachezee chama chake.

Lakini jambo la kufurahisha pro-Chadema taratibu mnaanza kujitambua.

Chadema wapo kama FIFA ukipeleka kesi mahakamani ni niko halafu wanajiita chama demokrasia.
Nivema kujua Katiba ya chama inasemaje maana ndio chombo cha mwisho kimamuzi na si matakwa ya mtu yoyote nilazima katiba tuheshimu kwani imewekwa kwa mamlaka yakisheria hakuna aliyejuu ya katiba

Arnold Ringo
 
Huu nao ni ujinga sana,vijana hebu kuweni makini na vishauri vya kipumbavu. Bora kuchelewa jangwani kuliko kufika na watu wepesi kama nyie na mnaoweza kucheza ngoma bila kujua mpigani amekaa wapi........yaani ukubali mpinzani wako akupangie jambo kisa watasema????? Ukiumia unamfuata tu wala haina shida wala upungufu
 
Ukishasema propaganda basi huna haja ya kuzikimbia ila kuzikabiri, ni ajabu kubadiri mlengo wako ambao uko sahihi kwa wakati husika kisa kuepuka propaganda ambazo hupikwa kwa kuzingatia wakati

Katiba ya chama imejieleza na ipo wazi kabisa sioni kuna haja yoyote ya kubishania hapa maana siyo mahali pake
 
Unaweza kuwa na mawazo mazuri lakini tatizo ni kwamba una hisia kuliko facts. What matters is to have the systems and processes that are manageable to remain on course na si kuangalia matukio. CCM imekuwa inarespond kuangalia public mood na nafikiri majority being like vultures term limit usije ukafikiri wanaifurahia. Lazima inawaumiza na ndio maana wamemeteka kila mfumo wa kisiasa ili wabaki madarakani. Kuondoa term limit kwa CHADEMA ni process iliyowekwa na haikuwekwa blindly kwamba mtu mmoja aliamka akaota ndoto nzuri na kuondoa kipengere hicho. As we criticize it CCM cannot be our bench mark at all maana mfano mzuri toka CCM hautufai. Halafu unataka mabadiliko kwa kuangalia sura za watu na wanakotoka na nafikiri bado unaweza kuegemea tofauti zingine na kidini, kijinsia na kiumri. Kama mabadiliko yanatakiwa it should not be a quick fix programe lazima kuwa na brainstorming na research then we can make due conclusion
 
Hivi wewe unafikiri watanzania wanaohongwa kanga na vitenge wana uelewa kama wako?

Kuna ugumu gani wa kufanya hayo mabadiliko?

Tusitoe mwanya wa propaganda kwa mambo ambayo si ya lazima na yanayoweza kuepukika.

Acha hizo ndugu yangu, jitafakari sana na hizi kauli zako unazotoa leo hapa... Na ndiomaana nikataka kujua leo umeamkia wapi Kaka??

Hivi kwasababu kuna watanzania wanaokubali kuhongwa kanga kwasababu ya uelewa wao (Kwa mujibu wa maelezo yako) Basi namimi nikubali kuhongwa hizo kanga ili tuende Sambamba.... Come oooooon Kamanda....!!! Hivi uko sawasawa leo??

Mara kadhaa Chadema imewaaminisha hao wananchi wanaopokea hizo kanga kwamba "Waendelee kupokea kwa wingi hizo kanga then linapokuja suala la Kura wapige Chadema. Na sote tumeona madhara ya ELIMU hii husasi hapa Tdm. Siwezi hata siku moja mimi ambaye ni Muelewa (kwa mujibu wa maelezo yako) Kumshawishi mtu ambaye si muelewa kula MAVI wakati mimi natambua kwa uhakika kwamba huo ni uchafu na kwamba ukitumia uchafu huo moja kwa moja unapata kipindupindu na aghalabu itakupelekea KIFO.

Salary Slip jirudi kamanda wangu, leo umekengeuka pakubwa sana (Samahani kwa kusema haya hakika sioni neno lingine la kutumia)

Khaaaaaaaaaaa......!!!!!!!

Tusitoe mwanya kwa propaganda kwa mambo yanayoweza kuepukika... Wewe jamaa wewe!!! Tambua hapo ulipo umepewa mdomo,macho,masikio na kubwa kuliko yote umepewa Ubongo, ni jinsi gani utatumia hiyo ni juu ya Ubongo wako na mdomo wako...!!! Kamwe huwezi kuzuia propaganda, maadam wewe ni mwanasiasa na uko kwenye siasa... Propaganda ni lazima utarushiwa tu taka usitake na wakati mwingine waweza kujipanga kujibu hii ikaibika ile.. Kama huna msimamo thabiti utaishia kutangatanga tu bila mwelekeo wowote... Huwezi kumpangia mtu cha kusema, maadam mdomo na ubongo anavyotumia ni vyake wewe piga kazi tu na wenye kuelewa wataelewa na wasiotaka kuelewa kwa makusudi watabakia hivyo (Kamwe huwezi kumridhisha kila mtu)

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Asante kamanda na umemaliza ndio maana watu wanakuwa wagumu kusoma katiba alafu wanakimbilia humu

Arnold Ringo
 

Salary umepotoka yaani unashauri kucheza jinsi propaganda zinavyoelekeza
 
Japokua umejita wewe nimwanachadema na nilikua nakuona humu ndani ukipambania chama lakini nimeanza kukutazama kwa jicho la tato jitafakari kama hayo uliyoyandika yana Afya kwa chama?

Kamanda Arnold Ringo mimi Msimamo wangu juu yawasaliti wa chama sitawakopesa nitawambia ukweli tuu, nilishasema hapa kuna rangi za watu wanaojita makamanda kumbe ni bendera fwata upepe na ndio ambao ccm wanawatumia sana kwa ulafi wao wa madaraka na uchumia tumbo Zitto amepata stahili zake alivyokitendea chama na ukipanda maharage utavuna maharage na si mchicha tunawatafuta baado wasaliti wengine na ninaelekea kuziangalia Rangi zao

Chadema Kwanza
 

Kamanda nimeshaona machua kwenye Mchele tutaendelea kuyapembua hatutavumilia usaliti wala hatutafumbiana macho. Asanteni sana

Chadema Kwanza
 
Last edited by a moderator:
Propaganda kama hizi ni useless katika nchi ambazo elimu ya urai iko juu na watu wake wengi wana elimu ya kutosha.

Hapa kwetu ni tofauti na ndio maana watu wanarubiniwa kwa kanga na vitenge.

Kitu cha kushukru kwa sasa ni uwepo wa UKAWA ambao kwa kiasi fulani unaweza kusaidia ku-neutralize hizi propaganda.

Tuache kupuuza haya mambo kwani yamekuwepo kwa muda mrefu sasa.
 
Jitafakari sana kwa hizi kauli je wewe unafa kuitwa Mwanachadema?
 
Last edited by a moderator:
Salary Slip sintoshangaa kama hili ni bandiko lako, nishakutazama kwa tahadhari muda mrefu sana, mguu nje mguu ndani
 
Last edited by a moderator:
Salary Slip

Una Mawazo Mgando sana Ndugu.
Kama vp na wewe nenda ACT kama unaona Chama hakina makazi bora kwako
Salary Slip leo naona unakumbana na mihemko ya wanachadema ambao hawataki kusikia hata siku moja wakikosolewa, iwe kwenye vikao ama nje ya vikao. Ona sasa sikutegemea mtu kama wewe ambaye umetoa mawazo mazuri lakini umeanza kushambuliwa.
 
Last edited by a moderator:
Serikali ikiondoa ruzuku tu kwa vyama vya siasa,Hayo yote uliyosema yanaweza fanyika na demokrasia ukaiona.Lakini kama pesa zipo za ruzuku na za wafadhili kwenye chama hayo unayoshauri ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.Unataka kukatiza ulaji wa watu wewe,shauri yako watakutimua kama walivyomtimua Zitto.

Mchaga siku zote anatafuta hela sasa Mbowe kaona kwenye chama kuna hela wewe unamwambia achia.Yuko tayari kufia hapo kwenye hela. Utaondoka wewe unayemwambia achia.
 

Hapa ndio sehemu sahihi kwenye pakusema? Soma kadi yako ya uwanachama au rejea katiba

Chadema Kwanza
 

Ningekuwa ni mwalimu ningekupa alama hasi maana sioni ulichoshauri. Propaganda umeambiwa ni kitu kinachokua na kinabadilika hata afadhali ya upepo. Hivi ni katiba gani inayoweza kuzuia negative propaganda who aim is to put people off track? Umeambiwa zimeanza propaganda za chama cha Wachaga, mara cha Wakristu, mara cha ukanda, mara ugaidi na sio kesho watakuja na nini. Hivi ni katiba gani ambayo inaweza kuwa anti- propaganda. Sidhani kama ipo maana bianadamu naweza kuwa distractive kuliko maelezo. Kinachotakiwa na Chadema ni kueneza elimu yenye dhamira njema hata kwa wana CCM. Dhamira nzuri ndio silaha kubwa sana . Katiba na vilivyomo ni kijaribu kuweka discipline. Disciplie peke yake haitoshi na ndio maana watu wabaya katika historia walikuwa na katiba zenye nishamu ya hali ya juu lakini kwa sababu walisahau roho(dhamira) waliishia/wameishia kuleta maangamizi dunia. Hitler, Musolini walikuwa na katiba na majeshi yenye nidhamu. Walichoiachia dunia ni maangamizi. Alcaeda, Alshababu, Bhoko Haramu, Hezbolla, ISIS na nyinginezo zina katiba na sharia kali ambazo wafuasi wanazitii lakini angalia maangamizi yao katika dunia. Tusijidanganye kuwa CDM inaweza kuwa na katiba isyo mawaa inachotakiwa ni kuongea sauti ya watu na kusikia sauti ya moyoni mwa Watanzania
 
te teh teh ama kweli nimeamini misukule iko mingi

Heri mimi ni msukule wa wanamageuzi kuliko wewe msukule wa Lumumba ambaye hata mfukoni buku 2 hauna lakini mabwana zako wanagawana bilion 200 kwenye viroba tena wengine wanatumia milion 10 kununua mboga huku ukibakia mpuuz kama wewe huna hata hela ya kununua chips kavu.

UKOMBOZI KWANZA DEMOKRASIA BADAE
 
Usitegemee hata siku moja kuona propaganda chafu dhidi ya CDM zitaisha,, hiyo ndiyo hali halisi ya siasa za upinzani hapa nchini. Utabadilisha kila kitu lakini as far wewe ni mpinzani na kadidri siku zinavyokwenda unakubalika kwa wananchi, ndio propaganda chafu, fitina na kila mbinu chafu kutoka ccm zitakuandama. Kuepukana na hayo, ni pale tu CDM itakapo dhoofika kama vyama vingine vya upinzani, ambavyo imebidi vitegemee kudra za ccm.
Siasa za upinzani ni mapambano, tena makubwa kwelikweli, hayo mabadiliko yote unayosema ni mbinu za adui, wala hakuna kasoro yoyote, na hata ukibadilisha hakuachii kirahisi, ataibua yote ya kabla ya mabadiliko kama silaha yake mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…